Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  13 Rajab 1441 Na: 1441/07
M.  Jumapili, 08 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji ya Waislamu nchini India: Hizb ut Tahrir / Malaysia Imefanya Maandamano katika Ubalozi wa India, Ikiwataka Wanajeshi wa Kiislamu Kusonga na Ummah Kushirikiana na Hizb ut Tahrir Kusimamisha Khilafah

Hizb ut Tahrir / Malaysia ilifanya maandamano ya amani mbele ya Ubalozi wa India, Kuala Lumpur mnamo 06/03/2020, kupinga mauaji ya Waislamu nchini India, haswa mjini New Delhi. Mabaniani walio vuka mipaka, kwa idhini na ushirikiano wa Waziri Mkuu Narendra Modi walianza kuwaua Waislamu, kuchoma misikiti, kuharibu nyumba na mali nyingine baada ya Waislamu kupinga Sheria ya Marekebisho ya Uraia 2019.

Licha ya madai yake na fahari yake ya kuwa demokrasia kubwa zaidi ulimwenguni, India, bila aibu, imepitisha Sheria ya kibaguzi na kufunua nia yake ya kuifanya India iwe Serikali ya Kibaniani bila Muislamu yeyote. Modi anasubutu kufanya uhalifu mbaya kama huu huku bwana wake, Trump, akimpa ruhusa kuua Waislamu kwa kisingizio cha kupambana na ‘Misimamo Mikali ya Kiislamu’.

Mkusanyiko ulianza mara tu baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Jamiul Ihsan ulioko umbali wa mita 250 kutoka Ubalozi huo. Waandamanaji waliandamana kutoka msikitini wakiimba kwa nguvu na kupiga Takbeer njiani. Walipofika, Ustadh Abdul Hakim Othman kama msemaji wa Hizb ut Tahrir / Malaysia aliye ongoza maandamano hayo alinyimwa ruhusa ya kukabidhi ujumbe na akaambiwa tu kuiweka kwenye sanduku la barua nje ya jengo hilo.

Katika hotuba yake ya kusisitiza baadaye, Abdul Hakim alionyesha umati wa watu kwamba kutokubaliwa ujumbe na Balozi au mwakilishi wake hakuashirii chochote ila uwoga na uthibitisho wa hatia ya uhalifu uliotekelezwa na serikali iliyo vuka mipaka ya Kibaniani ya India.

Katika hotuba yake, Abdul Hakim pia alitaka vikosi vya majeshi ya Malaysia na vikosi vyote vya majeshi ya Waislamu kwa jumla, hususan Pakistan and Bangladesh, kutangaza Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuwaokoa Waislamu nchini India na kuwakomboa wao kutokana na ukandamizaji wa serikali iliyo vuka mipaka ya Kibaniani.

Hatimaye, kabla ya kumaliza hotuba yake, Msemaji wa Hizb ut Tahrir / Malaysia aliwataka Waislamu wote kufanya kazi kwa kushirikiana na Hizb ut Tahrir kurudisha tena Khilafah, ikiwa ndio suluhisho pekee la kuwaokoa Waislamu ulimwenguni kote, Mbali na kuwaunganisha chini ya uongozi mmoja kama inavyo lazimishwa na Uislamu. "Hizb ut Tahrir inafanya kazi mchana na usiku kote ulimwenguni ili kurudisha tena maisha ya Kiislamu na kusimamisha tena Khilafah ambayo kurudi kwake kuliahidiwa na Rasulullah (saw)", Abdul Hakim alifunga hotuba yake iliyo jaa hamasa.

Maandamano hayo yalimalizika kwa amani hata ingawa hasira ya waandamanaji kwenye mjumuiko huo ilikuwa dhahiri sana. Hizb ut Tahrir / Malaysia kwa hivyo inawalingania Waislamu wote, haswa India kukataa sio Modi tu, bali pia nidhamu ya kidemokrasia iliyo mruhusu Modi, mchinjaji wa Gujrat kutawala juu ya Waislamu kupitia mikono ya Amerika. Hizb ut Tahrir ingependa kuwakumbusha Waislamu wa India kwamba mara tu baada ya kuanguka kwa Khilafah mnamo 28 Rajab 1342 H nchini Uturuki, wanachuoni na Waislamu nchini India walikuwa miongoni mwa kundi la kwanza lililokuwa linataka

kusimamishwa upya kwa Khilafah. Walijua kabisa kuwa Khilafah ndio Dolan a nidhamu pekee ya Waislamu na Khilafah ndio mlinzi pekee na ngao ya Waislamu wote. Hizb ut Tahrir hivyo basi inaomba kwamba Mwenyezi Mungu (swt) awape nguvu na subira Waislamu wanaoteswa wa India na kwamba Yeye (swt) aziangamize serikali zote za kandamizi na kuzibadilisha kwa Dola ya Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume.

Abdul Hakim Othman
Msemaji wa Hizb ut Tahrir Malaysia

#ReturnTheKhilafah      #YenidenHilafet     #TurudisheniKhilafah       أقيموا_الخلافة#

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu