Afisi ya Habari
Kenya
H. 20 Jumada II 1441 | Na: 1441/07 |
M. Ijumaa, 14 Februari 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uzinduzi Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Kenya wa Kampeni Pana Chini ya Kauli Mbiu: BBI Mchezo Ule Ule Mbinu Mpya
Hizb ut Tahrir / Kenya inafuraha kuzindua rasmi Kampeni Pana ambayo itakwenda kwa miezi mitatu kwa kauli mbiu "BBI Mchezo Ule Ule Mbinu Mpya" kuanzia mnamo Jumamosi 15 Februari 2020 na kumalizika 24 Mei 2020.
Ripoti ya Mradi wa Kuunganisha Daraja (BBI) iliyochapishwa katika gazeti rasmi la serikali mnamo 24 Mei 2018 na ikawekwa hadharani kwa umma mnamo Novemba mwaka jana ili kujadiliwa na umma, imeonekana kama 'Alfajiri Mpya' na kudhaniwa kuwa italeta umoja, mapinduzi ya kiuchumi na kupambana na kasumba ya watu fulani tu kukwamia madarakani na ufisadi-sugu ambayo ni majanga ya kudumu yanayoikumba Kenya kwa zaidi ya nusu karne. BBI, ambayo tayari imesababisha migawanyiko ndani ya tabaka la kisiasa, inajiri chini ya miaka kumi tu tangu kuidhinishwa kwa Katiba mpya iliyo anzisha nidhamu mpya ya serikali za ugatuzi na bado nchi ingali inakabiliana na matatizo yayo hayo.
Kampeni hii inalenga kuangazia shina la majanga yote yanayoikumba Kenya na ulimwengu kwa jumla ambalo si jingine ila ni Urasilimali na nidhamu yake ya kisiasa ya Demokrasia inayoyapa kipaumbele maslahi ya viongozi wa kisiasa ambao kwa kiburi huwaacha wengi wakiteseka maishani mwao. Pia itawasilisha nguvu ya itikadi ya Kiislamu katika kufungamanisha pamoja mujtama kwa kudumu kama taifa moja, wote wakiwa ni waja wa Mwenyezi Mungu (swt) pamoja na kutoa utatuzi wa changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii zinazoukabili sio tu mujtama wa Kenya pekee bali wanadamu wote.
Katika kufaulisha Kampeni hii, Hizb ut Tahrir / Kenya itaandaa amali kadhaa zikiwemo mihadhara katika sehemu tofauti tofauti, matembezi mitaani, kuandaa warsha pamoja na wasomi na wanafikra mashuhuri miongoni mwa amali nyinginezo.
Katika kutamatisha, tunatoa wito kwa Ummah kwa jumla hususan Ummah wa Waislamu kushiriki pamoja nasi katika kampeni hii tukufu ambayo tunalenga kuiwasilisha kwa upana ambayo itatusaidia katika Dunia hii na Akhera.
Fuatilia alama ishara za kampeni:
#BBIOldGame_NewStrategy
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |