Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  4 Rabi' II 1442 Na: 1442 H / 011
M.  Alhamisi, 19 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watoto wa Ummah wa Kiislamu Wanazama Baharini na Serikali Zinawapuuza Huku Zikikimbilia kutoa Masharti ya Uaminifu na Utiifu kwa Dola za Kikoloni!

(Imetafsiriwa)

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa lilitangaza, mnamo siku ya Alhamisi tarehe 12/11/2020, kwamba wahamiaji 74 waliuawa wakati boti lao lilipozama katika pwani ya Libya. Katika taarifa, shirika hilo lilitangaza kuwa "watu 74 waliuawa baada ya boti lao kuanguka leo katika pwani ya Al Khums nchini Libya." Taarifa hiyo iliongeza kuwa boti hilo lilikuwa limebeba watu 120, wakiwemo wanawake na watoto, na Walinzi wa Pwani na wavuvi walifanikiwa kuokoa watu 47, huku miili 31 ikiwa imepatikana hadi sasa, wakati shughuli ya utafutaji wa wengine waliopotea ikiendelea. Kulingana na data ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, hadi kufikia Oktoba iliyopita, watu wasiopungua 900 walizama katika Bahari ya Mediterania wakati wakijaribu kufika pwani za Ulaya, baadhi yao kutokana na kucheleweshwa kwa shughuli za uokoaji.

Katika nchi hii yenye utajiri wa mafuta, pande mbili za mzozo, Khalifa Haftar na Fayez al-Sarraj, na wafuasi wao si kitu bali ni vibaraka wa mamlaka ya kikoloni. Nchi hizi zinazoamiliana na hali katika nchi hii kulingana na maslahi ambayo watafikia, bila ya kujali mtawanyiko, umaskini na upotezaji unaoweza kuwakumba watu wake. Vita vinavyoendelea nchini Libya vimewasukuma watu kwa kile kinachoitwa "uhamiaji usio na mpangilio," ambapo maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wameuawa. Bahari ya Mediterania huwafukuza kama maiti au wanabaki idadi tu katika orodha ya watu waliopotea. Kila mtu hukimbia ama kwa kuogopa kuuawa kwa maangamivu ya mabomu au kufa njaa kutokana na kuzorota kwa hali, gharama kubwa ya maisha na kupanda bei. Katika "boti za kifo" maelfu ya watu hujitupa baharini, wakitumaini kufikia nchi yoyote ya Ulaya itakayowakumbatia ili kuishi maisha mazuri. Lakini uhalisia ni kinyume na hivyo ambapo huregeshwa katika nchi zao kukabiliwa na kifungo, unyanyasaji, kudhulumiwa na kulanguliwa na hali yao inakuwa kama ya yule atafutaye usalama kutokana na joto kali katika moto! Aghlabu hurudishwa nchini mwao kuteseka kutokana na kuvunjika moyo (watu wengine 11,000 wamerudishwa Libya, kulingana na linavyoashiria shirika la UN.)

Matukio kama hayo, ambayo maelfu ya wahasiriwa wasio na hatia wanauawa, yanarudiwa mara kwa mara, na mateso yanaregeshwa upya. Hii ni ajali ya nane ya boti kunazama zinazobeba wahamiaji katika bahari ya Mediterania, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji. (RT, 12/11/2020) Je! Ni nidhamu gani hii ambayo haiwajali watu au kulinda maisha yao?! Je! Ni nidhamu gani hii inayowatupa vijana kuzimu ya kukata tamaa na kuchanganyikiwa kukimbia kutoka kwa uhalisia wao kwenda kwa ulimwengu wa uhalifu na uraibu, au kwa kifo kuungua, kujinyongwa, au kuzama? Sura mbaya ya mfumo mbaya wa kiulimwengu ambao huharibu tu maisha ya watu na kudhikisha chumo lao, na hali mbaya na shida ambazo ulimwengu unashuhudia leo ambazo zimetwika mzigo kwenye mabega ya vijana kabla ya wazee na wanawake kabla ya wanaume ni ushahidi la watu kuhitaji kuutema mfumo huu mbovu na uliofeli na kuutupa nje ya maisha, na kurudisha mfumo wa Uislamu ambao hurekebisha mambo ya watu na kuwaondoa katika maisha ya shida na taabu hadi maisha ya usalama, furaha na kuridhika na hukumu zake za haki za kamilifu za kimungu.

Hakika mfumo wa Uislamu ndio pekee wenye uwezo wa kutoa mahitaji ya watu na kuwapata kupitia mgao wake wa haki wa mali. Ni mfumo unaomtunza mtu kama mwanadamu ambaye ana mahitaji na ghariza ambazo hazina budi zidhaminiwe ushibishaji wake. Hukmu za Mola wa Walimwengu zimekuja ili kubainisha hilo na kufanya kazi kulitekeleza hilo na Dola ya Kiislamu kwa zama nyingi ilijaa matukio yaliyobainisha kiasi ambacho kujitolea kwake kusimamia mambo ya raia na kuhakikisha utoaji wa wale wanayoyahitaji; iliwasaidia vijana ambao hawakumudu gharama za ndoa kuoa, na kuwapa wasio na ajira kazi, bali hakika usimamizi waje ulijumuisha mpaka kwa wanyama na ndege, kwa hivyo ilitengeneza barabara na kueneza nafaka milimani.

Enyi Ummah wa Uislamu na enyi vijana wa Ummah huu: nyinyi ni Ummah bora aliouleta Mwenyezi Mungu kwa watu, kwa hivyo msikate tamaa au kuvunjika moyo, kwani sisi ni Ummah ambao haukati tamaa na Rehema ya Mwenyezi Mungu, sisi ni Ummah ambao Mwenyezi Mungu ameuchagua kwa ufunuo bora zaidi ya yale yaliyofunuliwa katika mwongozo na hukumu zinazoongoza maisha yake vizuri, bali zinazoongoza maisha ya watu wote, kwa hivyo vipi basi tunabadilisha kilicho bora kwa kilicho duni?! Rudi kwa Mola wenu na mfumo wake, ambao aliuteremsha kwa Kipenzi chake, Mteule, swala bora, salamu takatifu zimshukie, na ulinganieni uhukumu, na fanyeni kazi pamoja na wafanyikazi kuregesha maisha kamili kwa Uislamu.

وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿

"Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu" [Aali-Imran: 133]

Kitengo cha Wanawake

Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu