Yemen yakabiliwa na baa la njaa la kutisha lililowahi kutokea ndani ya miaka 100 ya ulimwengu likisababishwa na mzozo kati ya Uingereza na Marekani ambao umeutia nchi hiyo katika vita wasivyostahiki wakiongozwa na vibaraka wa kitaifa na kieneo!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa mujibu wa duru za Umoja wa Mataifa, Yemen kwa sasa inakabiliwa na baa la njaa baya zaidi ulimwenguni kwa miaka 100. Uzani wa janga hilo umefananishwa na ule uliokumba Afrika katika miaka ya themanini. Ripoti ya hivi majuzi ya shirika la habari la BBC imenukuu kuwa kwa mujibu wa Lisa Grande, Msimamizi wa Misaada ya Kibinadamu wa UN nchini Yemen, zaidi ya raia milioni 13 wako katika hatari ya kufa kutokana na ukosefu wa chakula katika miezi mitatu ijayo