Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  27 Ramadan 1445 Na: H 1445 / 19
M.  Jumamosi, 06 Aprili 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Hasina Ilishindwa Kabisa Kulinda Usalama wa Maisha na Mali ya Watu na Ubwana wa Nchi hii kutokana na Kundi la Kujitenga la Kisilaha la Kitaifa la Kuki-Chin (KNF), lakini haisiti kukandamiza Watu ili kusalia Madarakani

(Imetafsiriwa)

Mnamo Aprili 2, 2024, Jumanne saa 8:30 jioni huko Upazila Ruma ya Bandarban na saa 1:00 adhuhuri mnamo Jumatano katika eneo jengine la Upazila, matawi matatu ya Benki ya Sonali na Benki ya Krishi yalishambuliwa kwa mtindo wa sinema mbele ya idadi kubwa ya watu. Huko Ruma walishikilia watu mateka kwa mtutu wa bunduki na huko Thechi walizua hofu kwa kurusha risasi tupu kwenye soko. Walishambulia matawi ya Benki ya Sonali na Benki ya Bangladesh Krishi huko Thani na kuchukua lakh 17.5. Huko Ruma walimchukua mateka meneja wa tawi la Benki ya Sonali, ambaye baadaye aliachiliwa huru baada ya masaa 48 mnamo Alhamisi jioni kwa uingiliaji kati wa Kikosi cha uchukuaji Hatua za Haraka (RAB  -Rapid Action Battalion). Pia walipora silaha 14 na risasi 415 za polisi na wanachama wa Ansar na pia walichukua simu za rununu za watu waliopo kwenye soko. Tukio hili limeibua maswali miongoni mwa watu kwamba serikali ya Hasina haishindwi kupeleleza watu (kwa kutumia mtandao wa spyware ya unaotoka ‘Israel’) na hata wasisite kutumia silaha na risasi kukandamiza wanafunzi wa shule na vyuo vikuu ambavyo tuliona kwenye harakati ya usalama barabarani, basi kwa nini ujasusi ulishindwa kukabiliana na shambulizi hili kubwa la kikundi kidogo cha kujitenga? Je! Kwa nini kulikuwa na ombwe la usalama katika eneo hilo hata baada ya masaa 17 ya shambulizi la kwanza, ambalo liliruhusu kikundi hiki cha silaha kuzindua shambulizi la pili? Kwa hivyo tukio hili ni kufeli kwa serikali au mchezo wa kuigiza? Baada ya tukio la ujambazi, jinsi KNF ilisubutu kushambulia polisi na kituo cha pamoja upekuzi cha jeshi huko Alikadam baada ya shambulizi la Ruma na Thechi! Na jambo la kushangaza zaidi ni kwamba serikali inapambana na kikundi hiki chenye silaha tu na polisi-BGB badala ya kuhakikisha haraka usalama wa maisha ya watu na mali kwa kupeleka vikosi vya kutosha vya jeshi kulingana na ushauri wa wachambuzi wa usalama! Matokeo yake hofu imeongezeka miongoni mwa watu, watu wanakimbia makaazi yao.

Enyi watu, maeneo ya Mlima wa Chittagong pamoja na Bandarban ni muhimu sana kutoka kwa mkakati wa kijeshi na mtazamo wa siasa ya kijiografia.

Lakini serikali ya Hasina imetishia ubwana wa nchi hii kwa kuondoa vikosi vyetu vya jeshi kutoka hapo kwa jina la Mkataba wa Amani wa Chittagong Hill 1997 kwa ajili ya India. Mbali na hilo, kanda hii yenye umuhimu wa kijiografia ni mahali penye kuzivutia dola za kikoloni. Matokeo yake, tunaona mabalozi wa Marekani, pamoja na wanadiplomasia wao wa hali ya juu, kihistoria wakisafiri kwenda eneo hilo na kuendelea na shughuli zao mbali mbali za mashirika yasi ya kiserikali (NGO) zinazozingatia jamii za walio wachache. Kwa mfano, “Balozi wa Marekani jijini Dhaka, Peter D. Haas, alizuru maeneo ya Mlima wa Chittagong, eneo lenye vilima la Bangladesh. Alitumia wakati mwingi huko. Balozi Haas alitembelea miradi mbali mbali katika eneo hilo inayofadhiliwa na kusimamiwa na mashirika ya maendeleo ya kimataifa ya nchi yake - USAID, Ubalozi wa Marekani na Mipango ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa - UNDP” [Human Land, March 12, 2023].

Baada ya tukio la ujambazi, KNF ilifanya machapisho kadhaa kwenye Facebook yao ambayo kupitia kwayo nia yao iko wazi, “majaribio ya kutatua matatizo za jamii za zilizo nyuma kimaendeleo kupitia uvamizi na vita vya silaha ni hatua ya kitoto na isiyoweza kuelekezwa na safu ya juu ya serikali.

Wanadai kwamba Maeneo ya Mlima wa Chittagong yaliundwa mnamo 1860 kwa sababu ya Uasi wa Kuki. Maelfu ya wanajeshi wa Uingereza walipata hasara kubwa katika vita hivyo. Tena mnamo 2021-22, watu wa Kuki-Chin walianza uasi kulinda ardhi ya babu zao na vita vikali vilifanyika na vikosi vya serikali” [Samakal, 05 Aprili 2024]. Kwa hivyo ni kwa maslahi ya nani serikali inawabandika kibandiko tu cha  makundi ya kigaidi badala ya kama makundi ya kujitenga? Je! Ni kwa maslahi ya nani serikali iliingia katika mazungumzo ya amani nao badala ya kuwamaliza? Kwa kweli, watawala vibaraka wa nchi yetu hawatasita kuharibu ubwana wa nchi hii na kuitupa idadi nzima ya watu katika janga ili kutumikia maslahi ya wakoloni.

Enyi Watu, Mwenyezi Mungu (swt) anatuonya kuhusu kudhamini maisha na mali yetu kwa watawala hawa Ruwaibidha. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّهُ لَكُمْ قِيَامًا]

“Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu.” [Surah An-Nisaa: 05]. Kando na hayo, ubwana wa Umma wa Kiislamu kamwe hauko salama mikononi mwa watawala hawa vibaraka. Kuhusu usalama na ubwana, Mtume (saw) amesema,

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam (Khalifa) ni ngao watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye.” Kwa kweli, baada ya kuvunjwa Khilafah, mkoloni wa Magharibi Uingereza-Marekani alipandikiza juu yetu vikundi vya watawala, ambao wanatumikia maslahi ya kisiasa ya wakoloni kwa kuuza ubwana wa nchi za Waislamu, wanasalia madarakani kupitia kuwakandamiza watu bila kujali usalama wa maisha ya watu na mali. Kwa hivyo lazima muungane na uongozi wa dhati wa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha tena Khilafah na mutoe wito kwa watoto wetu jasiri katika jeshi ili kuipa Nusrah Hizb ut Tahrir katika kusimamisha tena Khilafah.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu