Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: 06:54:29 (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  2 Ramadan 1441 Na: 1441/10
M.  Jumamosi, 25 Aprili 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya Kisingizio cha Kuhifadhi Maisha ya Watu, Serikali Inarefusha Karantini na Kuongeza Ugumu kwa Watu na Hatua Ambazo Haingesubutu Kuzitekeleza Kabla ya Sheria ya Ulinzi!
(Imetafsiriwa)

Janga la maambukizi ya virusi vya Korona ambalo limesambaa ulimwenguni halikuwa sababu ambayo kwayo sheria ya ulinzi ilitekelezwa, mbali ya kuwa ilikuwa ni fursa ambayo utawala na serikali yake walikuwa wakingojea kuweka hatua na vizuizi ambavyo havihusiana na Karantini na tahadhari kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya Korona. Ushahidi wa hili ni ubunifu na mgongano ambao ulijitokeza kwa serikali katika maamuzi yake na sheria za ulinzi zinazo tolewa kila wakati kwa ili kurudi taratibu kwa maisha ya kawaida.

Hapo awali, ilitumia vitisho, uoga na hofu kutokana na janga hili ili kuweza kulazimisha hatua zake, kuwafungia watu kabisa na kuweka watu karantini katika nyumba zao na kusitisha maisha na utafutaji riziki, isipokuwa kwa nyakati na maeneo (iliyo yainishwa), pamoja na ukumbusho wa mara kwa mara wa janga ambalo lingekuwa lingetokea, ikiwa haingetanguliwa na ulinzi mkali. Mwezi umepita na sasa waziri mkuu anazungumza juu ya mwendelezo wa janga hilo kwa wiki na miezi, licha ya kupungua kwa kesi za maambukizi na udhibiti wa ugonjwa kwa jumla, ambayo inaonyesha kuwa serikali ya Jordan bado haijamaliza kuweka hatua inazotafuta kuzitekeleza kwa watu, ambayo ni kama fursa ambayo imekuwa ikitumiwa kutekeleza ukandamizaji laini ambao haukupatikana kabla ya virusi vya Korona. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ»

“Ewe Mwenyezi Mungu, yeyote atakaye pata aina fulani ya usimamizi wa mambo ya Ummah wangu kisha akawadhikisha – na wewe mdhikishe, na yeyote atakaye pata aina fulani ya usimamizi wa mambo ya Ummah wangu kisha akawa mpole kwao – basin a kuwa mpole kwake”.

Utawala na serikali yake zinaendelea kuzuia watu kufanya kazi ili kujipatia kipato, na kuwazuia kufungua maduka yao na kufanya mazoezi ya kununua na kuuza, isipokuwa kwa hali ya ukandamizaji ambayo iko mbali na mshikamano na ushirikiano, unaokaririwa na msemaji wa serikali kwa vyombo vya habari, na mbali na jukumu la utunzaji wa kweli. Serikali ilifanya unyang'anyi katika hali yake mbaya na shida zake, mtu yeyote anayetaka misaada ya kitaifa, ambayo hainenepeshi au kuondoa njaa (isiyo na maana), na yeyote anayetaka kuendelea na kazi yake na kufungua duka lake, inahitajika kujiandikisha katika Usalama wa Jamii hata kama usajili huu ni hiari, na kuna taasisi zaidi ya 100,000 ambazo hazijasajiliwa. Na wale ambao hawatimizi masharti haya hawataruhusiwa kufanya kazi. Je! Kuna unyanyasaji zaidi ya huu? Bali, kile ambacho serikali inataka ni habari ya kibinafsi, data, na hesabu ya idadi ya watu, na ufikiaji wa shughuli zao za kifedha, kuondoa mifuko yao na kuamsha ushuru usio halali na mfumo wa ushuru. kuongezea serikali kwa nguvu ilichukua mishahara ya kawaida ya wafanyikazi kwa kuzuia posho za raia na za kijeshi za mwaka huu, na kuzuia marupurupu ya walimu ambayo serikali hiyo ilijitolea mwanzoni mwa mwaka wa shule; Haya ndiyo malengo ambayo serikali hutafuta kutoka kwa masharti haya na taratibu zote.

Licha ya ripoti za mara kwa mara juu ya kudhibiti janga hilo katika maeneo mengi ya Jordan, isipokuwa katika maeneo ambayo vizuizi vimeondolewa, bado serikali inatabanni mawazo ya kidikteta katika kupambana na watu, kwa kutowawezesha watu kutekeleza ibada na swala za faradhi, na haswa swala za ijumaa, na faradhi ya Ramadhan kwa kuruhusu watu kuswali Qiyam na kufunga na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa njia bora katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, ambayo serikali inasisitiza kuifunga. Uhalifu huo umekuwa wazi kwa watu, takriban watu wote wanakubaliana juu ya hili, na nyudhuru za serikali zimekuwa dhaifu kuliko nyumba ya buibui, Mtume (saw) alisema:

«مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللَّهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ»

Hakuna mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atampa usimamizi wa raia, na afe hali ya kuwa amewadanganya raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamuharamishia juu yake pepo.”

Hatua za kiuchumi, ushuru na usaliti ambazo utawala na serikali yake inafuata kuwaruhusu wale tu ambao hufuata masharti yake kuepuka janga la Korona, na sheria za ulinzi ambazo inazitekeleza ambazo zinamomonyoa haki za watu na kuwatayarisha wao kuamiliana na nidhamu ya kiuchumi ya riba ya kirasilimali kwa kuamiliana na malipo ya kielektroniki, na kuendelea kufunga misikiti kwa uwezekano wa kuchukua hatua zinazofaa kuifungua, na kuwazuia wale ambao hufunga kwa kuweka amri ya kutotoka nje kabla ya Iftar, serikali isingesubutu kulazimisha hatua hizi zote kabla ya janga la Corona, na isingelisubutu sasa isipokuwa kwa dhihirisho la unyanyasaji na udhalilishaji unaofanywa, ambayo yako mbali na kisingizio cha kuhifadhi afya ya watu ambayo serikali na mawaziri wake hudai wakati inapo chukua hatua yoyote mpya.

Ummah amegundua zaidi michezo ya serikali, uongo, na ukosefu wake wa wasiwasi isipokuwa katika uwepo wake. Wasiwasi wake wote ni kufanya kazi tu juu ya kutekeleza mipango ya Taasisi ya Fedha ya Kimataifa na kutekeleza masharti ya mpango wa Trump, na sio wasiwasi wa maisha na afya ya watu, lakini badala yake kuwatawala na kuwahadaa wao kwa kukubali vipimo hivi. Makubaliano ya gesi na umbile vamizi la Kiyahudi yalianza miezi michache tu, ilhali idadi ya watu wote wameyakataa.

Kama ambavyo ufahamu wa Ummah unavyokua ya kwamba serikali hizi tawala zipo tu kutumikia makafiri wakoloni, na kutokomeza kitambulisho chake cha hadhara ya Kiisilamu, ufahamu wao na shauku ya kufanya kazi na wafanyikazi wa kurudisha serikali ya Khilafah Rashida ambayo iko makini kuiwezesha na kumridhisha Mola wake kwa kusimamisha ibada zake za swala, zaka na funga, na kuhifadhi matukufu yake na utajiri na kuwakomboa wao kutoka katika mikono ya makafiri wa kikoloni na vibaraka wao.

[الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجاً أُولَٰئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ]

“Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali” [Ibrahim: 3]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Wilayah Jordan

#Covid19    #Korona         كورونا#

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu