Jumanne, 14 Rajab 1446 | 2025/01/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  20 Sha'aban 1442 Na: 1442/17
M.  Ijumaa, 02 Aprili 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Da’wah kutoka katika Kizazi cha Kwanza
Sheikh Yaseen Yousuf Zalloum (Abu Ammar)

(مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23].
(Imetafsiriwa)

Kwa kujisalimisha kwa amri ya Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Ta'ala na kuridhika na Qadhaa Yake, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan inaomboleza kwa Umma wa Kiislamu kwa jumla, na kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al- Rashtah, na kwa Shabab wa Hizb ut Tahrir haswa, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, mbebaji mahiri wa Da'wah na mwanasiasa mkuu, Sheikh Yaseen Yousuf Zalloum (Abu Ammar), mmoja wa wanachama wa kizazi cha kwanza cha Hizb ut Tahrir, na kaka wa Amiri wa pili wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Abdul-Qadeem Zalloum (Rahimahullah), aliyefariki leo Ijumaa tarehe 20 Sha'aban 1442 Hijria sawia na 2/4/2021 katika mji wa Amman nchini Jordan, baada ya umri wa maisha ambao aliutumia katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kurudisha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya pili la Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Abu Ammar (Rahimahullah) alikuwa shina tukufu la mti uliobarikiwa; alikuwa mwanachama mchangamfu wa Hizb ut Tahrir tangu ilipoanza, kwani yeye ni mtoto wa Hafidh wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Sheikh Yousuf Zalloum, na kaka wa Amiri wa pili wa Hizb ut Tahrir Sheikh Abdul-Qadeem Zalloum, na yeye, Rahimahullah, alikuwa akifanya kazi kwa umakini na bidii ili kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah Rashida. Amefariki kabla ya Mwenyezi Mungu (swt) kumruhusu ashuhudie alfajiri ya Khilafah, kumpa ahadi ya utiifu (bay'ah) Khalifa wa Waislamu na kupata wema na thawabu kutoka kwa Allah (swt), lakini kinachotufariji ni kwamba amekufa huku akiwa amejitolea kwa Uislamu, aliyejitolea kubeba ulinganizi wake hadi siku ya kifo chake.

Yeye – Rahimahullah – alikuwa mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuregesha Aqeeda na mfumo wa maisha wa Kiislamu, na alikuwa mkweli kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) katika kufuata nyayo zake katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, hivyo basi kwa kweli – na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Mjuzi Zaidi – alikuwa miongoni mwa wale:

 (صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً)

“walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23].

Tunamwomba Mwenyezi Mungu (swt) akurehemu, Abu Ammar, na akufufue pamoja na Manabii, wakweli, Mashahidi na wema, na hawa ndio watu bora kuwa pamoja nao. Tunamwomba Mwenyezi Mungu amlipe malipo bora zaidi kwa niaba yetu na kwa niaba ya Waislamu, na kutumiminia subira na kuongeza thawabu zetu, wa la hawla wa la quwata illa billah. Mwenyezi Mungu akurehemu Abu Ammar, tumesikitishwa na kuondoka kwako, lakini hatusemi isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu (swt) ametuamuru:

(الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُمْ مُصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ)

“Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah:156]. Hivyo Inna Lillah Wa Inna Ilayhi Raji’oon - Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu