Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  18 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 026
M.  Jumamosi, 21 Septemba 2024

Barua ya Wazi
Kwa kina Mama, Wake, Dada na Mabinti wa Watu Wenye Nguvu katika Majeshi ya Waislamu

(Imetafsiriwa)

Letter2 Cover AR.jpg1

Huu ni ujumbe kutoka kwa wanawake wenye shida wa Umma wa Kiislamu, uliotumwa kwenu, kina mama, wake, mabinti, na dada wa maafisa na askari wa majeshi ya Waislamu. Wao ni mwili ndio wa matumaini, baada ya Mwenyezi Mungu, kukomesha mauaji ya kikatili huko Gaza na kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina.

Tunakuhutubieni kwa barua hii ya wazi kwa sababu muna ushawishi na mawasiliano ya moja kwa moja na watoto, waume, na ndugu zenu ambao ni maafisa na askari katika majeshi ya Waislamu. Tunawafikieni tukiwa na matumaini kwamba maneno yetu yatagusa nyoyo na masikio yenu, na kwamba mtayafikisha kwa wapendwa wenu, mkiwashajiisha kuwanusuru kaka na dada zao huko Gaza na Palestina yote.

Huu ni ujumbe ulioelekezwa kwenu, ukitambua dori yenu kama washajiishi kwao kutimiza wajibu wao wa kuwalinda watoto wa Ummah na kuwalinda dhidi ya jambo lolote linalotishia usalama na maisha yao.

Tunakugeukieni ili mufahamu jukumu kubwa alilokukabidhini Mwenyezi Mungu kama mama, wake na dada, kuwashajiisha kuharakisha kuwasaidia wanaodhulumiwa miongoni mwa watoto wa Ummah katika sehemu yoyote ya dunia. Wanusuruni na muwasimame pamoja nao ili waweze kuwa mashujaa, walio tayari kuilinda Dini yao na kuinua Raya (bendera) yake dhidi ya madhalimu na maadui.

Tunawasihi imani yenu, mapenzi yenu kwa Dini yenu, na Ummah wenu, tukiamini kwamba mumeumizwa na hali hii na kwamba nyoyo zenu zinapasuka kwa ajili ya mauaji na mauaji ya halaiki yanayofanywa dhidi ya kaka na dada zenu. Tunalitegemea hili, na tunakuombeni muwasukume watoto wenu, baba zenu na kaka zenu wachukue misimamo yao inayostahiki na watimize faradhi yao ya kutetea ardhi, matukufu na maeneo matakatifu ya Waislamu, na kulinda damu na heshima ya Waislamu.

Hatuna shaka kuwa mumebubujikwa na machozi kwa matukio muliyoshuhudia na vilio vya kuomba msaada kutoka kwa wanawake na mayowe ya watoto muliyoyasikia. Hakika, nyinyi mumeghadhibishwa na dhulma ya umbile la Kiyahudi na washirika wake na washirika kutoka kwa makafiri ambao wana chuki dhidi ya watu wa Gaza na Palestina kwa sababu tu wametangaza imani yao kwa Mwenyezi Mungu. Tunajua kwamba mumekerwa na hali hii, hamjaridhika na yanayowapata dada zenu, na munatamani mungeharakisha kuwasaidia, kuwalinda, na kuwaepusha na madhara ya adui kutoka kwao. Hata hivyo, huenda mukahisi hamuna nguvu, kwa kuwa jambo hilo liko mikononi mwa wale walio na nguvu, watoto wenu, baba, na kaka zenu. Hata hivyo, munaweza kuwanusuru dada zenu kwa kuwasihi watu wenye mamlaka miongoni mwa jamaa zenu watoke kambi zao na kutekeleze dori zao za kweli.

Wapendwa Dada Watukufu,

Tunakuhutubieni kwa ujumbe huu kwa mtazamo wa imani ya Kiislamu ambayo sisi, nyinyi, na jamaa zenu katika majeshi ya Waislamu tunashiriki. Imani hii inawafanya waumini kuwa ndugu na inamlazimu kila Muislamu kumnusuru Muislamu mwenzake. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [Surat At-Tawba:14]

Vipi wale wenye kubeba silaha na waliopewa mafunzo ya matumizi yake wasiitikie wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake? Ni wajibu ambao Mwenyezi Mungu amewakabidhi. Ikiwa si kwa siku kama hizi ambapo watoto, kina baba, waume, na ndugu zenu walijiunga na jeshi na kuchukua silaha, basi walikuwa wakijitayarisha kwa siku gani? Na ikiwa matukio haya na mauaji hayataamsha ndani yao hisia ya heshima na ari, basi ni matukio ya aina gani yatakayoamsha?

Aqidah (itikadi) hii inaamrisha utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kwa waja wake waumini, na inawajibisha kuwaasi makafiri na washirika wao. Tunakusihini kwa jina la Mwenyezi Mungu (swt) mutimize dori zenu, muwashike jamaa zenu katika majeshi, ili wapate kumtii Mwenyezi Mungu, wasimame pamoja na Dini yao na Ummah wao, na wawakemee watawala wasaliti. Ni lazima wakaidi amri ambazo zinawazuia kuwasaidia ndugu zao wanaokandamizwa huko Gaza na kwengineko, amri zinazowataka watumie silaha zao kuua watu wao wenyewe katika maeneo kama vile Sudan, au kupigana katika vita vya wakala kwa ajili ya mabwana wa kikoloni wa watawala wao nje ya nchi zao wenyewe, kama Erdoğan alivyofanya nchini Libya, na kama UAE na Saudi Arabia zilivyofanya nchini Yemen.

Wakumbusheni kwamba hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba, na kwamba watawala hao watawakanusha Siku ya Kiyama na hawataweza kuwanufaisha kwa chochote.

[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّار]

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Surat Al-Baqara:166-7].

Enyi kina Mama, Wake, Mabinti na Dada za Askari na Maafisa katika Majeshi ya Waislamu: Tunajua kwamba kila mmoja wenu ana hofia wapendwa wake, wasipate madhara wala balaa, na mnawatakia kheri tu. Basi washikeni mkono na muwaonye kwamba adhabu ya Mwenyezi Mungu huenda ikawapata, na watakuwa wamefedheheka duniani na Akhera ikiwa wataendelea kuwatelekeza wanawake, watoto, wazee na wanaume mjini Gaza na Ardhi nzima Iliyobarikiwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ، وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ، إِلَّا خَذَلَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ. وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ، وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ، إِلَّا نَصَرَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ»

“Hakuna mtu (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu mwengine mahali ambapo hadhi yake inavurugwa na heshima yake kuvunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu kumtelekeza mahali ambapo angependa msaada wake; na hakuna mtu (Muislamu) atakayemsaidia Muislamu mwengine mahali ambapo hadhi yake inavurugwa na heshima yake kuvunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsaidia mahali ambapo angependa msaada wake.” (Imepokewa na Ahmad na Abu Dauud).

Dada wapendwa,

Washikeni mikono jamaa zenu katika majeshi ili waandike majina yao katika kumbukumbu za heshima duniani na Akhera. Majina yao yaandikwe pamoja na yale ya Sa’d ibn Mu’adh na Usayd ibn Hudayr, ambao walimnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu na daw’ah yake, na hivyo kuchangia kuasisiwa kwa Dola ya Kiislamu.

Hebu na wawe maanwari wa zama hizi, majina yao yaandikwe miongoni mwa safu za viongozi watukufu kama Al-Mu'tasim, Muhammad ibn Qasim na wengineo, walioitikia wito na vilio vya waliodhulumiwa. Hebu majina yao na yaandikwe miongoni mwa wakombozi wa Msikiti wa Al-Aqsa, eneo la Safari ya Usiku wa Mtume na kibla cha kwanza, pamoja na Umar ibn Al-Khattab na Salahuddin. Hebu majina yao na yaandikwe miongoni mwa watakaotimiza bishara njema ya Mtume (saw) na ahadi za Mola Mlezi wa walimwengu wote: ahadi ya ukhalifa, tamkini, vita dhidi ya Mayahudi, kuenea Uislamu kila pembe ya dunia, na kufunguliwa kwa Roma, kama vile Konstantinopoli ilivyofunguliwa na Muhammad Mfunguzi kabla yao.

Enyi kina Mama, Wake, Mabinti na Dada wa Askari na Maafisa katika Majeshi ya Waislamu: Ni wajibu juu yenu kuchukua msimamo na vipenzi vyenu, kuwahimiza kuunusuru Uislamu na Waislamu kwa njia inayomridhisha Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Waumini. Hatuna shaka na mbegu ya wema ndani yenu na ndani yao, kwani Ummah wa Uislamu daima una rutuba, na kutoka tumboni mwake wanazaliwa watoto watiifu na wenye ari ambao kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu wataleta kheri kubwa kupitia matendo yao.

Huu ndio ujumbe wetu kwenu. Ewe Mwenyezi Mungu tumefikisha. Ewe Mwenyezi Mungu, shuhudia.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu