Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  22 Jumada II 1443 Na: 1443 H / 021
M.  Jumanne, 25 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tunawakabidhi kwa Mwenyezi Mungu, Enyi Wana wa Syria
(Imetafsiriwa)

Watoto watatu walifariki katika kambi za wakimbizi kufuatia dhoruba kali za msimu wa baridi nchini Syria na nchi jirani. Dhoruba hizi zilizidisha hali ya maisha ya wale waliokimbia makaazi yao nchini Syria na wale wanaoishi katika kambi za wakimbizi nchini Lebanon, Jordan na Uturuki kuwa mbaya zaidi.

Imetimia miaka 12 tangu kuzuka kwa mapinduzi nchini Syria, na watoto wasio na hatia, wanawake na wazee bado wanalipa gharama ya vita vya kizembe, kwa ushiriki wa nchi ghushi juu ya ardhi ya Waislamu na zile zinazoichukia Dini ya Uislamu na hukmu zake. Ndege, vifaru na kila aina ya silaha zilizopigwa marufuku zilitumiwa, pamoja na mazoea ya kiholela ya utawala wa Baathi na wanamgambo wake, ikiwa ni pamoja na kukamatwa, ukimbizi na uhamiaji wa kulazimishwa. Vita hivi vimeua zaidi ya mashahidi elfu 350 na kulazimisha mamilioni (karibu nusu ya watu) kuhamishwa kutoka kwa miji na vijiji vyao. Idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Syria, kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kushughulikia Wakimbizi, imefikia zaidi ya milioni 6.7, na idadi ya wakimbizi katika nchi jirani, kama vile Jordan, Lebanon na Uturuki, ni karibu wakimbizi milioni 6.8.

Miaka 12 tangu kuzuka kwa mapinduzi nchini Syria na taarifa zetu kwa vyombo vya habari zinaendelea, sio kuwasilisha idadi ya majeruhi ambayo inazidi kuongezeka, wala kuelezea mateso na kuelezea hali za watu ili kumwaga machozi juu yao. Hali yao ya kuhuzunisha sio siri tena kwa mtu yeyote. Lakini kila wakati, tunajaribu kuwahamasisha wanaume waaminifu kukataa njama zote za kigeni zinazoharibu usalama wa nchi. Vile vile tunasihi mara kwa mara majeshi ya Kiislamu yaondoe ukandamizaji, fedheha na dhulma kutoka kwa watu wetu wa Syria, pamoja na wito wetu wa kuendelea kufanya kazi pamoja nasi ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo ndani yake mna fahari na usalama wetu.

Enyi Wana Mapinduzi Wenye Ufahamu: Je! Haistahiki, baada ya miaka yote hii mirefu, kwamba mavuno ya mihanga yote hii iwe ni kutimia kwa kauli mbiu yenu mliyoipaza: “Ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” na lengo lenu ambalo mlilitangaza kutoka mwanzo, ambalo ni kuupindua utawala wa vibaraka wa Baathi katika sura na nembo zake zote?!

Enyi Waislamu Wenye Ikhlasi: Je, si wajibu juu yenu baada ya kurudia wito wetu kwenu, mfanye bidii pamoja na Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili kumuonyesha Mwenyezi Mungu (swt) wema mkubwa kutoka kwenu kwa kutimiza ahadi yake (swt) na kutimiza bishara njema ya Mtume wake (saw)?

Hakika Khilafah, ndiyo ambayo kwayo tutaibua kumbukumbu ya kuvunjwa kwake katika siku zijazo, ambayo tunaihitaji mno, tunapoihesabu miili ya watoto wetu wasio na hatia, na kusikia vilio vya wafiwa na wajane, na tunaona machozi ya watu wanaodhulumiwa. Je, wakati haujawadia wa kuondoa dhulma kutoka kwa watu wa Syria, Palestina inayokaliwa kwa mabavu, Iraq, Libya, Sudan, Afghanistan na wengine wengi ambao wanateseka kwa kutokuwepo kwa dola ya Kiislamu na kutokana na utawala wa mabepari, wenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu?!

Kamwe hatutachoka, hatutapumzika na tutapaza sauti zetu zaidi na zaidi kila wakati, kwa matumaini kwamba zitapokewa na masikio makini na akili zinazofahamu kurudisha fahari yetu na chanzo cha utukufu wetu; Khilafah kwa njia ya Utume.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa” [Al-Anfal: 24]

Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu