Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  26 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 16
M.  Jumapili, 29 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bangladesh Haipaswi Kuyaangalia Mataifa ya Kibeberu ya Magharibi kwa Mafanikio na Ufanisi wake na Isiwe Mwathiriwa wa Siasa za Jografia za India na Marekani

(Imetafsiriwa)

Mshauri mkuu wa serikali ya mpito ya Bangladesh Dkt. Muhammad Yunus alitoa wito kwa viongozi wa kimataifa kuunga mkono ujenzi wa Bangladesh mpya wakati akizungumza kwenye mapokezi kando ya Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa jijini New York mnamo Jumanne. Mara tu baada ya hotuba hiyo, rais wa Marekani Joe Biden pia alisema ikiwa wanafunzi wa Bangladesh wanaweza kujitolea sana kwa ajili ya nchi yao, Marekani pia inapaswa kufanya zaidi. Hapo awali, Dkt. Yunus alitafuta usaidizi huo wa Fedha wa Kimataifa wakati ujumbe wa Marekani wenye uwezo mkubwa ukiongozwa na Waziri Msaidizi katika Idara ya Hazina ya Marekani Brent Neiman walipokutana naye jijini Dhaka. Ujumbe wa Marekani pia umeeleza dhamira ya dhati ya kufanya kazi na serikali ya mpito, na tayari nchi hizo mbili zimetia saini makubaliano ambapo Marekani itatoa msaada wa dolari milioni 202 kwa Bangladesh kama msaada wa maendeleo.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inaitaka serikali ya mpito kuzingatia ushauri ufuatao:

Kwanza: Kwa nini kile kinachoitwa msaada kutoka kwa nchi za kibeberu za Magharibi kinahitaji kutafutwa mara kwa mara katika kuijenga upya Bangladesh! Hapo awali, dhalimu Hasina pia angetafuta msaada kama huo kutoka kwa Marekani na mataifa mengine ya Magharibi. Kama ambavyo Marekani inaiunga mkono serikali ya mpito hivi sasa, ilitumika pia kutoa uungaji mkono sawia kwa dhalimu Hasina (“Biden amwandikia Waziri Mkuu Hasina, akionyesha kujitolea kusaidia malengo ya kiuchumi ya Bangladesh”, Dhaka Tribune, 04 Feb 2024). Mataifa haya ya Magharibi ya Machiavellian ndiyo yaliyomwacha Hasina kuwa dhalimu wa kutisha kwa maslahi yao ya kijografia. Kwa hivyo, kupinduliwa kwa Hasina na watu wengi kwa kweli ilikuwa changamoto kwa mfumo na utawala wa kilimwengu wa Magharibi. Kujitolea kwa watu, utashi na matarajio yao havikuwa kukabidhi nchi kutoka kwa mshiko wa India hadi kwa mabeberu wa Magharibi. Kwa hiyo, tunaishauri serikali ya mpito itoke kwenye dhana hii kwamba mamlaka inayotawala na uhalali unapaswa kutoka kwa mabeberu. Mamlaka yako yanatokana na watu wa kawaida na matendo yako lazima yaakisi mapenzi na matarajio yao. Kwa hivyo, ni lazima uendelee kwa tahadhari na mkoloni Marekani ili uache kuwa kikaragosi wa mchezo wa siasa za kijografia wa India na Marekani. Tunakukumbusha kwamba Marekani tayari imeimarisha uhusiano wake wa kiulinzi na usalama na India kwa kiasi kikubwa kama sehemu ya Mkakati wake wa Indo-Pacifiki (IPS). Ushirikiano kama huo wa kimkakati kati ya Marekani na adui yetu jirani una madhara makubwa kwa Bangladesh.

Pili: kile ambacho nchi inahitaji zaidi katika wakati huu muhimu ni umoja wa kitaifa wenye nguvu zaidi kuliko msaada wa kigeni. Kando na njama za India, wawezeshaji wa serikali ya Hasina, ambao wamepandikizwa kwa nguvu katika vyombo vyote vya dola katika miaka 15 iliyopita, pia wanangojea wakati mwafaka wa kujibu. Hivyo, kipaumbele kikuu cha serikali ya mpito kinapaswa kuwa kuleta pamoja vikosi vyote vinavyopinga ubeberu, vinavyounga mkono nchi na vinavyounga mkono Uislamu ili kukabiliana na maadui zetu na vibaraka wao wa ndani. Na chukua ushauri kwamba mchakato huu wa uunganishaji unapaswa kuanza kwa kuondoa mara moja marufuku iliyo kinyume cha sheria ya Hizb ut Tahrir, ambayo ni moja ya vikosi muhimu vya kupinga ubeberu, yenye kuunga mkono nchi na yenye kuunga mkono Uislamu nchini Bangladesh. Kwa hivyo, dhana ya umoja katika makutano haya muhimu haiwezi kufikirika kwa kuiweka Hizb ut Tahrir nje ya mchakato huo. Ubwana wa nchi hii hauwezi kulindwa kupitia kuuweka imara ubaguzi na udhalimu wa Hasina.

Tunatoa wito kwa serikali ya mpito isikilize nasaha zetu za ikhlasi kwani Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal ni shahidi kwamba hatukutakii nyinyi na watu wetu ila kheri. Kwa hivyo, endelea kwa tahadhari na mabeberu wa Magharibi. Hatua zozote dhaifu kutoka kwako zitatufanya tuwe hatarini kwa madhara katika michezo ya maadui zetu.

[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنْ الْمُنكَرِ]

“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu” [At-Tawba: 71].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu