Watoto wa Iraq … Uhalisia Unaoogofya na Mustakbali Unaotoa Bishara ya Miaka Mingi ya Kuzorota!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hazina inayoshughulikia maswala ya watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF) imesema katika ripoti iliyotolewa mnamo Ijumaa 19/1/2018 kuwa watoto 270 waliuwawa nchini Iraq mwaka jana kwa sababu ya vita vilivyo anzishwa na serikali ya Iraq dhidi ya ISIS. Vita hivi pia vilisababisha watoto 1.3 milioni kukosa makao miongoni mwa 2.6 milioni waliokosa makao kutokana na vita hivi vya miaka mitatu. Kulingana na taarifa hiyo, watoto milioni nne katika mikoa ya Nineveh na Anbar waliathirika na ghasia hizo na watoto wengi walilazimika kushiriki katika vita safu za mbele. Taarifa hiyo ilifichua kwamba umasikini na mizozo ilisababisha kusita kwa mchakato wa elimu kwa watoto milioni tatu kote nchini Iraq, baadhi yao wakikosa kabisa fursa ya kukaa ndani ya darasa katika maisha yao yote, huku zaidi ya robo ya watoto wa Iraq wakiishi ndani ya umasikini.