Jumanne, 14 Rajab 1446 | 2025/01/14
Saa hii ni: 03:21:09 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  23 Sha'aban 1442 Na: 1442 / 18
M.  Jumatatu, 05 Aprili 2021

 Tanzia ya Mbebaji Da’wah
Haj Abdelrahman Husain (Abu Maher)

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23].
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Jordan anamuomboleza mtu katika ya watu wake bora, mbebaji Dawah, Haj Abdelrahman Husain (Abu Maher), ambaye alikwenda katika rehma za Mwenyezi Mungu Azza wa Jal mnamo Alhamisi akiwa na umri wa miaka 87 baada ya maisha ambayo aliyatumia katika kumtii Mwenyezi Mungu (swt) na kufanya kazi na Hizb ut Tahrir kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Haj Abdelrahman Husain (Abu Maher), Mwenyezi Mungu airehemu roho yake, aliubeba ulinganizi wa kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu katika safu za Hizb ut Tahrir tangu miaka hamsini ya karne iliyopita, hadi alipofutwa kazi jeshini kwa sababu hiyo na kufungwa gerezani, na kukabiliwa na mateso makali, na alibaki thabiti na kuvumilia, akiamrisha wema, akipuuzia uovu hata katika uzee wake na udhaifu wa mwili wake akiwapenda Mashababu, akitangaza ushindi, akimwomba Mwenyezi Mungu amshuhudishe Khilafah, mpaka amri ya Mwenyezi Mungu ilipokuja na yeye yuko juu ya hilo, na roho yake ikenda kwa Muumba wake.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu amfinike kwa rehma Yake pana na ampokee katika bustani Zake kubwa na tunamuomba Mwenyezi Mungu amlipe kwa niaba yetu na kwa niaba ya Waislamu kwa malipo bora zaidi. Wa Inna Lillah Wa Ina Ilaihi Rajiun.

Hakika, Mwenyezi Mungu huchukua kilicho chake, na anachotoa ni chake, na tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi, Subhanahu wa Taalla, Wa Inna Lillah Wa Ina Ilaihi Rajiun.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu