Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  10 Shawwal 1445 Na: 1445 H / 21
M.  Ijumaa, 19 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Iliandaa Maandamano dhidi ya Kuwasili kwa Ndege Mbili moja kwa moja kutoka Tel Aviv hadi Dhaka kwa Siku Mbili Mfululizo kama Sehemu Uhalalishaji Mahusiano wa Serikali ya Hasina na Umbile haramu la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh, leo (19/4/2024) iliandaa maandamano na matembezi katika majengo tofauti ya misikiti ya Dhaka na Chittagong mnamo Ijumaa (19/4/2024) kwa kichwa, “Ndege mbili zilizowasili Dhaka siku mbili mfululizo moja kwa moja kutoka kwa dola haramu ya Israel, hatua muhimu katika uhalalishaji uhusiano na dola hiyo haramu ya Kiyahudi” - kupitia hili, serikali ya Hasina Imenyakua Jani la Mulberry ambalo lilisitiri Uchi wa Usaliti wake wa Uislamu na Waislamu”.

Wazungumzaji katika mkutano huo walifichua kutapatapa kwa serikali ya Hasina kuhalalisha mahusiano na dola hiyo haramu ya Kiyahudi wakisema: Kutapatapa kuiridhisha Marekani na kubakia madarakani, serikali ya Hasina inajiunga na safu za watawala wasaliti wa Kiarabu wa Waislamu ambao walitia saini (na wale wanaosubiri kutia saini) Makubaliano ya Abraham jijini Washington DC mnamo Septemba 15, 2020, yaliyofungishwa na Marekani. Huku ukatili wa umbile lililolaaniwa la Kiyahudi juu ya Waislamu wa Palestina unasumbua dhamiri ya ulimwengu, huku Waislamu ulimwenguni wakipaza sauti katika matakwa yao ya kupelekwa vikosi vya majeshi ya Waislamu kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa, huku ombi la Waislamu kwa Mwenyezi Mungu (swt) katika mwezi huu wa Ramadhan likiwa ni ukombozi wa Palestina; Serikali ya Hasina bila aibu ilikimbilia kuhalalisha mahusiano na dola haramu ya Israel kwa mujibu wa sera ya “suluhisho la dola mbili” la Marekani. Serikali ya Hasina iliweka hatua muhimu ya kuhalalisha mahusiano na dola haramu ya Kiyahudi kupitia kutua kwa siri ndege ya Israel yenye makao Marekani kwenye ardhi ya nchi hiyo bila kujali hisia za watu na kuchagua njia ya usaliti wa Uislamu na Ummah wa Kiislamu.

Wazungumzaji kwenye mkutano huo, walifichua sera ya udanganyifu ya serikali ya Hasina kuelekea Waislamu wa Palestina, wakisema: Hasina ni mtawala mnafiki ambaye amewapotosha watu wa nchi hiyo kwa kuwalilia Waislamu wa Palestina, wakati serikali yake inadumisha mafungamano na umbile la Kiyahudi.

Serikali yake ilipeleka wanajeshi 75 wa Jeshi la Wanamaji la Bangladesh hadi Lebanon chini ya misheni ya kulinda amani kulinda umbile la Kiyahudi kutokana na mashambulizi ya Mujahidina. Hapo awali, serikali yake iliondoa maneno “isipokuwa Israeli” kutoka kwa pasi za Bangladesh katika harakati za kuhalalisha mahusiano na dola haramu ya Kiyahudi. Wakati maisha ya Waislamu wa Palestina 33,000, pamoja na watoto na wanawake 25,000, yamepotea hadi kufikia sasa katika mauaji ya halaiki ya 'Israel', serikali ya Hasina, kwa kuruhusu ndege za 'Israel' kutua kwenye ardhi ya nchi hii, imevujisha damu zaidi ndani ya nyoyo za Waislamu kwa mshale wake wa khiyana.

[قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ] “Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Surah Al-Munafiqun: 4]

Kuwakumbusha Waislamu juu ya jukumu lao la kuikomboa Ardhi takatifu ya Palestina, wazungumzaji walisema: Ummah wa Kiislamu umeshuhudia jinsi baada ya kuvunjwa Khilafah mnamo 1924 M, Mayahudi walivyoikalia kimabavu Ardhi Takatifu ya Palestina kwa msaada wa Wakoloni Makafiri wa Magharibi, kwa kimya cha watawala vibarala wa kisekula waliopandikizwa juu ya Ummah wa Kiislamu, bado wanaendelea kuwafanyia ukatili Waislamu wa Palestina wanaoikwamilia Ardhi hii Takatifu na mara kwa mara kuunajisi Msikiti wa Al-Aqsa, Qibla cha kwanza cha Waislamu.

Kwa hivyo, njia pekee ya kuikomboa Palestina ni kuungana pamoja na Hizb ut Tahrir katika mapambano ya kisiasa ya kusimamisha tena Khilafah na kuhamasisha wale katika watoto wetu wanaohudumu katika jeshi kuipa Nusrah Hizb ut Tahrir katika kusimamisha tena Khilafah, ambayo itakomboa Palestina kupitia operesheni za jeshi, Insha'Allah.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu