Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  28 Muharram 1445 Na: 1445 H / 002
M.  Jumanne, 15 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kukabiliana na Uhamiaji usio wa kawaida nchini Tunisia na Hatua Madhubuti kwa Badali ya Msaada wa Ulaya!
(Imetafsiriwa)

Mnamo mwaka 2023, kama ilivyoripotiwa kwenye wavuti ftdes.net mnamo Julai 31, 2023, takwimu zifuatazo zilirekodiwa:

- Idadi ya majeruhi ya uhamiaji usio wa kawaida kwenye mipaka ya Tunisia ilifikia waathiriwa na watu waliopotea 903.

- Idadi ya majaribio ya wahamiaji waliozuiliwa kuvuka pwani za Tunisia (raia wa Tunisia pamoja na wasiokuwa raia wa Tunisia): wahamiaji 35,143.

- Idadi ya watoto wa Tunisia ambao walifika kwenye pwani za Italia: watoto 1,526.

- Idadi ya wanawake wa Tunisia ambao walifika kwenye pwani za Italia: wahamiaji 379.

Jukwaa la Tunisia la Haki za Kiuchumi na Kijamii zilitoa data katika ripoti moja, ikionyesha kuwa takwimu hizi sio za mwisho na sahihi. Kuna nambari "zisizoonekana" zinazowakilisha wahamiaji ambao hufika Ulaya kupitia njia mbali mbali bila kupita mamlaka za eneo au miundo ya kimataifa, na nambari hizi hazionekani katika takwimu zozote. Nambari hizi ambazo hazionekani ni muhimu na zinatofautiana kulingana na mbinu za mitandao ya ulanguzi wa wahamiaji. Pia ni pamoja na matukio ya kuondoka kutoka kwa mpwani za Tunisia ambazo inaweza kukwepa ufuatiliaji wa usalama au zinazuiliwa kuvukwa bila kuripotiwa au kutangazwa.

Siku chache zilizopita, janga lilitokea upya huku wahamiaji 41 wakipoteza maisha yao katika tukio la kuzama pwani ya kisiwa cha Italia cha Lampedusa, kulingana na shirika la habari la Italia (ANSA), likinukuu ushuhuda wa waathirika. Shirika hilo lilibaini kuwa watu wanne ambao walinusurika tukio hilo waliwaambia waokoaji kwamba walikuwa ndani ya mashua ambayo iliondoka katika mji wa SFAX nchini Tunisia na kuzama njiani kuelekea mwambao wa Italia. Wahamiaji hao hutoka kwa mataifa mbali mbali. Jiji la SFAX limekuwa eneo kubwa la usafirishaji kwa wahamiaji wasio wa kawaida kujaribu kuifikia Italia, kutokana na ukaribu wake na Lampusa ambapo tukio la kuzama la hivi karibuni lilitokea. Mamia ya wahamiaji wanahatarisha hatima isiyojulikana, na uwezekano wa kuishi na kufikia mwambao wa Italia kwa maisha bora kuliko yale waliyoyaacha katika nchi zao, au kukabiliwa na kifo, kutoweka, na kuathiriwa na wahalifu.

Tunisia imekuwa ndio mafikio kwa wahamiaji wengi wanaokimbia mizozo na migogoro katika nchi zao, labda wakitafuta kimbilio au kama mahali pa uzinduzi wa uhamiaji wao kuelekea Italia (pamoja na Wasyria na Waafrika). Walakini, Tunisia yenyewe haiko katika hali nzuri kuliko nchi zao, kwani raia wake wanavumilia umaskini, ukosefu wa ajira, bei za juu, na kupungua kwa nguvu ya ununuzi - haswa baada ya mapinduzi. Migogoro ambayo imeikabili imeifanya iwe mlengwa wa unyonyaji zaidi chini ya utawala wa viongozi mafisadi ambao wameizamisha ndani ya madeni na utumwa. Hii imesababisha kudhoofika kwa hali ya maisha, kuongezeka kwa bei, kuongezeka kwa ukosefu wa ajira, na umaskini ulioenea kwa sababu ya mfumko wa bei ya fedha na uchakavu wa sarafu. Kwa kweli, viwango vya mfumko vimefikia viwango visivyo kawaida (karibu 8.2%).

Watu hawa mafisadi wametandika zulia jekundu kwa nchi za Magharibi, wakijivunia kwa kiburi na jeuri huku wakidhibiti nchi, kuamuru masharti yao, na kulazimisha vizuizi vyao. Mashirika na vyombo vyao vimetawanyika kila mahali, kunyonya utajiri na rasilimali za nchi, kuweka vikwazo, na kuifunga na deni ambalo serikali inajitahidi kutoa pesa taslim kwalo na kuagiza bidhaa muhimu. Wakati huo huo, watu wake wakibaki na njaa, wakisimama katika foleni kwa ajili ya kofi la sukari, unga, au kiasi kidogo cha mafuta.

Je! Nchi imeingia katika hali gani hii, na ni udhalilifu ilioje watu wake wanaouvumilia!

Idadi kubwa ya vijana nchini Tunisia hawaoni mustakabali kwao binafsi isipokuwa kuhama kwenda Ulaya. Wamepoteza motisha wote katika nchi yao wenyewe, kwani viwango vya mshahara havitoshi hata kukidhi mahitaji yao ya msingi.

Vijana wetu wanatapatapa, huku milango yote ikionekana kana kwamba imefungwa kwao. Hakuna kazi, hakuna maisha ya staha, na hawawezi hata kumudu mahitaji yao ya msingi. Hakuna ajira, hakuna maisha ya staha, na hawawezi hata kumudu mahitaji yao ya msingi. Je! Wanawezaje kufikiria kujenga nyumba na kusaidia familia?

"Kutapatapa" sio tena tu fahamu ambayo inaathiri vijana, lakini imekuwa, kama wengine wanavyoiita, utamaduni ambao umekamata idadi ya watu wote. Je! Ni familia ngapi zimeabiri mashua za kifo? Je! Ni watoto na wanawake wangapi wamehesabiwa miongoni mwa wafu na waliopotea? Kila mmoja anakimbia kwa ajili ya maisha yao kwa sababu katika nchi yao wenyewe wao ni kama wafu tu. Mahitaji ya maisha yenye staha hayapo, na hadhi ya mwanadamu inapuuzwa.

Pindi mtu anapobeba watoto wake wadogo na kuwatupa ndani ya bahari ya wazi, bila kujua iwapo watafika salama au kuwa chakula cha papa, na pindi mama anapomtuma binti yake mdogo kwa matumaini kwamba atafikia mwambao wa Italia na kupata hifadhi, bila kuzingatia hatari ambazo angeweza kukumbana nazo... hadithi hizi zinakuwa sugu kwa kila kitu mbele ya ruwaza zilizokwamishwa na kupotea kwa tumaini la maisha ya staha.

Enyi watu wa Tunisia:

Hali ni tete na jambo hili ni baya sana! Misiba na kuzama kwa sababu ya uhamiaji usio wa kawaida, ambao almaarufu hujulikana kama "al-Harga," lazima ukomeshwe. Lazima tuwaokoe vijana na binti zetu kutokana na kuwa maiti zinazopigwa na mawimbi kwenye fukwe za kigeni, na kuzikwa kwenye makaburi ya wageni. Suala hili linaenda kina zaidi kuliko kuwa tu ni matukio ya kuzama pekee yaliyoripotiwa na mamlaka za Italia.

- Wakati Italia inapokuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa mnamo Julai 23, 2023, kushughulikia uhamiaji usio wa kawaida, unaosababisha kile kinachoitwa "Mchakato wa Roma" unaolenga kutatua sababu msingi za uhamiaji usio wa kawaida,

- Wakati mchakato huu unajumuisha hatua kadhaa, pamoja na kuzima ulanguzi wa binadamu na kuboresha ushirikiano kati ya nchi za Ulaya na Afrika katika maeneo mbali mbali,

- Wakati wasiwasi mkubwa wa kongamano hilo ni kuiga mfano wa Tunisia, ambapo viongozi wa Ulaya wametia saini makubaliano ya kuahidi nchi msaada unaozidi euro bilioni moja kwa badali ya kuchukua hatua ngumu kushughulikia uhamiaji usio wa kawaida kupitia eneo lake, tunapata maelezo ya ripoti zinazoonyesha kuhusika kwa walinzi wa pwani na mamlaka katika majanga haya na kuzama kwa wahamiaji wasio na hatia.

Sisi, katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunaomboleza sana msiba ambao mamia ya familia wamekabiliwa nao, wakipoteza vijana na binti zao. Tunalaani utumiaji wa jambo hili na mitandao ya wahalifu ambayo inatafuta kujikusanyia pesa nyingi. Wanasaidiwa na watu walio na akhlaki dhaifu ambao wako tayari kuua nafsi zisizokuwa na hatia kwa badali ya pesa chache, cheo, au hadhi.

Tunawasihi watu wetu nchini Tunisia wachunguze sababu halisi za mateso, maumivu, fursa haba zilizoko, na tumaini yaliyopotea. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuibua masuluhisho msingi kwa shida zote za maisha na kufanya kazi kwa pamoja kuyapata.

Na tunawalingania wafanye kazi pamoja nasi kuregesha tena mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24]

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu