Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  22 Muharram 1441 Na: 1441 / 04
M.  Ijumaa, 17 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Kenya iliandaa amali wakati wa kampeni ya kiulimwengu: Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema ikatimia inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine

Chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Maarufu, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amuhifadhi, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir imezindua kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio adhimu la Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli (mji wa Heraclius) ambao ulizingirwa kuanzia 26 Rabii' al-Awwal hadi 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M na hivyo bishara njema ya Hadith tukufu ya Mtume (saw) ilitimia:

«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»

“Konstantinopoli itafunguliwa, na Amiri bora ni Amiri wake, na jeshi bora ni jeshi hilo.”

Hizb ut Tahrir / Kenya iliadhimisha kampeni hii mnamo Januari 13, 2020 kupitia kipindi cha redio cha moja kwa moja kilicho andaliwa na Radio Rahma. Katika kipindo hicho, Shabani Mwalimu, Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Kenya, pamoja na mwenzake katika Afisi ya Habari Ali Omar walijadili kuhusu ukombozi wa Konstantinopoli: bishara njema ikatimia inafuatiwa na bishara njema nyingine.

Mnamo Jumatano, 15 Januari 2020 M, sawia na 20 Jumada al-Awwal 1441 H, mashababu wa Hizb ut Tahrir Kenya waliandaa msururu wa maandamano baridi na mihadhara kote nchini. Jijini Mombasa, maandamano baridi yalifanywa nje ya Msikiti wa Al Aqsa – Kisauni, Msikiti wa Khairat – Kilifi na Msikiti wa Lungalunga. Wakati wa maandamano hayo baridi, Mashababu walikuwa na mabango yanayosomeka: "Ufunguzi wa Konstantinopoli Bishara Njema ikatimia… Inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine! Kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Mtume (saw), kupigana na kuwashinda Mayahudi, na kukombolewa Roma."

Katika siku hiyo hiyo baada ya swala ya Maghrib, mihadhara iliyo ongozwa na Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Kenya Shabani Mwalimu ilifanywa jijini Mombasa, Nairobi na Kilifi.

Mihadhara hiyo ilikuwa ni kuwakumbusha Ummah kuwa na hakika ya kutimia kwa bishara njema tatu nyingine za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa kuwa moja tayari ishatimia kwani Mtume (saw) huzungumza kwa kupitia Wahyi pekee. Zaidi ya hayo, Mashababu walisisitiza kuwa bishara hizo njema hazitotimia kupitia malaika wema kutoka mbinguni, ambao watawatunukia juu yao. Bali, Sunnah ya Mwenyezi Mungu ni kuwa tutakapo mnusuru Mwenyezi Mungu yaani kufanya kazi kusimamisha tena Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume, basi bila shaka atatuletea ushindi Wake kwetu.   

 (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

“Na siku hiyo Waumini watafurahi* Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu