Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  9 Rabi' I 1443 Na: 1443/02
M.  Jumamosi, 16 Oktoba 2021

Uingizaji Usekula na Kutengwa kwa Mitaala ya Elimu ni Sehemu ya Sera Fisidifu ya Serikali katika Nchi za Kiislamu ...

Uoanishaji wa Aina za Jinsia kama Muundo

 (Imetafsiriwa)

Kwa kuzingatia shambulizi la kimpangilio la kuyagonga maadili ya Uislamu katika nchi za Kiislamu, Wizara ya Elimu nchini Jordan ilisambaza vitabu kwa idara za elimu 42 katika magatuzi anuwai kutekeleza mpango wa mafunzo kwa walimu wa kiume na wa kike juu ya "uoanishaji jinsia katika elimu na mazingira ya shule.” Kwa ufafanuzi wa hili, msemaji wa Wizara ya Elimu, Ahmed Al-Masa'fa, alithibitisha: "Hakuna masharti kutoka kwa serikali ya Canada inayofadhili mradi huu katika kufanya kozi hizi, kuonyesha kwamba wizara imejitolea kwa falsafa ya elimu, sheria ya Kiislamu, na mila na desturi za jamii ya Jordan.” Kuonyesha ubatili na ujanja wa madai haya, tunasema:

Unapozungumza juu ya maneno ya Kimagharibi, ni muhimu kuregelea wamiliki wa maneno hayo ili kuelewa maana halisi waliyoikusudia. Pindi unapochukua neno hili, na unapozungumzia kuhusu jinsia, Shirika la Afya Dunia limelifafanua kama: "Neno ambalo matumizi yake ni muhimu kuelezea sifa ambazo wanaume na wanawake wanazo kama sifa ngumu (za kijamii), yaani, zisizohusiana na tofauti za kimaumbile. na muundo wa kibaolojia.” Katika Encyclopedia Britannica, neno jinsia limefafanuliwa kama: "hisia za mtu mwenyewe kama mwanamume au mwanamke bila ya kujali jinsia yake ya kibaolojia." Utamaduni wa kijinsia ni moja ya vifungu vya Makubaliano ya CEDAW Kifungu cha 5, Aya A - ambayo Jordan iliyatia saini mnamo 1992 na kupasishwa na kuchapishwa katika Gazeti Rasmi mnamo 2007.

Kutokana na hayo yaliyotangulia, yafuatayo yanajitokeza:

Kwanza, ni wazi kuwa sababu ya kubuniwa kwa neno jinsia ni ukwepaji wa watetezi wa "usawa kamilifu kati ya mwanamume na mwanamke" juu ya jinsia, ambayo hauwezi kuvukwa kwa sababu ya uwazi wa tofauti katika viungo na mwili.

Pili: Utamaduni wa kijinsia huanzisha ushoga, na huchukulia uhusiano wa kingono kati ya wanaume wawili au wanawake wawili kama uhusiano halali baina ya aina tofauti, ambapo mmoja wao anahisi kama mwanamume na mwingine kama wa mwanamke.

Tatu: Utamaduni wa kijinsia hufuta umama na huuchukulia kama kazi tu ambayo inaweza kufanywa na mwanamume au na wengine kando na mama. Mwanaharakati wa wanawake wa Kiingereza Anne Oakley - ambaye ndiye wa kwanza kuanzisha neno hili kwa masomo ya kijamii - anaamini kuwa umama ni hadithi iliyoundwa na jamii na haina mizizi katika silika ya mwanadamu. Badala yake, ni kazi ya jamii ambayo inaweza kufanywa kupitia badali nyingine yoyote, na hili lilithibitishwa na Makubaliano mabaya ya CEDAW katika kifungu cha 5, Aya B.

Ikiwa huu ndio uhalisia wa utamaduni wa kijinsia, na ikiwa hiki ndicho kiini cha mawazo yanayoulingania, basi ni kujitolea kupi kwa sheria ya Kiislamu inakodai Wizara ya Elimu inapojaribu kuchanganya mawazo haya na hukmu za sheria za Kiislamu?! Je! Ni uhalili upi unaoisukuma Wizara ya Elimu katika ufisadi huu kwa kuoanisha thaqafa hii ndani ya mitaala ya elimu?!

Hivyo basi, Enyi Watu wa Jordan:

Utetezi wa haki za wanawake chini ya kaulimbiu ya usawa na utamaduni wa jinsia ni sehemu tu ya kampeni za kimpangilio za kithaqafa na kisiasa za kimfumo zinazoongozwa na Magharibi katika nchi za Waislamu tangu kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah katika jaribio la kuupotosha Umma wa Kiislamu kutoka kwa dini yake na ufahamu wake wa kadhia zake, kwa lengo la kupenya ndani ya maisha ya kijamii ya Waislamu, na kuharibu familia ya Kiislamu, kwa kuwafisidi wanawake wake na hivyo kuharibu kizazi chote cha Waislamu, na Umma wa Kiislamu na wanawake wake wanajua kikamilifu malengo ya kampeni hizi ambazo zinaungwa mkono na juhudi za kisiasa katika ngazi zote za ulimwengu, kwa hivyo inafadhili na inasaidia kozi kama hizo kuwaleta wanawake wa Kiislamu katika kimbunga cha mitego hii, na yote haya yako chini ya masikizi na ushajiishaji wa serikali nchini Jordan, ambayo inazuia, inatesa na inawafunga gerezani wabebaji dawah, ilhali wanalingania Uislamu kupitia chama cha siasa ambacho hufanya kazi ya kifikra ya kisiasa, huku ikimruhusu mgeni kuingilia kati mambo ya Ummah na uvamizi kwa uvamizi wa thaqafa potofu ya Kimagharibi na mawazo yake ya uadui kwa Uislamu na Waislamu.

Mfumo wa Kiislamu hubeba muundo wa kipekee wa aina yake kama nidhamu ya wanadamu inayoshughulikia matatizo ya wanadamu. Uislamu umewaheshimu wanawake, umehifadhi haki zao, na umetungia sheria kwao ambazo zinahakikisha haki zao na utu, awe ni mtoto mdogo au mwanamke mzee, na awe ni mama, binti, dada, khale au shangazi. Au mke au mwanamke wa kando, kwa hivyo Uislamu unaamuru kuwaheshimu wazazi na kumpa mama nafasi iliyo kubwa kuliko baba, na ndiye anayestahiki zaidi kwa watu kwa wema na ushirika mzuri, na yeyote atakayewalea binti zake vizuri, watakuwa ni ngao yake kutokana na Moto, na umeamuru kuweka mafungamano ya kizazi, ulinzi wa heshima na kushusha macho chini, na umeamuru wanaume wajitahidi katika kujilinda wao, na sheria na amri zengine ambazo zilikuja kwa ufafanuzi wa kina katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake (saw), na ambazo zilitabikishwa kwa zaidi ya karne kumi na tatu, wakati ule ambapo Ulaya ilikuwa ikiishi katika Zama za Katikati ndani ya giza kamili.

Enyi Watu wa Jordan:

Kataeni kozi hizi zote, makubaliano, na tamaduni, na wafundisheni watoto wenu mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw), wafundisheni Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah ya Mtume wake (saw), waambieni kuhusu Maswahaba watukufu (ra) na jinsi walivyobeba Uislamu na kujitoa muhanga kwao ili kusimamisha dini ya Mwenyezi Mungu duniani, waambieni kuhusu mama wa waumini (ra) na maswahaba wakubwa (ra) ambao waliacha athari kubwa katika njia ya kuubeba Uislamu ambao vizazi bado vinaipitisha kwa wengine. Kuzeni ndani yao utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na utiifu kwa Mtume wake (saw). Kaeni na watoto wenu na kujadiliana nao juu ya hukmu za Uislamu na muwafahamishe juu ya kile maadui wa Uislamu wanapanga juu yao, na muwaonye dhidi ya kufuata nyayo za Shetani au kushirikiana na maadui wa Uislamu, itikieni wito wa Mwenyezi Mungu Mtukufu pindi aliposema:

 [يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ]

Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.” [At-Tahrim 66:6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu