Afisi ya Habari
Kenya
H. 1 Muharram 1442 | Na: 1442/01 H |
M. Alhamisi, 20 Agosti 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uzinduzi Rasmi wa Kampeni ya Hizb ut Tahrir / Kenya Chini ya Kauli Mbiu 'Kila Mmoja Wenu ni Mchungaji'
Janga la maambukizi ya virusi vya Korona linaendelea kuchua maisha ya watu wengi ulimwenguni pia limepelekea kusitishwa kwa amali nyingi za kiuchumi; na kuharibu njia za watu za kujikimu kimaisha. Pia limepelekea kufungwa kwa taasisi za masomo ambapo imesababisha janga jengine nchini Kenya; ongezeko la mimba za wasichana wa shule. Data kuhusu mimba za matineja iliyotolewa hivi majuzi inaonyesha takriban wasichana wa shule 152,820 kote nchini wamepachikwa mimba tangu kufungwa kwa shule. Ingawa serikali imepuuzilia mbali tarakimu hizo ikizitaja kama za kuchukiza, ukweli bado ungalipo kuwa vitendo vya ngono ni miongoni mwa maovu yaliyokithiri ndani ya jamii ya kisekula.
Kwa wasiwasi mkubwa, Hizb ut Tahrir / Kenya inazindua kampeni kubwa chini ya mada: "Kila Mmoja Wetu ni Mchungaji" kuanzia tarehe 25 Agosti 2020 hadi 31 Disemba 2020.
Msururu wa matukio wakati wa kampeni hii utajumuisha darsa za ummah misikitini, jaula mitaani na midahalo ya moja kwa moja, miongoni mwa mengine. Mada kuu ya mazungumzo itakuwa ni namna gani Urasilimali na itikadi yake potofu ya usekula zimechangia sio tu janga la kijamii bali majanga yote katika kila nyanja ya maisha. Ummah unaojumuisha wazazi na walezi watakumbushwa kuhusu jukumu lao la kuwalinda watoto wao kutokana na uvamizi wa thaqafa ya Kimagharibi kupitia kuhakikisha kuwa wanaasisi Kitambulisho cha Kiislamu katika watoto wao.
Tunausihi ummah kujiunga nasi katika kampeni hii kwani ni sehemu ya kazi tukufu ya kuamrisha mema (Maa’ruf) na kukataza maovu (Munkar).
Fuatilia alama ishara za kampeni:
#Covid-19_Inafichua_Urasilimali
#Covid-19_Usekula_Unatenganisha_Dini
#Covid-19_ Majanga_ya_Umma_yaliogeuzwa rasilimali_na_Warasilimali
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |