Afisi ya Habari
Kenya
H. 16 Ramadan 1441 | Na: 1441/10 |
M. Jumamosi, 09 Mei 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali kuongeza hofu nyengine ya njaa baada ya ile ya Virusi vya Korona!
Kama hatua yake mpya ya kukabiliana na janga la kiulimwengu la Virusi vya Korona, serikali imeamua kuyafunga maeneo mawili yenye idadi kubwa ya Waislamu ambayo pia ni vituo muhimu vya kibiashara; Eastleigh Jijini Nairobi na Old Town, Mombasa. Madai ya Serikali kuwa hatua hio haikuchukuliwa kwa nia ya kuadhibu wakaazi wake, bali ni kwa malengo ya kulinda maisha ya wakenya dhidi ya maambukizi, kwa kuwa maeneo hayo yamerekodi visa vingi vya Covid-19.
Hatua hii itaendeleza zaidi hali mbaya ya kiuchumi hasa ikizingatiwa kwamba maeneo hayo hutumiwa na watu wengi katika kuendesha biashara kama njia ya kuweza kukimu mahitaji yao kila siku. Hatua ya kuweka vikosi vikubwa vya polisi inaonyesha wazi kwamba marufuku hiyo ya kuzuia kuingia na kutoka maeneo hayo kwa siku kumi na tano, ni kuwaadhibu na kuwanyanyasa wakaazi wake kiuchumi. Ni bayana kwamba serikali imeamua kuongeza hofu nyengine ya njaa kwa raia wake baada ya ile ya maradhi ya Korona. Cha kutamausha ni kwamba vikosi vya usalama vinavyo hakikisha marufuku hiyo inatekelezwa, havikuonekana pindi magenge ya vijana yalipokuwa yakitekeleza uhalifu dhidi ya wakaazi wa Old Town. Na huku serikali ikidai kuwa hatua yake hiyo ni kujali maisha ya raia wake, maajabu serikali imepuuza raia wengine walioachwa bila makao kwa sababu ya mafuriko! Linalo huzunisha ni kuwa tokea msimu wa mvua za masika kuanza hadi sasa mafuriko tayari yameua zaidi ya raia 100!
Tunasema kuwa, dola za kirasilimali huyapa kipaumbele mapato ya kiuchumi juu ya maswala ya kiafya, wakuu wa serikali ya Kenya waliruhusu ndege kutoka China kutua humu nchini baada ya mkurupuko wa maradhi ya Korona huko China. Na sasa kinacho onekana ni kwamba serikali inacheza mchezo wa kuwatupia lawama raia wake ilhali iliruhusu virusi hivyo kuingia nchini.
Kimsingi, suala upimaji maradhi hayo ni jambo zuri, ila hatua ya raia kususia zoezi hili inamaanisha kwamba hawana imani na viongozi ambao wamekuwa na mazoea ya kuhadaa raia kila siku. Mifumo duni ya kiafya na takriban huduma zote za kijamii yote haya yamewafanya raia kutokuwa na imani na Serikali. Tayari kuna ripoti kwenye baadhi ya vyombo vya habari zinazo onesha watu wakitoroka vituo vya karantini za serikali viko katika hali mbaya na wengine kutishia kujitoa uhai wao kwa sababu ya shida wanazo kumbana nazo.
Kwa ujumla, maambukizi haya ya virusi vya Korona yametuonyesha kwamba umma sio tu nchini Kenya bali ulimwengu kwa jumla umekosa usimamizi wa kikweli wa mambo yao. Na kwamba viongozi wa kisekula kote duniani huwabwagia lawama na kuwatisha raia wao kama njia mojawapo ya kujaribu kuficha utepetevu wao wa kila mara. Hivyo kuna haja kubwa sana ya umma kote duniani kufanya kazi na Hizb ut-Tahrir kuleta uongozi unaojali kweli maisha ya watu sio kwa misemo tu bali kwa vitendo. Uongozi huo sio mwengine bali ni Khilafah ambao kiongozi wake hatochukulia utawala kama chombo cha kunyanyasa raia wake kwani atafahamu kwamba kuna siku ataletwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mfalme wa wafalme ahesabiwe jinsi gani alivyo endesha uongozi wake. Serikali hiyo ni Khilafah kwa njia ya Utume ambayo kikweli raia ndio watakuwa na imani nayo.
Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kenya |
Address & Website Tel: +254 707458907 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke |