Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 24 Sha'aban 1441 | Na: 1441/09 |
M. Ijumaa, 17 Aprili 2020 |
(وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ)
“Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitajidi kuiharibu.” [Al-Baqara: 114]
Je, Sheria Haikukataza Kukatiza Swala za Ijumaa na za Jamaa
(Imetafsiriwa)
Waziri wa Wakfu na masuala ya Kiislamu nchini Jordan, Dkt. Muhammad Al-Khalayleh, juzi alitangaza mwendelezo wa kufungwa kwa misikiti katika Ufalme huo na kutoanzishwa kwa swala za Tarawehe katika misikiti na kujitolea kuzitekeleza majumbani, na akasema kwamba tunaupokea mwezi ulio barikiwa wa Ramadhan, lakini tutaswali katika nyumba zetu na kufungwa kwa misikiti wakati wa Ramadhan; hakuna Tarawehe wala swala za Ijumaa, ili kufikia madhumuni ya sheria za Kiislamu na kulinda maisha ya watu.
Kuhusiana na taarifa hii, tunaonyesha yafuatayo:
1- Unyonyaji wa Utawala nchini Jordan wa janga la virusi vya korona, na ukizingatia kuwa fursa ya kuendelea kufunga misikiti inathibitisha njia yake na kuelezea uadui wake wa wazi na wa siri kwa Uislamu na Waislamu, kutengwa kwa Uislamu na vifungu vyake vya kisheria kutoka uwanja wa vita vya maisha, na nia ya kufunga misikiti na kuzuia wajibu wa swala ambazo hufanyika tu katika misikiti, kama vile swala ya Ijumaa, na kwa kufanya hivyo, inatumika hadithi ya Mtume (saw):
«لَيُنْقَضَنَّ عُرَى الْإِسْلَامِ عُرْوَةً عُرْوَةً، فَكُلَّمَا انْتَقَضَتْ عُرْوَةٌ تَشَبَّثَ النَّاسُ بِالَّتِي تَلِيهَا، وَأَوَّلُهُنَّ نَقْضًا الْحُكْمُ، وَآخِرُهُنَّ الصَّلَاةُ»
“Hakika, mafundo ya Uislamu yatafunguliwa moja baada ya moja. Kila fundo moja likifunguliwa, basi watu hulikimilia lile linalofuata. Fundo la kwanza litakuwa ni utawala na la mwisho litakuwa ni swala” kwa kuwa imeacha kuhukumu kwa sheria za Mwenyezi Mungu na hapa inakataza kuswali katika misikiti.
2- Imegundulika kuwa serikali inatafuta, kupitia Kituo cha Kitaifa cha Usalama na Usimamizi wa Majanga, kuregesha maisha ya kawaida kwa sekta mbali mbali za jamii, pamoja na masoko makubwa, na kwa maeneo ambayo hayajaathirika na janga hili kama vile Aqaba, kwa uangalifu wake kuchukua hatua na tahadhari muhimu za kiafya na ni nini kinachofanikisha masilahi yake kabla ya kufanikisha masilahi ya watu Kwa hivyo, ikiwa ilikuwa na nia ya kufungua misikiti ingechukua hatua sawa na tahadhari, badala ya kutumia hoja ya Waziri wa Wakfu na kutaradhilia kwa maisha ya watu na kutumia mahitaji yao ya kufunga misikiti.
Nchi ambayo inasimamia kuingia kwa makumi ya watu katika masoko, mabenki na viwanda ambavyo ni maeneo yaliyo chafuliwa zaidi, inaweza kufanya vivyo hivyo kwa nyumba za Mwenyezi Mungu kuruhusu watu safi kuingia sehemu bora na safi kabisa duniani.
3- Kuzuia swala za Ijumaa na Jamaa wakati wa kuenea kwa majanga ya kuambukiza hakutekelezwi kiujumla, lakini badala yake wagonjwa ndio wanatengwa na hawaruhusiwi kuingia misikitini kwa swala za jamaa na ijumaa, na hatua zote zinachukuliwa kutoka kwa usafi na uoshaji mikono na kuvaa barakoa ikiwa inahitajika, na kadhalika, na watu wenye afya wanaendelea kuswali swala za Ijumaa na Jamaa bila kuwazuia.
4- Ushahidi juu ya swala za Jamaa na Ijumaa haujumuishi shida ya kudumu, lakini badala yake hazihitaji idadi kubwa ya utekelezaji wake, kwa sababu swala ya jamaa ni faradhi ya kutoshelezana ambayo lazima idhihirishwe kwa watu, kwa sababu ya maneno ya Mtume (saw):
«مَا مِنْ ثَلَاثَةٍ فِي قَرْيَةٍ وَلَا بَدْوٍ لَا تُقَامُ فِيهِمْ الصَّلَاةُ إِلَّا قَدْ اسْتَحْوَذَ عَلَيْهِمْ الشَّيْطَانُ، عَلَيْكَ بِالْجَمَاعَةِ فَإِنَّمَا يَأْخُذُ الذِّئْبُ مِنَ الْغَنَمِ الْقَاصِيَةَ»
“Ikiwa kuna watu watatu katika kijiji au katika jangwa ambapo swala hazitekelezwi (kwa Jamaa), shetani ametawala juu yao. Basi tekelezeni (swala) kwa jamaa), kwa kuwa mbwa mwitu humla mnyama dhaifu pekee.” [Imesimuliwa na Abu Dawud]
5- Ama swala ya Ijumaa, ni swala ya faradhi ya lazima (wajibu wa mtu binafsi), na haiondolewi isipokuwa kwa dharura, kwa sababu ya maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):
(إِذَا نُودِي لِلصَّلاَةِ مِنْ يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ)
“Enyi mulio amini, ikiadhiniwa swala siku ya Ijumaa, basi nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara.” [Al-Jumu’a: 9] na maneno ya Mtume (saw):
«الْجُمُعَةُ حَقٌّ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي جَمَاعَةٍ إِلَّا أَرْبَعَةٌ: عَبْدٌ مَمْلُوكٌ، أَوِ امْرَأَةٌ، أَوْ صَبِيٌّ، أَوْ مَرِيضٌ»
“Swala ya Ijumaa kwa jamaa ni jukumu la lazima kwa kila muislamu, isipokuwa watu wa nne; mtumwa, mwanamke, kijana, na mgonjwa.”
6- Kukimbilia kwa Waziri wa Wakfu juu ya uamuzi wa kuendelea kufunga misikiti mapema, yaani, siku kumi kabla ya kuanza kwa mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, inaonyesha nia ya kuwatenga waumini misikitini chini ya kisingizio chochote bila ya kushikilia uamuzi, hata wiki hadi wiki, kufuatilia matokeo ya kupungua kwa janga na kuwa na maeneo mengi huru kutokana na ugonjwa huo, ambayo ni dhahiri, badala ya uamuzi wa jumla wa muda mrefu. Kama kusema kuwa kuna uwezekano mdogo wa shaka kwamba kila mtu ana hatari ya kuambukizwa na haiwezi kuzuiwa, ni uwezekano dhaifu, haswa kwa kuwa idadi ya chini kabisa ya swala ya jamaa ni watu wawili na kwa swala ya Ijumaa ni watu watatu, na hii inawezekana kufikiwa. Kuchukua tahadhari haimaanishi kuacha wajibu, lakini badala yake hufanywa pamoja na kuchukua tahadhari na hatua za kuzuia maambukizi.
7- Ili kudumisha umakini wa kukataza swala ya jamaa na Ijumaa, serikali inaweka kwa makusudi kufungwa kabisa siku ya Ijumaa haswa, na hapa inafanya hivyo kwa Ijumaa ya tatu mfululizo na iliongezea Jumamosi ili kusiibuliwe shauku za kimakusudi za kuzuia swala ya Ijumaa na kuwazuia Waislamu kukusanyika katika makawanja kutekeleza swala za Ijumaa, ambayo inaonyesha dhamira yake ya kupiga vita mila ya Uislamu, haswa swala ya Ijumaa ambayo hutumika kama ishara ya umoja wa Waislamu na Mkutano wa kujadili masuala yao mapya, kuomba kwa Mwenyezi Mungu ili kuliondoa janga hili kutoka kwa Ummah wa Kiislamu.
8- Ni lazima kuwakataa watawala katika nchi za Kiislamu ambao hufuata nyayo za makafiri, shubiri kwa shubiri na dhira kwa dhira. Na ikiwa nchi hizo zinasumbuka kupata matibabu ya ugonjwa fulani, wanawafuata wao, na ikiwa wangependekeza suluhisho, hata kama haifai, watawala katika nchi za Kiislamu wangewapongeza, na kuzingatia kuwa ndani yake kuna afya na tiba! Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:
«سَتَكُونُ أُمَرَاءُ فَتَعْرِفُونَ وَتُنْكِرُونَ، فَمَنْ عَرَفَ بَرِئَ، وَمَنْ أَنْكَرَ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ قَالُوا: أَفَلَا نُقَاتِلُهُمْ قَالَ: لَا مَا صَلَّوْا»
“Kutakuwa na viongozi (watawala) mutawajuwa na muta yapenda matendo yao mema na kuchukia matendo yao maovu. Mtu anayeona kupitia matendo yao (na kujaribu kuzuia kuregelea kwao), ameondolewa lawama, na mtu anayechukia maovu yao (nyoyoni mwao, akiwa hana uwezo wa kuzuia kutokea kwake), pia yuko salama. Lakini mtu anayekubali matendo yao maovu na kuwaiga ameharibika kiroho.” Wakauliza, “Je, Haipaswi kupigana nao?” Akajibu: “Hapana, Maadamu bado wanaswali.”
Enyi Waislamu ... Enyi watu wetu nchini Jordan:
Dola ya Khilafah, inakuja hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, haitafuata njia za makafiri katika kushughulikia mambo kama haya, lakini badala yake itaongozwa na mwongozo wa Mtume (saw), kwa hivyo, swala ya Ijumaa au ya Jamaa haitositishwa. Badala yake, yule ambaye ana dharura ya kisheria anasamehewa hatohudhuria na wengine huhudhuria. Wagonjwa wanatengwa, na watu wenye afya huendelea kufanya kazi zao; wanakwenda misikitini kuswali na kumuomba Mwenyezi Mungu awalinde dhidi ya maovu ya ugonjwa huu. Huu ndio ukweli
(فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ)
“Na ni nini baada ya ukweli isipokuwa upotofu?” [Yunus: 32].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: |