Jumatano, 16 Safar 1446 | 2024/08/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kesi ya Kisiasa Inafichua Uungaji Mkono wa Denmark kwa Uvamizi wa Mauaji ya Halaiki

Serikali ya Denmark inaendelea na uungaji mkono wake wa dhati kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza, ambayo yameitia hofu kila nafsi adhimu katika sayari hii, na kuwaamsha watu kuona kwamba vima vinavyodaiwa vya dola za Magharibi vimezikwa na maiti hizo za maelfu ya wanawake na watoto chini ya magofu ya Gaza. Haki za binadamu, haki ya kuishi na kujiamulia, haki za wanawake na ustawi wa mtoto - yote haya yanatupwa chini ya tingatinga la Uzayuni na wanasiasa na mamlaka, ambao kwa hivyo wanaonyesha unafiki wao wa hali ya juu na kufichua jinsi gani "vima" hivi kivitendo ni ala tu za kisiasa.

Soma zaidi...

Kuwekwa Kizuizini kwa Sababu ya Majadiliano Tu ya Hadhara kuhusu Kanuni za Shariah ya Kiislamu katika Demokrasia Kubwa Zaidi Duniani

Mamlaka za polisi kutoka jimbo la Tamil Nadu nchini India zimeripoti kuzuiliwa kwa Waislamu sita kwa kufanya amali za Hizb ut Tahrir (HT). Watu hao waliokamatwa ni pamoja na Dkt Hameed Hussain, ambaye ana shahada ya uzamifu ya Uhandisi Mitambo, Baba yake Hussain Ahmed Mansoor na kaka yake Abdul Rehman ambaye ni Msomi wa Kiislamu na wengine watatu, Mohammed Maurice, Khader Nawaz Sherif na Ahmed Ali.

Soma zaidi...

Pongezi za Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1445 H

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu, wenye kulemewa na majeraha na kustahamili shinikizo la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la kikoloni. Kwa mnasaba huu, tunawataja makhsusi watu wetu wenye subira mjini Gaza Hashim na kwa jumla katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tukimuomba Mwenyezi Mungu azifanye siku za Idd hii kuwa chanzo cha utulivu wa nyoyo zao.

Soma zaidi...

Mauaji ya Nuseirat Yanafichua Dini ya Ukafiri Na Yanafichua Ufadhili na Uungaji Mkono wa Marekani kwa Umbile la Uhalifu

Mnamo tarehe 8 Juni 2024, umbile la Kiyahudi lilifanya mauaji ya kutisha katika kambi ya Nuseirat katika Ukanda wa Gaza kwa usaidizi wa Marekani kwa kisingizio cha “kuwaokoa wafungwa 4” wanaozuiliwa na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (Hamas) na kuwakomboa kutoka mikononi mwake.

Soma zaidi...

Pongezi kwa Mnasaba wa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd

Maumivu yetu yanazidi tunaposhuhudia jinai hii kwa macho yetu wenyewe, huku majeshi ya Umma wa Kiislamu yakibaki bila kuchukua hatua yoyote, yakiwa hayana mwelekeo wa kuwasaidia ndugu zao wanaodhulumiwa. Vilio vya wafiwa na machozi ya watoto haviwasumbui, na majeshi haya bado hayajibu kwa sauti ya juu kabisa “Labbaik Allahumma Labbaik” katika kuitikia mwito wa Mola wao wa jihad na kuwanusuru Waislamu wanaodhulumiwa. Je, udhaifu na udhalilifu umefikia kiwango hiki?

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan Yawapongeza Waislamu Wote kwa Mnasaba wa Idd al-Adha na Inasisitiza Umoja wa Sherehe za Kidini kama Kanuni ya Sharia!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inatoa pongezi na salamu za dhati kwa Waislamu wote duniani kote kwa mnasaba wa Idd ul-Adha. Vile vile tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) azikubali swala, ibada, mapambano na mihanga ya Waislamu wote kwa Rehema zake na aikubalie Hijja yao.

Soma zaidi...

Watawala wa Pakistan wanatekeleza Ukamataji ili Kuzuia Hizb ut Tahrir Kutaka Kuhamasishwa kwa Jeshi la Pakistan Kuinusuru Gaza. Badala ya Kushambulia umbile la Kiyahudi, Watawala Wanawashambulia Waislamu

Huku Mayahudi wa Kizayuni wakivuka mipaka yote katika ukatili wao, wito wa kampeni ya kisiasa ya Hizb #ArmiesToAqsa umefika kila barabara na kila kona, kwa Fadhila za Mwenyezi Mungu (swt). Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali, viongozi wa kisiasa, wanaharakati wa mitandao ya kijamii na umma kwa jumla sasa wote wanazidi kuimba, “Enyi Majeshi ya Waislamu, nendeni Palestina, nendeni Palestina.”

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu