Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  15 Sha'aban 1445 Na: 1445 H / 16
M.  Jumapili, 25 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
25 Februari "Maasi ya BDR"

Kumbukumbu ya Usaliti wa Serikali ya Hasina dhidi ya Jeshi letu na Ubwana wetu

(Imetafsiriwa)

Leo inatimia miaka 15 ya njama mbaya ya serikali ya Hasina ya kulidhoofisha jeshi la nchi hii iliyotokea katika makao makuu ya BDR (Bangladesh Rifles) katika Pilkhana ya mji mkuu Dhaka. Katika tukio hilo, jumla ya watu 74 wakiwemo maafisa 57 shupavu na mahiri wa jeshi akiwemo mkuu wa BDR Meja Jenerali Sakil Ahmed waliuawa kwa jina la uasi wa askari wa BDR. India ilitekeleza njama hii kwa msaada wa serikali ya Hasina kudhoofisha jeshi la nchi hii. Hivi majuzi mwandishi wa habari wa Kihindi (Avinash Paliwal, Profesa Mshiriki wa Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha SOAS jijini London, aliyebobea katika uchambuzi wa sera za kigeni na usalama kwa kuzingatia eneo la Asia Kusini) aliandika katika chombo kikuu cha habari nchini humo 'Hindustan Times' kufafanua ushiriki wa India.

Taarifa yake ilifichua kwamba India ilitishia kuingilia kijeshi moja kwa moja nchini Bangladesh wakati wa uasi wa BDR ili kuzuia operesheni ya jeshi la Bangladesh huko Pilkhana. Mbali na hayo, ili kuleta hali ya hofu miongoni mwa wanajeshi wote, serikali ya Hasina iliwafuta kazi maafisa wa kijeshi watiifu kwa visingizio mbalimbali, ikawalazimisha kuacha kazi zao kupitia vitisho, na maafisa wengi walipotezwa kwa nguvu au kuuawa. Ombwe lililotokana na hili jeshini tangu wakati huo liliendelea na mradi wa kupanga upya jeshi kama kikosi cha chini cha India kwa kulifanyia mageuzi kikamilifu jeshi. Mchoro wa udhibiti wa India juu ya jeshi la nchi hii kupitia mafunzo kwa maafisa wa jeshi na serikali ya adui, makubaliano ya kijeshi na India, kuongezeka kwa uchokozi wa vikosi vya India kwenye mpaka sasa ni wazi kama mwangaza wa mchana. Kwa upande mwingine, kutokana na uhusiano mpya kati ya Marekani na India, muungano kibaraka wa Marekani wa BNP pia ulicheza dori ya kipofu katika njama hii na kufanya mageuzi makubwa ndani ya chama chao vilevile. Kwa sababu, Marekani inaimakinisha India kama mlinzi katika eneo hili ili kukabiliana na China na kukabiliana na kuibuka kwa Khilafah - matarajio ya kisiasa ya Umma wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[إِنَّهُمْ إِنْ يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَنْ تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا]

“Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao; na hapo hamtafanikiwa kabisa!” [Sura Al-Kahf: 20].

Enyi Watu, tabaka tawala la sasa la kisekula, lililorithiwa kutoka enzi ya Waingereza, ni vibaraka wa makafiri-wakoloni na kwa hakika wao ni maadui wa nchi na Waislamu. Hivyo mnapaswa kukataa kabisa haya makundi ya vibaraka wa kisekula, kwa sababu hayalindi maslahi ya nchi na wala hayawawakilishi Waislamu. Ikiwa tunataka kukombolewa kutoka kwenye makucha ya Kafiri-Washirikina, lazima tuungane na wanasiasa wanyoofu wa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha tena Khilafah. Mtume (saw) amesema,

«وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao watu hupigana nyuma yake na kujihami kwaye” (Sahih Muslim).

Enyi Maafisa Wanyoofu katika Jeshi, mnajua jinsi serikali ya Hasina inavyokufundisheni kuwa waoga badala ya kuwa wanaume kukabiliana na India. Moja ya ishara yake ni kwamba mmoja wa wenzenu anachukuliwa na kuuawa na BSF ya India, na kukulazimisha kutokuwa wachangamfu katika kujibu. Hivyo munapaswa kusonga mbele katika kusimamisha tena Khilafah chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir kwa kuuondoa utawala huu kibaraka, na kuipa Nusrah (nguvu) Hizb ut Tahrir kwa ajili hiyo. Kwa sababu ni Khilafah pekee ndiyo itakayokufanyeni kuwa jeshi lenye nguvu dhidi ya adui. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِنْ دُونِهِمْ لاَ تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنفِقُوا مِنْ شَيْءٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنْتُمْ لاَ تُظْلَمُونَ]

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.” [Surah al-Anfal: 60].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu