Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  10 Safar 1442 Na: 004 / 1442 H
M.  Jumapili, 27 Septemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wazimu wa Wanasiasa wa Kifaransa kwa Hijab Unajumuisha Hofu ya Uislamu na Kasumba ya Usekula

(Imetafsiriwa)

Siku ya Alhamisi Septemba 17, wabunge wa Ufaransa kwa mara nyengine tena waliweka wazi ubaguzi wa rangi, dhidi ya Uislamu, wa serikali ya kisekula uliokithiri nchini Ufaransa kwa upande wa kutoka bila sababu katika kikao cha uchunguzi kilichofanyika katika Bunge la Ufaransa, kupinga uwepo wa mwakilishi wa wanafunzi aliyevaa khimar (kitambaa cha kichwa cha Kiislamu). Mchakato wa kujiondoa uliongozwa na Anne Christine Lang, mbunge wa chama tawala cha Rais Macron (Jamhuri Mbele), akiungwa mkono na wabunge wengine kutoka chama cha mrengo wa kulia cha Republican. "Siwezi kukubali kwamba katikati ya Bunge, moyo wa demokrasia ... tunakubali uwepo wa mtu aliyevaa hijab mbele ya kamati ya uchunguzi ya bunge," Lang alisema baadaye kwenye video iliyochapishwa kwenye Twitter. Alitoa maoni pia katika nukuu yake kwenye Twitter, akisema: "Kama mwanamke anayethamini misingi ya jamhuri, misingi ya kisekula na haki za wanawake, siwezi kukubali mtu yeyote aje kushiriki katika kazi yetu katika Bunge la Kitaifa huku amejifinika hijab, ambayo inabaki kwangu kuwa ni ishara ya kujidhalilisha." Na mwanamke wa Kiislamu aliyekuwa amevaa hijab, Maryam Pougetto, kiongozi wa Muungano wa Kitaifa wa Wanafunzi wa Ufaransa, alikuwepo kwenye kikao hicho cha bunge ili kushughulikia suluhisho la athari za Covid-19 kwa vijana na watoto. Dada huyo wa Kiislamu pia alihujumiwa mapema mnamo 2018 na wanasiasa kadhaa, pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Usawa wa Jinsia wa wakati huo, kwa kutawalishwa nafasi ya kiongozi wa Chuo Kikuu cha Sorbonne katika Muungano wa Kitaifa wa Wanafunzi wa Ufaransa akiwa amevaa hijab wakati wa safari ya shule pamoja na mtoto wake wa kiume kwenda katika bunge la jimbo huko Bourgogne-Franche-Comte, mashariki mwa Ufaransa, alidhalilishwa kutoka kwa mwanasiasa wa kulia wakati wa mkutano wa Baraza la Bunge. Na akamtaka avue hijab yake "kwa jina la misingi ya kisekula." Na katika mwaka huo huo, Rais wa Seneti, Gerard Larch, aliweka wazi akimaanisha "hijab", ​​kwamba ilikuwa dhidi ya "kila kitu kinachoweza kuwafunga wanawake.".

Wanasiasa wenye msimamo mkali wa Kifaransa wa pande zote za kisiasa wanaonekana wameamua kuendelea kukuza hadithi ya uwongo, iliyopitwa na wakati na ya wakoloni kwamba mavazi ya Kiislamu yanawakandamiza wanawake. Je! Sio wakati sasa wa kuingia karne ya ishirini na moja na kugundua kuwa ni kauli zao, vitendo na sheria za kupinga Uislamu ambazo zinanyamazisha, zinaweka kando na kuzuia maisha ya umma ya wanawake wa Kiislamu na kugeuza usimamizi wao kuwa wa daraja la pili ndani ya jamii na kuwalazimisha kuishi kwa kujisalimisha kwa maagizo ya kibaguzi ya wanasiasa wenye fursa ambao hucheza na jamii ndogo ili kunyanyua cheo chao cha uchaguzi?! Kwa kuongezea, kupagawa huku kwa kisekula kutokana na hijab si chochote isipokuwa ubaguzi halisi na chuki dhidi ya wageni iliyofichwa nyuma ya mazungumzo ya kike na haki za wanawake! Rekodi ya Ufaransa katika kupambana na hofu ya Uislamu inajulikana. Kwa kweli, tangu Ufaransa ilipotangaza hali ya hatari mnamo Novemba 2015, imehusika katika uvamizi kadhaa wa kibaguzi na ukamataji kwa nguvu dhidi ya Waislamu, ikilenga zaidi ya nyumba 5,000, maduka, na maeneo ya ibada ya Waislamu.   

Waislamu katika nchi nyingine nyingi za kisekula - Mashariki na Magharibi - pia wamefanyiwa sera na sheria za kibaguzi na za ukandamizaji, pamoja na marufuku ya hijab na niqab. Yote haya yanathibitisha ukweli kwamba kasumba ya kidini imekita mizizi katika mfumo wa kisekula, ambao haufai kuwatawala wanadamu. Je! Ni serikali ya aina gani hii ambayo inawaunda wanasiasa wanaoyatazama mavazi ya kidini kuwa ni hatari zaidi kuliko athari za janga hatari?! Kwa kuongezea, ni aina gani hii ya mfumo wa kuchekesha unaobeba dharau kwa usemi wa haya, huku ukiruhusu maoni juu ya fikra na picha zote chafu na fisidifu katika jamii yake, pamoja na filamu za ngono? Mtazamo huu uliopotoka wa maadili umejumuishwa katika maneno ya Rais wa Ufaransa Macron, ambaye ametetea kwa nguvu kuchapishwa tena kwa vikaragosi vya kuchukiza dhidi ya Nabii wetu mpendwa (saw), kwa msingi wa mfumo wa kisekula wa uhuru wa kujieleza, wakati hapo awali alisema kuwa hijab (vazi la heshima) "haiendani na ustaarabu (hadhara) wa nchi yetu"!

Kwa sifa yetu kama Waislamu, hili lazima liwe ni ukumbusho mkali kwetu kwamba mfumo mbovu wa kisekula, wenye kuathiri migawanyiko, na kupingana na Uislamu unasimama kwa upinzani kamili wa dini yetu, na kwa hivyo lazima tukatae kikamilifu utekelezwaji wake katika nchi zetu! Kwa kweli, mfumo pekee unaokubalika mbele ya Mwenyezi Mungu na ambao utalihami vazi la Kiislamu na imani zetu zote imara za Kiislamu ni mfumo wa Khilafah kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

﴿وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الإِسْلاَمِ دِيناً فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

"Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri." [Aali-Imran: 85]

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu