Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  8 Dhu al-Hijjah 1441 Na: 1441 / 14
M.  Jumatano, 29 Julai 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pongezi Kutoka Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan
kwa Sikukuu ya Eid al-Adha Iliyo Barikiwa ya Mwaka 1441 H, sawia 2020 M
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha ila Allah...Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi Al Hamd
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu (swt) na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu na jamaa zake na Maswahaba zake na wale wanaomfuata yeye (saw), na wanaofuata nyayo zake na kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi wa fikra zao na hukmu za Shariah kipimo na chimbuko la matendo yao, na Khilafah kama nidhamu ya utawala.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan tunafuraha kutoa pongezi zetu za dhati kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, watu wa Jordan na Ummah wa Kiislamu kwa jumla, na kwa wabebaji Da'wah nchini Jordan na ulimwenguni; kwa sikukuu ya Idd ul-Adha iliyo barikiwa, tukimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuukubali utiifu wetu na amali zetu njema, na kuziregesha siku hizi zenye baraka hali ya kuwa nchi za Waislamu nimeungana katika dola moja chini ya kalima ya “La Ilaha ila Allah, Muhammadun Rasoolullah”, na hali Mwenyezi Mungu amezineemesha kwa kurudi Dola ya Khilafah. Mwaka wenu huu na uwe uliojaa kheri.

Kama tunavyo omba kila mwaka, kwa Yule Mungu Mmoja, Aishiye milele, Mwenye kuhuisha kutukirimu kwa Khilafah Rashidah, tunawakumbusha watu wa Jordan na Waislamu wote kwa jumla lile ambalo ni dhahiri mithili ya mwangaza wa jua mchana; la hali ambayo watawala wetu wametuletea ya udhalilifu, mateso, ukandamizaji na ukamataji kila anaye wahesabu kwa kulegea kwao dhidi ya maadui wao na kushirikiana kwao na wakoloni makafiri wa Magharibi, wakiongozwa na Amerika, kwa miradi inayozitawala nchi na watu, na hata kuwatuliza Mayahudi wadhalilifu kwa suluhisho lolote la kadhia ya Palestina; dola moja, dola mbili, au kutokuwa na dola kabisa, yote ni sawa maadamu hawawazingatii nyinyi, kwani wao wamo ndani ya bonde tofauti na bonde muliomo nyinyi.

Kuhukumu kwa mengine yasiyokuwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, yaani hukmu ya kisekula ambayo serikali inaitekeleza juu yenu, ndio msingi wa ufisadi uliozizonga huduma zote za dola, kuangamiza uchumi, hali ya madeni haramu ya riba imefikia idadi ya juu sana, kodi zimepanda, mifuko yenu kuporwa, ukosefu wa ajira kufikia kilele. Na hamupati badali ya hilo hata kwa uangalizi na usimamizi wa chini kabisa wa mambo yenu, hivyo wasiwasi wenu mkubwa umeishia kuwa ni namna gani ya kusimamia maisha yenu ya kila siku, kuelimisha watoto wenu na afya ya wagonjwa wenu,

 [فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلا يَضِلُّ وَلا يَشْقَى * وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً]

“basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika* Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Ta-Ha: 123-124]

Enyi Watu wa Jordan … Enyi Watu mnaomiliki Nguvu:

Katika Idd hii iliyo barikiwa, tunawakumbusheni tu jukumu lenu kwa Dini yenu ambayo kwayo uko ukombozi wenu na radhi za Mola wenu kwenu hapa duniani na Akhera. Na tunakumbusheni kuwa kimya chenu kuhusu dola yenu na hali ya kiza ya Ummah wenu haimridhishi Mola wenu ambaye amewaahidi ushindi na tamkini, hivyo basi onyesheni yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, na fanyeni bidii na kwa ikhlasi kuinusuru Dini yenu na mtekeleze Shariah yenu kupitia kufanya kazi ya kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu, tunamuomba Mwenyezi Mungu atubariki Idd inayokuja tuswali nyuma ya Khalifah muongofu atakaye tuongoza katika Msikiti wa Al-Aqsa, ambao hakuna tamaa ya kuukomboa isipokuwa kwa majeshi ya Kiislamu. Ummah wa Kiislamu haukati tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, na unatambua kwamba baada ya uzito ni wepesi, baada ya dhiki ni faraja, na baada ya kiza cha usiku itakuwa ni alfajiri… Hautikiswi na mateso, bali unafanya kazi na kufanya kazi kwa ikhlasi kwa Mwenyezi Mungu, waaminifu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), wala hawadhuriwi na wale wanaopotoka au kupotea njia kutokana nao, kwani Ummah huu haukubali badali yoyote ya Uislamu.  

 [وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu