Jumamosi, 25 Rajab 1446 | 2025/01/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  28 Shawwal 1443 Na: 1443 / 05
M.  Jumamosi, 28 Mei 2022

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Kuwazuia Mayahudi Kunahitaji Vitendo Sio Maneno
(Imetafsiriwa)

Wanachama wa Baraza la Wawakilishi la Iraq walipiga kura kuunga mkono sheria iliyopendekezwa ya "kuharamisha usawazishaji mahusiano" na umbile la Kiyahudi, sheria iliyopendekezwa na kambi ya Sadr na washirika wake.

Kifungu chake cha kwanza kinasema: "Marufuku ya kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia, kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kitamaduni au aina nyingine yoyote na umbile nyakuzi la Kizayuni."

Sheria hiyo pia inataja adhabu, ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha au kifungo cha muda, na adhabu ya kifo kwa mujibu wa Kifungu cha 201 cha Kanuni ya Adhabu ya Iraq kwa mtu yeyote anayepigia debe "kanuni za Uzayuni, ikiwemo Freemasonry, au anahusishwa na taasisi yake yoyote, au anawasaidia kifedha au kimaadili, au anafanya kazi kwa njia yoyote iwezekanayo ili kutimiza malengo yake.”

Sheria hii imewasha cheche za athari na shutma kutoka kwa nchi kadhaa; Washington imeelezea wasiwasi wake juu ya kupitishwa kwa sheria hii, ikisema kuwa sheria hii inahatarisha uhuru wa kujieleza na inasaidia kujenga mazingira ya chuki dhidi ya Mayahudi, kinyume kabisa na maendeleo yaliyofikiwa na majirani wa Iraq katika ujenzi wa madaraja na kusawazisha mahusiano na umbile Kiyahudi.

Uingereza ilikosoa sheria hiyo kwa sauti kali zaidi, kama msemaji wa Masuala ya Kigeni katika Baraza la Wawakilishi la Uingereza, David Lammy, alivyosema katika taarifa yake, "Inashangaza kwamba Bunge la Iraq limepitisha sheria kuharamisha, na hata kutishia kifo, kwa wale walio na mahusiano na Israel. Serikali ya Uingereza kwa haraka lazima itumie uzito wake wa kidiplomasia kuizuia Iraq kutokana na sheria hii hatari."

Wizara ya Mambo ya Nje ya umbile la Kiyahudi ilitoa tamko la kulaani sheria hiyo, na msemaji wake akasema: "Hii ni sheria inayoiweka Iraq na watu wa Iraq katika upande mbaya wa historia na kutengwa kutokana na uhalisia."

Mchunguzi wa sheria hii anaona waziwazi kwamba inawapa Mayahudi haki nchini Palestina. Wale wanaokataa kusawazisha mahusiano na nchi hiyo wanasema kuwa imekuwa ikikalia kwa mabavu ardhi za Waarabu nchini Palestina, Syria na Lebanon tangu 1967 na inakataa kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina na Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wake, ikimaanisha kuwa wako pamoja na dola ya Palestina kwa msingi wa 'Mipaka ya 1967 na mji wake mkuu ukiwa ni Jerusalem ya Mashariki, na kwa hivyo wale matapeli wenye kusawazisha mahusiano na umbile la Kiyahudi walikubali kile ilichosalia cha ardhi ya Palestina na kile ilichoinyakua mwaka wa 1948. Hawataki kuikomboa Palestina kutokana na wanyakuzi wake, lakini badala yake wanataka suluhisho litolewe na Amerika kupita kuanzisha muundo wa kijidola kidogo ambacho hakina mamlaka juu ya ardhi, anga wala bahari.

Ushabiki huu wote ni utafutiaji soko wa vyombo vya habari ili kucheza na hisia za Waislamu, na shinikizo kwa umbile la Kiyahudi kukubali suluhisho la Kiamerika. Lau wapinzani hawa wa usawazishaji mahusiano wangekuwa na nia ya dhati kuhusu msimamo wao juu ya umbile la Kiyahudi, wangekuwa wamekata uhusiano na nchi zilizosawazisha mahusiano nalo, na ujumbe wa ngazi ya juu wa Iraq haungekwenda Imarati kutoa rambirambi kwa kifo cha rais wake, Khalifa bin Zayed Al Nahyan, na hakungekuwa na uhusiano na Misri, Jordan, Bahrain, Morocco na Sudan, walio na uhusiano wa umma nao.

Uamuzi wenu huu ni nyongeza ya mafuta kwenye moto, dhihirisho la kiwango cha ubaraka wenu, na kauli ya udhaifu wenu, na ni sheria unayo nyumbuka, kwa hivyo ni upi msimamo wenu kwa wale walio na uraia zaidi ya mmoja? Na wako wengi katika serikali na bunge lenu, kwa hiyo je atawajibishwa kama Muiraqi? Au atakwepa adhabu kwa kuwa Mmarekani, Muingereza au Muirani?

Enyi Waislamu wa Iraq: Sisi katika Hizb ut Tahrir, ambayo imejitolea kwa ajili ya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu na kuzikomboa nchi za Kiislamu hususan Masra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na kuziunganisha nchi za Kiislamu katika dola moja ambayo ni dola ya Khilafah, ingawa tunalaani usawazishaji mahusiano na umbile la Kiyahudi na kuuchukulia kuwa ni khiyana kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Waislamu, lakini tunakataa kuudanganya Ummah na kuufanyia hila hisia zake, suala hili sio suala la maneno na miito mitupu, bali ni suala la mitazamo na matendo. Ikiwa Ruwaibidah hawa (watawala duni watepetevu) wangekuwa na ikhlasi, wangejua kwamba nusra kwa watu wetu wa Palestina na ukombozi wake kutokana na umbile nyakuzi inaweza kupatikana tu kupitia kuyahamasisha majeshi na kutangaza jihad, kwa kuitikia kauli ya Mwenyezi Mungu:

 [وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Al-Baqara: 191]. Kwa njia hii, ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mayahudi itatimia kwamba wakati wowote watakaporejea kwenye utukufu, ufisadi na dhulma, Mwenyezi Mungu atawapa uwezo wa kuwaadhibu na kuwafedhehesha. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema,

 [عَسَى رَبُّكُمْ أَنْ يَرْحَمَكُمْ وَإِنْ عُدْتُمْ عُدْنَا وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيراً]

“Huenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni. Na mkirudia na Sisi tutarudia. Na tumeifanya Jahannamu kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri.” [Al-Israa: 8].

Hivyo basi ili kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir, tunawalinganieni enyi Waislamu, kusimamisha mamlaka yenu, na muondoe udhalilifu kutoka shingoni mwenu, ili mupewe izza kwa dini yenu, mkiogopewa na adui yenu, wala msiogope lawama za wenye kulaumiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu