Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  15 Rabi' I 1443 Na: 1443 / 03
M.  Ijumaa, 22 Oktoba 2021

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

 [مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir Wilayah ya Jordan inaomboleza kifo cha mbebaji Dawah:

Hajj Abd Al-Raouf Muhammad Alyan Bani Atta (Abu Hudhayfah)

ambaye alikwenda kwa rehema za Mwenyezi Mungu (swt) jana, Alhamisi 21/10/2021 akiwa na umri wa miaka 60; alitumia miaka hiyo kumtii Mwenyezi Mungu na katika kubeba ulinganizi wa kuregesha tena maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume.

Hajj Abu Hudhayfah alikuwa makini kubeba Dawah popote alipotembelea au kusafiri, ambapo aliibeba Dawah katika nchi za Hijaz, Misri, Libya, na Jordan. Alibaki thabiti kama uthabiti wa milima iliyotia nanga, na dhamira isiyoyumba na azma iliyodumu, akitumaini kwamba Mwenyezi Mungu atamfanya aishuhudie Khilafah, mpaka amri ya Mwenyezi Mungu ilipokuja na ilhali juu ya hilo. Roho yake ilikwenda kwa Muumba wake, na jambo la mwisho aliloandika jana asubuhi kwenye ukurasa wake ilikuwa ni dua yake kwa Ummah wake:

 “Ewe Mwenyezi Mungu, urehemu udhaifu wetu, ponya maumivu yetu, na andaa ushindi kwa Umma wetu unaoupa utukufu wake na kuuwezesha kukutii na kukuabudu kwa kuhukumu kwa Sheria yako kama ulivyoamuru. Utukufu ni wako, hapana mungu wa haki ila Wewe hatuwezi kukusifu vya kutosha.”

Twamuomba Mwenyezi Mungu ammiminie rehma zake na amuingize katika pepo Yake pana na amlipe kwa niaba yetu na kwa niaba ya Uislamu na Waislamu malipo bora.

Ni cha Mwenyezi Mungu alichotoa na ni cha Mwenyezi Mungu alichochukua, na hatusemi isipokuwa yale yanayomridhisha Mola wetu (swt):

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

- Kalima ya Ustadh Bilal Al-Qasrawi katika mazishi ya Hajj Abd Al-Raouf Bani Atta -

- Kalima ya Ustadh Muhammad Al-Fuqaha katika Rambirambi za Hajj Abd Al-Raouf Bani Atta -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu