Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  17 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 H / 28
M.  Jumatatu, 28 Juni 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuuawa kwa Mbebaji Ulinganizi Mkweli Omar Faruq ni Onyo Dhahiri kwa Ummah kwamba Uislamu na Waislamu Daima Watabaki bila ya Ulinzi chini ya Watawala wa Kisekula

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inatoa rambi rambi zake za dhati kwa Waislamu waliofiwa wa wilaya ya mbali ya milima ya Bandarban ya Bangladesh ambao wamempoteza kiongozi wao mhamasishaji Omar Faruk Tripura, Mwislamu mwenye umri wa miaka 55 aliyeuawa mbele ya nyumba yake kama shahidi (inshaAllah) mikononi mwa maadui wa Uislamu. Tunasema tu yale yanayompendeza Mola wetu: "Sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarudi". Mwenyezi Mungu (swt) amkubali ndugu huyu miongoni mwa Manabii, Siddiqeen, na Shuhada ' (mashahidi) katika Pepo na aifanye hadithi yake kuwa hamasa kubwa kwa sisi sote kutumia maisha yetu na utajiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Ndugu Omar alisilimu kutoka kwa Ukristo mnamo 2014, na pia alisaidia kuzisilimisha familia zingine 30 tangu wakati huo. Alianzisha msikiti wa kwanza kabisa kwa Waislamu huko kwa gharama zake mwenyewe na katika ardhi yake mwenyewe. Alikuwa Muislamu wa kwanza katika kijiji cha mbali cha Rouyachory wilayani Bandarban, na sasa pia amepatana heshima ya kuwa wa kwanza kuuawa shahidi. Kulingana na maelezo ya Waislamu wa kijiji hicho, kikundi cha kishupavu kigaidi kilikuwa kinamtishia ndugu Omar kutokana na da'wah yake isiyokoma ya Uislamu, na hatimaye wakamuua. Waislamu wachache wa eneo hilo sasa wanaishi kwa hofu na wasiwasi kwani polisi wameshindwa kuhakikisha usalama kwao.

Hadithi ya kaka huyu lazima iwe kiamsha-moyo kwa Waislamu wote nchini Bangladesh, haswa wale wanaofurahiya hadhi ya kipekee, kutambua ni zipi zinapaswa kuwa dori za kweli za Waislamu wakati huu ambapo Uislamu na Waislamu wanashambuliwa vikali na washabiki wa kisekula wa mfumo wa dola za kitaifa. Alikuwa Mwislamu aliyesilimu wa ajabu mno wa zama zetu ambaye alichukua jina la 'Omar Faruq' kuiga shakhsiya ya Khalifa wa pili wa Uislamu - 'Umar bin Khattab (ra). Hakika, kaka huyu alimuiga vyema Umar ‘al-Faruq’ mtukufu (yaani yule anayetenganisha kati ya haki na batili). Alisimama waziwazi kwa ajili ya Uislamu na alijaribu kuutetea Uislamu bila hofu yoyote dhidi ya vitisho vya maisha. Kuhusu wanaume kama hawa, Allah Azza Wa Jal asema,

 [مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surah Al Ahzab: 23].

Enyi Waislamu, Hizb ut Tahrir kamwe haitakwepa kuwakumbusha ukweli kwamba Uislamu na Waislamu kamwe hawatakuwa salama chini ya utawala wa demokrasia ya kisekula. Kwa kuwa usekula unagongana moja kwa moja na Uislamu, uongozi wake unachukulia utawala wa Uislamu kama tishio kubwa kwa uwepo wake. Haswa, wakati kuenea kwa Uislamu katika maeneo ya milima ya Bangladesh ni muhimu sana kwa kuzingatia siasa za jiografia ya eneo, serikali ya Hasina kamwe haitawasaidia Waislamu kwa kuchukua msimamo mkali dhidi ya vikundi vya kigaidi vya makafiri huko. Kwa hivyo, katika maeneo hayo ya mbali nchini Bangladesh ambapo Waislamu ni wachache, serikali ya Hasina itawaacha kuwa wahasiriwa wa makafiri. Zaidi ya hayo, katika bara, itazuia usemi wowote wa kisiasa wa Uislamu hata kama utatoka kinywani mwa Mwislamu yeyote. Kutekwa nyara kwa mzungumzaji mchanga wa Kiislamu na wakala mashuhuri wa serikali kwa hotuba zake juu ya kurudi kwa Khilafah na njama ya makafiri dhidi ya Uislamu inatoa ushahidi wa ukweli huu. Kwa hivyo, tunatoa wito wa dhati kwa Waislamu wote nchini Bangladesh kuhamasishwa na kujitolea kwa shahidi Omar Faruq kwa Uislamu, na kuunga mkono kazi ya kusimamisha tena Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Kwa hili, Waislamu na dhimmi (raia wasio Waislamu wa Dola) wataondolewa kutoka kwenye giza la mfumo wa Kimagharibi, na watahudumiwa kikamilifu na Dola na maisha yao kutunzwa.

Enyi Maafisa wenye ikhlasi wa Jeshi la Bangladesh, Omar Faruq mkweli na jasiri alitambua misheni yake, na kwa hivyo aliweka ahadi yake na Mwenyezi Mungu kwa kujitolea maisha yake kueneza Uislamu licha ya kuwa alikuwa raia dhaifu sana. Na huku mkishikilia ufunguo halisi wa nguvu na mamlaka, mnapaswa kuwa makini zaidi juu ya kutimiza ahadi yenu kwa Mwenyezi Mungu (swt). Mnapaswa kuchukua msimamo mkali kulinda Uislamu na Waislamu. Mnapaswa kukimbilia kuwaondoa watawala wa sasa wa kisekula na kukabidhi mamlaka kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah Rashida. Mkipuuza jukumu hili, nguvu zenu za kimada za ulimwengu huu ndizo zitakazokuwa chanzo kikubwa cha fedheha yenu na udhalifu wa milele siku ya hesabu mbele ya Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu