Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  27 Shawwal 1443 Na: 1443 H / 036
M.  Ijumaa, 27 Mei 2022

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kambi ya Rukban, Khiyana na Kurudi kwa Waliohamishwa katika Enzi ya Iliyopita
(Imetafsiriwa)

Shirika la Kuchunguza Haki za Binadamu la Syria liliripoti kwamba familia 4 ziliondoka kwenye kambi ya al-Rukban, iliyoko kwenye mpaka wa mashariki wa Syria na Jordan na Iraq, na limenakili kuondoka kwa familia 18 na vijana 19 katika makundi sita hadi maeneo yanayodhibitiwa na serikali, huku kukiwa na ripoti kwamba makumi ya familia zinajiandaa kuondoka kambi ya Al-Rukban wakisubiri idhini ya usalama ya kundi la "Maghawer Al-Thawrah".

Haya yanajiri baada ya utawala wa Syria kuimarisha mzingiro wa kambi ya al-Rukban kwenye mpaka wa Iraq na Jordan, ambapo uliendelea kwa wiki ya pili mfululizo kuzingira kambi hiyo, kwa mujibu wa Shirika la Kuchunguza Haki za Kibinadamu la Syria, ukizuia kuingia kwa mahitaji msingi na kuwasili kwa magari ya chakula na dawa kambini humo, hali iliyosababisha upungufu wa vyakula kutoka vituo vya mauzo na bei yake kubwa, pamoja na kukaribia kukatika kabisa kwa dawa na mafuta.

Kambi ya Al-Rukban inawahifadhi Wasyria zaidi ya 10,000 waliokimbia makaazi yao, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, katika hali mbaya ya maisha. Wakaazi wa kambi hiyo waliripoti kuwa vikosi vya serikali na Urusi viliweka vituo vya ukaguzi ili kuzuia kuwasili kwa wafanyabiashara wanaotoka katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali, kuisambazia kambi hiyo chakula, dawa na maziwa kwa watoto. Shirika la Anatolia lilisema matanuri ndani ya kambi hiyo yalilazimika kutumia wishwa ambao hutumiwa kama lishe ya wanyama ili kukidhi mahitaji ya mkate wa wakaazi wa kambi hiyo.

Utawala wa Syria umeshindwa kuifunga kambi hiyo na kuwaregesha tena waliofurushwa katika udhalimu wake. Mzingiro huu wa sasa sio wa kwanza. Imeizingira mara nyingi na kuungwa mkono na utawala wa Jordan, ambao ulifunga mipaka yake mbele ya raia wasio na ulinzi na kuwazuia kuingia katika ardhi yake, haswa baada ya operesheni ya ulipuaji wa mabomu katika moja ya vituo vya ukaguzi katika mpaka wa Jordan na Syria mwaka wa 2016. Mapema mwezi Juni 2019, Jordan ilidai kuregeshwa kwa wakimbizi kutoka kwa ukandamizaji wa utawala hadi udhibiti wa utawala huo! Waziri wa mambo ya nje wa Jordan Ayman Safadi alizingatia kuwa suluhisho la tatizo la Wasyria waliokimbia makaazi yao katika kambi ya Rukban ni kurudi kwa wakaazi wake katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa utawala huo wa kihalifu, ambao waliukimbia kutokana na dhulma na ukandamizaji wake.

Wakati huo huo Uturuki pia inazungumzia haja ya wakimbizi kuregea tena Syria baada ya kubeba mzigo wa matatizo ya kiuchumi na migogoro inayoikabili nchi hiyo, licha ya hakikisho na ahadi zote za awali za kuwalinda. Hii ni sambamba na kampeni za uchochezi na ubaguzi wa rangi dhidi ya wakimbizi wa Syria walioko Ulaya kama nchini Denmark na Ujerumani, ambazo zilifikia hitaji la kuhamishwa kwa nguvu hadi nchi kwao.

Yote haya yanalenga kuwahamisha waliohama makaazi yao na kuwaregesha wahamiaji kwenye chimbuko la dhalimu kwa mara nyingine tena, ili kuyatokomeza mapinduzi yaliyobarikiwa ya Ash-Sham, kama vile Marekani na ala zake zilivyotaka kutoka kwa nchi na mawakala tangu kuanza kwa mapinduzi hayo, kwa kutumia aina mbaya zaidi za maovu na udanganyifu, kuhamasisha zana na uwezo wake wote, kuwanyenyekesha watu waheshimiwa wa Ash-Sham kwa matakwa ya kiongozi wa ukafiri huko Amerika, kupitia suluhisho la kisiasa linalohitimisha mapinduzi na kuwarudisha watu wake kifuani mwa utawala, na kuifanya mihanga mikubwa iliyotolewa na watu wa Ash-Sham kuwa bure, na kisha kurudisha uhusiano rasmi wa kimataifa kana kwamba hakuna kilichowahi kutokea!

Sisi, kwa upande wetu, tunatoa wito kwa watu wetu wa Ash-Sham kuwa na uthabiti licha ya matatizo yote, na wadumu katika misingi yao ambayo kwayo mapinduzi haya yenye baraka yaliasisiwa, moja ya misingi yake ikiwa ni kupinduliwa kwa utawala na nguzo zake zote na nembo, na kukataa kila aina ya majadiliano. Hii ikiwa ni pamoja na kujitenga na tawala na nchi zote zilizokula njama dhidi ya watu wa Ash-Sham na mapinduzi yao, kama vile serikali ya Uturuki na serikali za Ghuba.

Mwisho na la muhimu zaidi, tunawalingania wafanye kazi ya kusimamisha mfumo utakaoeneza uadilifu miongoni mwa watu wote na kufikia utu na uchungaji kwa namna zake zote. Ni mfumo mtukufu wa Uislamu, Khilafah kwa njia ya Utume, ili kupata izza ya duniani na Akhera.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu