Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 4 Jumada II 1439 | Na: 1439/012 |
M. Jumanne, 20 Februari 2018 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
UN – Wanaotarajiwa Kuwa Walinzi Ndio Wauwaji!!
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Uingereza la The Times, lilichapisha ripoti kwa kichwa "Wafanyikazi wa UM 'wanahusika na ubakaji 60000 kwa muda wa muongo mmoja'". Ripoti hii inajiri wakati ambapo kumetukia uenezaji mkubwa wa habari na gazeti hilo kuhusu kufichuka kwa kashfa hii iliyo yashtua mashirika ya "misaada"; ambapo lilichapisha katika ukurasa wake wa mbele ripoti inayofichua kuwa shirika la Oxfam lilikuwa limemteua Roland Van Hauwermeiren kama mkurugenzi wa tawi lake la Haiti, ambaye hatimaye alikuwa katikati ya kashfa ya kuhusika na makahaba wakati wa shughuli za uokozi za shirika hilo kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Haiti, miaka miwili baada ya kutimuliwa kutoka kwa shirika jengine la misaada la Kiingereza kwa madai ya kuwatumia makahaba vile vile!
Huu sio mwanzo kufichuliwa kwa ukiukaji wa wafanyikazi na majeshi ya kuhifadhi amani ya UM. Mwaka jana, 2017, katika ripoti kadhaa, Umoja wa Mataifa ulieleza kuwa umepokea malalamishi 31 dhidi ya wafanyikazi wake kuhusiana na madai ya dhulma za kimapenzi katika kipindi kati ya Julai na Septemba mwaka huo (2017). Mnamo Juni, kitengo cha kuhifadhi amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kiliripotia kupokea ripoti za madai ya dhulma za kimapenzi zilizo tekelezwa na wanachama wa majeshi ya kimataifa ya kuhifadhi amani ya Umoja wa Mataifa yaliyotumia misaada kwa huduma za kimapenzi katika nchi walizohudumu ambazo Umoja wa Mataifa ulistahili kuzisaidia.
Ripoti ya gazeti la The Times, iliyo chapishwa kando ya kesi ya Oxfam, ilimnukuu aliyekuwa mkuu wa wafanyikazi katika kituo cha mawasiliano ya dharura cha Umoja wa Mataifa (UNCC), Andrew MacLeod, aliye watuhumu wafanyikazi wa UM kutekeleza maelfu ya ubakaji kote ulimwenguni. McCloud alitaja kuwa kuna takriban wahalifu wa dhulma za kimapenzi dhidi ya watoto 3,300 wanaofanya kazi katika shirika hili la kimataifa na taasisi zake. Ametegemeza makadirio haya kutokana na kuwa moja kati ya kesi 10 za ubakaji au dhulma za kimapenzi zinazo tekelezwa na wafanyikazi wa kimataifa huripotiwa.
Matokeo yake, ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya kazi za majeshi ya kuhifadhi amani ya shirika hili la kimataifa imetaka kuwa nchi za wanajeshi hao ambao wamethibitishwa kuhusika na dhulma za kimapenzi dhidi ya watoto kuzuiwa kushiriki katika operesheni za kimataifa za kuhifadhi amani.
Kama methali isemavyo, "Mlinzi wake ndiye mwizi wake!" shirika hili linalodai kutetea haki za kibinadamu, wanawake na watoto na kuwalinda kutokana na ghasia, ndilo ambalo idadi kubwa ya wafanyikazi wake wanatekeleza ghasia! Wanaodaiwa kuwa walinzi ndio wauwaji! Huu ni mfano mmoja tu wa shehena ya mifano kinzani ambayo shirika hili la kimataifa inakabiliwa nayo, inayo wakilisha mfumo katili, uliooza wa kirasilimali unaojitoa kama mlinzi wa haki, huku ukweli ukiwa unasimama na mwenye nguvu dhidi ya mnyonge na tajiri dhidi ya masikini, ukitekeleza maagizo na ajenda za dola zenye nguvu kwa gharama ya dola hafifu…
Enyi Waislamu popote mulipo:
Ni nani anayestahili zaidi kuwalinda na kudhamini maslahi na usalama wenu…. ni mashirika dhalimu yenye kupokea mishahara au ni nidhamu adilifu na imara iliyo teremka kutoka kwa Muumba; nidhamu inayo weza kutekelezwa pekee kwa kupitia kuwepo kwa Dola ya Khilafah Rashidah, inayo tawala kwa sheria ya Allah na kutekeleza vipengee vyake? Asema Ta'ala:
(وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ)
“Na ninani dhalimu zaidi kuliko yule anaye kumbusha kwa aya za Mola wake; kisha akazipa mgongo? Hakika Sisi, kwa wahalifu, tutajilipiza.” [As-Sajda: 22]
Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |