Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
H. 20 Sha'aban 1442 | Na: 1442 / 07 |
M. Ijumaa, 02 Aprili 2021 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Bajeti ya Iraq na Mifuko ya Wafisadi
(Imetafsiriwa)
Baada ya miezi mitatu ya mvutano na ugomvi kati ya wabunge kwa matusi na kupiga mikono, bunge la Iraq liliidhinisha bajeti ya 2021, ambayo ni sawa na dinari za Iraq trilioni 130 (dolari bilioni 89.65), Iraq inategemea katika bajeti yake mafuta ambayo inayasafirisha nje.
Tangu uvamizi wake wa Iraq mnamo 2003, Amerika imeikabidhi kwa kipote fisadi ambacho Amerika ilikinyanyua kwa mikono yake na kukiunda chini ya usimamizi wake, tangu wakati huo Iraq imekuwa mbaya zaidi. Wa mbali bali na karibu wanajua kuwa nchi hii ni moja ya nchi tajiri ambazo Mwenyezi Mungu amebariki kwa rasilimali na kheri. Nambari hizi tunazozisikia katika kuidhinisha bajeti kwa kipindi cha miaka kumi na saba ni pesa nyingi, ambazo zinatokana tu na hisa ya mafuta, kutoka kwa kiwango ambacho serikali ya Iraq huvuna kutoka kwa rasilimali zingine, kama vile sulphur, phosphates, gesi, na nyenginezo, ambazo watu wa Iraq hawajui chochote, na vile vile vivuko vya mpakani, kodi, umeme, maji, mafuta, hiba ya Idara ya Hiba, na nyenginezo ambazo ni nyingi sana kutaja hapa.
Tunasema: Je! Pesa hizi zote zinaenda wapi, na hakuna athari yake yoyote inayoonekana?! Watu wengi wanaishi katika umaskini na ufukara, na miundombinu ni mibovu. Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Iraq ni asilimia 27, huku kiwango cha umaskini ni asilimia 25, kulingana na takwimu za hivi karibuni za Wizara ya Mipango.
Jibu la hilo liko wazi na kila mtu analijua. Huingia mifukoni mwa wafisadi ambao hawaridhiki tena na chochote na hawazuiliwi na heshima au Dini. Ndio maana tuliwaona Bungeni wakimenyana, kugombana na kutukanana kana kwamba ni mbwa walioangukia mzoga, kwa hivyo lengo la kila mmoja wao ni kile anacho pata na hisa yake ya windo. Hili ndilo linalosababisha kutoidhinisha bajeti, kama vile ilivyotokea mnamo 2020, au kuichelewesha kwa miezi, kama vile ilivyotokea mwaka huu. Yeyote anayezitazama aya za bajeti na jinsi zinavyogawanywa huliona hili waziwazi mbele yake.
Enyi Waislamu nchini Iraq: Yote haya yanafanyika na pesa hizo zote ambazo mnazijua na ambazo hamzijui zinapotea, hampati chochote isipokuwa makombo kutoka kwake. Licha ya hayo, kila mwaka wanakupeni habari njema ya kuidhinisha bajeti, ambayo ni yenu kwa sababu msingi ambao kwao bajeti hiyo imeidhinishwa ni yale mafuta ya Iraq yanayouzwa nje; ambayo ni mali ya umma, na ilhali wanayagawa kana kwamba hamna usemi ndani yake. Mpaka lini mtakaa kimya na kwa nini mnanyenyekea wakati mnaonja adhabu mbaya zaidi?!
Enyi Waislamu nchini Iraq: Mwenyezi Mungu (swt) anawaamrisheni kuamrisha mema na kukataza maovu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” [Aal-i-Imran: 110].
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ الرَّسُولَ النَّبِيَّ الأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوباً عِنْدَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالإِنْجِيلِ يَأْمُرُهُمْ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنْكَرِ]
“Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu” [Al-A’raf: 157].
Je! Kuna uovu mkubwa zaidi kuliko huu? Wakati mnaona makatazo ya Mwenyezi Mungu yakikiukwa na haki zenu kuibiwa na pesa zenu kuporwa? Na Mtume mtukufu (saw) amesema:
«إِذَا رَأَيْتَ أُمَّتِي تَهَابُ فَلَا تَقُولُ لِلظَّالِمِ يَا ظَالِمُ فَقَدْ تُوُدِّعَ مِنْهُمْ»
“Pindi utakapoona Ummah wangu ukiogopa wala haumwiti dhalimu: “Ewe dhalimu.” Basi waage” (Imesimuliwa na Al-Hakim katika Al-Mustadrak).
Enyi Waislamu nchini Iraq: Jueni kuwa hakuna suluhisho kwenu na hakuna tiba kwa hali yenu isipokuwa kwa kuikomboa Iraq kutokana na mvamizi na wafuasi wake, na kwa kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu katika dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Dola inayoshughulikia mambo yenu kwa mujibu wa sheria ya Mola wenu, na mnapata haki zenu ndani yake.
]وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Iraq |
Address & Website Tel: |
E-Mail: hutiraq@yahoo.com |