Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  20 Jumada I 1440 Na: 1440/013
M.  Jumamosi, 26 Januari 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maradhi ya Utaifa Yamepelekea Kukamatwa kwa Wanawake na Watoto Wanaonyanyaswa wa Rohingya na Serikali ya Saudia

Mamia ya Waislamu wa Rohingya wanawake na watoto, waliokimbia mauwaji na ubakaji wa halaiki kutoka kwa Mabudha wenye misimamo mikali nchini Myanmar, wanaendelea kuzuiliwa pasipo kujulikana hatima yao katika Kituo cha Kizuizi cha Shumaisi nchini Saudi Arabia, baada ya kutafuta hifadhi katika dola hiyo. Baadhi yao wamefungwa jela kwa zaidi ya miaka 5 baada ya kuingia nchini humo – kwa madai ya kuwa na stakabadhi za usafiri zisizo halali. Imeripotiwa kuwa baadhi ya wanawake wa Rohingya walio kamatwa na mamlaka za Saudia huku wakiwa waja wazito, walilazimika kujifungua watoto wao wakiwa kizuizini. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wafungwa hao, wanateseka kutokana na msongamano wa watu na hali nyengine za maisha zisizo vumilika kituoni humo. Hii, pamoja na kurefuka kwa muda wa uzuizi imesababisha magonjwa ya kiakili miongoni mwa wafungwa wengi wa Rohingya, huku wengine wakiugua kutokana na maradhi tofauti tofauti kama vile malaria, kisukari na maambukizi ya fangas wakiwa bado hawajapokea matibabu yanayostahiki. Mapema mwezi huu imeripotiwa kuwa serikali ya Saudia iliwafurusha mamia ya wakimbizi wa Rohingya hadi nchini Bangladesh na kwamba inapanga kuwafurusha mamia zaidi. Ima watakabiliwa na kifungo cha serikali ya mhalifu Hasina au watakabiliwa na maisha ndani ya kambi duni mno “kambi za mauti” katika Cox Bazaar ambazo hazistahiki hata wanyama!   

Ni gonjwa sugu la utaifa ndilo linalo zalisha unyama kama huu na linalo sababisha serikali ya Saudia kuwachukulia ndugu na dada zao Waislamu wa Rohingya wanaoteswa kama wageni na wahalifu, kwa sababu tu wanatoka katika nchi tofauti, badala ya kuwapa hifadhi na kuwakidhia mahitaji yao msingi kama inavyo wajibishwa na Uislamu, kwani Mtume (saw) amesema,

«الْمُسْلِمُ أَخُوْ الْمُسْلِمِ، لا يَظْلِمُهُ، وَلا يَخْذُلُهُ»

“Muislamu ni ndugu yake Muislamu:hamdhulumu, wala hamtelekezi.”

Ni jambo la kuchukiza mno kuwa serikali ya Saudia iko tayari kutumia mabilioni ya dolari kuchinja na kuwanyima chakula Waislamu wa Yemen lakini haiko tayari kuwapa Waislamu wa Rohingya wanaoteswa hifadhi na mustawa mzuri wa maisha. Hakika, sio Rohingya wanaopaswa kuchukuliwa kama wahalifu bali ni watawala wa Saudia, Bangladesh na kwengineko katika ulimwengu wa Kiislamu kwa uhalifu wao dhidi ya Ummah huu wa Kiislamu – ikiwemo kuwatelekeza Waislamu wanao dhulumiwa.

Rohingya sio wageni katika ardhi hii, kwani hiii ni ardhi ya Ummah mzima wa Kiislamu … na wala sio mali ya wafalme madhalimu kuamua ni raia yupi Muislamu anastahiki kuingia au la! Hii ni ardhi iliyosifiwa kuwa tukufu na Allah (swt), ardhi ambayo ndio mahali pa mazazi ya Uislamu, na ardhi ambayo Mtume (saw) alisimamisha Dola ya Kiislamu juu yake. Waislamu wa Rohingya, na hakika kila Muislamu anastahiki kuingia na kuishi bila ya hofu ya kukabiliwa na sura mpya ya mateso. Kile kilicho kigeni katika ardhi hii ni ile serikali ya ubaraka inayo saidiwa na mkoloni Mmagharibi na utawala unaoendeshwa kwa matakwa ya madikteta ambao hauna uhusiano kamwe na Uislamu na unajitokeza kwa sera hizi za kitaifa zilizo chukuliwa kutoka kwa Wamagharibi makafiri, kwani Mtume (saw) amesema kuhusiana na uzalendo,

«دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ»

“Uacheni hakika huo ni uvundo.”

Enyi Waislamu! Waislamu wanao dhulumiwa hawatakuwa na hifadhi, wala ulinzi kwa maisha yao na mali zao, na wala maisha ya izza chini ya serikali hizi za kitaifa na watawala vibaraka wanaotawala juu ya ardhi zetu, kwani wao hawajali lolote kukomesha umwagikaji wa damu na kulinda utukufu na maisha mazuri ya Ummah huu. Badala yake wao ndio wameifanya kuwa misheni yao ili kutimiza ajenda ya mabwana zao wa kimagharibi ili kudumisha mgawanyiko kwa Ummah huu kupitia mipaka yao bandia ya kitaifa iliyo lazimishwa na wakoloni na vitambulisho vya uraia wa nchi iliyo pelekea Waislamu kuwatelekeza, kuwauwa, kuwafunga na kuwanyima hifadhi ndugu zao na dada zao Waislamu. Ni lazima tuzing’oe serikali hizi zilizooza na kanuni zao zilizotungwa na wanadamu na kwa haraka kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itakuwa ndio mlinzi wa kweli na ngao ya Ummah. Itaondoa mipaka yote bandia ya kitaifa inayo wagawanya Waislamu na kuunganisha ardhi zetu zote chini ya bendera moja na mtawala mmoja. Vile vile itahami matukufu ya Waislamu na kuwapa hifadhi na kuwakidhia mahitaji yao yote – bila ya kuzingatia rangi, kabila au ardhi asili wanakotokea – kwani hii ndio Amri ya Allah (swt). Mtume (saw) amesema,

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

“Hakika Imam (Khalifah) ni ngao; watu hupigana nyuma yake na hujihami kwayo.”

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu