Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
H. 27 Jumada I 1442 | Na: 02 / 1442 H |
M. Jumatatu, 11 Januari 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuhusu Tangazo la "Kifurushi cha Kupambana na Ugaidi" Nchini Austria
(Imetafsiriwa)
Mabadiliko ya kisheria yaliyopangwa na Serikali ya Kurz ni ukiukaji mpya wa kanuni ya ulinzi wa wachache, ambayo inawakilisha wajibu wa maadili au wa kidini ambao tamaduni tofauti zimetambua kwa jumla kwa lengo la kuhakikisha uhai wa vitambulisho tofauti. Shambulizi hili la serikali ya muungano linahatarisha msingi wa mshikamano kati ya Waislamu na wasio Waislamu nchini Austria na linashajiisha mtindo hatari wa mzozo wa kihadhara ndani ya jamii.
Mnamo Disemba 16, Waziri wa Mambo ya Ndani Karl Nehammer, Waziri wa Haki Alma Zadic na Waziri wa Uwiano Susanne Raab waliripoti kwamba Baraza la Mawaziri lilikuwa limejumuisha kifurushi cha "kupambana na ugaidi" kwenye ajenda yake, ambayo ingewekwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura. Mabadiliko haya ya kisheria yatashughulikia nyanja zote za kimahakama na za utendaji, "na haswa kile kinachofikiriwa kuwa uwanja wenye rutuba ambapo maoni yenye msimamo mkali yamenawiri." Waziri Raab alisema: "Lengo ni kupambana na Uislamu wa kisiasa na popote ambapo mfumo ilio kinyume na Magharibi, maadili msingi ya demokrasia na utawala wa sheria umeenea." Kifurushi hiki ni pamoja na mambo yaliyopangwa hapo awali kama vile kuunda sajili ya maimamu, kurekebisha sheria ya 2015 juu ya "kuzuia ufadhili wa kigeni," kupanua Sheria ya Kukataza Nembo na Mashirika, na kuanzisha Sehemu ya 247B kama kifungu kipya katika Kanuni ya Jinai, ambayo inaangazia kushtaki na kuadhibu "msimamo mkali wa kidini". Waziri alisema kuwa hatua zilizomo kwenye kifurushi hicho zinalenga, kwa jumla, kukabiliana na kuenea kwa mifumo yenye itikadi kali, ambazo hufanya "uwianishaji wa watu nchini Austria" kuwa mgumu zaidi na hivyo kupelekea "ghasia na ugaidi".
Yaliyomo kwenye kifurushi cha "kupambana na ugaidi" yanaonyesha kuwa serikali ya muungano inalitumia shambulizi la 2 Novemba kama kisingizio mwafaka cha kuamsha ajenda yake ya uoanishaji wa lazima, ambayo inakusudia kuwaoanisha kamilifu Waislamu wanaoishi Austria. Ijapokuwa neno "Uislamu wa kisiasa" halitumiki tena wazi wazi na limebadilishwa na maneno ya jumla ya "msimamo mkali wa kidini", taarifa za Susan Raab zinafichua ni nani anayekusudiwa na Kifungu cha 247b cha Kanuni mpya ya Jinai. Lengo kuu la sheria hii ni "kupambana na Uislamu wa kisiasa na misikiti (yenye msimamo mkali) ya Kiislamu ambayo hueneza mawazo hatari chini ya pazia ya haki za kimsingi," alisema. Kwa hivyo, kubadilisha jina katika sheria inayopendekezwa sio chochote ila tu ni ujanja wa kisheria kufinika maumbile yake ya kibaguzi na kuepuka kushindwa kupya mbele ya Mahakama ya Katiba. Mnamo 11 Disemba 2020, mahakama hii ilisema, wakati ikitoa uamuzi juu ya Sheria ya Kuzuia Khimar (hijab) katika Shule za Msingi za Austria: "Kuangazia dini fulani au mtazamo fulani wa maisha [...] haiendani na kanuni ya kutoegemea kokote.”
Mbali na taarifa zilizo wazi zilizotolewa na Waziri wa Uwiano, waraka unaoelezea rasimu ya mawaziri unaonyesha wazi kuwa kusudi la sheria hii ni haswa kupambana na wanaharakati wa Kiislamu. Dhana ya msimamo mkali wa kidini, kama ilivyoelezwa kwenye waraka huo, "mara nyingi hupatikana katika uwanja wa Uislamu" (yaani Uislamu wa kisiasa), ambao kimsingi umejengwa juu ya "kukinai kwamba Uislamu haudhibiti tu masuala ya kibinafsi pekee, bali pia jamii na maisha ya kisiasa, hata kwa uchache.” Maelezo haya yanathibitisha kuwa kuletwa kwa kifungu cha 247B kama kifungu kipya katika sheria ya jinai inalenga kuunda mfumo wa kisheria wa kuadhibu ukinaifu wa kiakili kwa kila mtu, ili yeyote anayejaribu "kuzuia uwazi (yaani uoanishaji) wa Waislamu katika jamii hii aweze kushutumiwa. " (kutoka Ripoti ya Afisi ya Ulinzi wa Katiba na Kupambana na Ugaidi ya 2018).
Njia hii ya kupindukia na ya upande mmoja ya serikali ya Kurz ni mshtuko mkubwa kwa uhusiano kati ya jamii za Waislamu wanaoishi kihalili nchini Austria na dola ya Austria ambayo inapaswa kuwapa ulinzi. Inapuuza sehemu kuu za kanuni za wachache: uhifadhi wa damu, uhifadhi wa pesa, uhifadhi wa heshima, na utukufu wa imani zinazounda kitambulisho. Kuhifadhi mambo haya ni sharti la lazima kwa uwepo na uhai wa jamii ndogo za kifikra na kidini, na kwa hivyo hujumuisha msingi usio weza kujadiliwa wa kuishi pamoja katika jamii moja. Lakini, sera ya serikali ya Austria ya uoanishaji wa lazima inadhoofisha msingi wa mshikamano kati ya Waislamu na wasiokuwaWaislamu, haswa kwa kutia hatiani majukumu na wajibu wa kidini, na sasa inahamia kushtaki na kutia hatiani imani za kimsingi ambazo zinajumuisha kitambulisho. Kwa hivyo, kuletwa kwa Ibara ya 247B katika Kanuni ya Jinai ilikuwa, kwa uchache kabisa, ukiukaji wa hadhara wanaojivunia kwayo na fedheha kwa Jamhuri ya Austria.
Ili kuepusha mzozo wa kihadhara ndani ya jamii, Hizb ut Tahrir anatoa wito kwenu mkomeshe ajenda hii ya uoanishaji, na murudi kwenye sera ya usawazishaji maslahi ambayo inazingatia mahitaji ya vikundi vyote katika jamii. Ingawa Hizb ut Tahrir inalengwa moja kwa moja kupitia kifurushi kilichopangwa cha "kupambana na ugaidi" na upanuzi wa Sheria ya Kukataza Nembo na Mashirika, sisi, kwa msingi wa ukinaifu wetu ya kimfumo na kidini, tumejitolea bila masharti kwa kanuni ya wachache. Kama Waislamu wanaoishi kihali nchini Austria, tumejitolea kwa utukufu wa damu, pesa, heshima na imani kwa raia wasiokuwa Waislamu na kwa jamii kwa ujumla. Kwa kuwa kanuni ya wachache inaweza tu kuzaa matunda kupitia majibu ya pande mbili, mwishowe inategemea uamuzi wa wanasiasa wa Austria, ima mustakbali wa Jamhuri ya Alpine utasifika kwa ubaguzi, mizozo na kutengana, au uelewa wa kijamii na amani.
Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولاً]
“Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.” [Al- Isra: 34].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Nchi Zinazozungumza Kijerumani |
Address & Website Tel: 0043 699 81 61 86 53 |
Fax: 0043 1 90 74 0 91 E-Mail: shaker.assem@yahoo.com |