Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  6 Shawwal 1441 Na: HTM 1441 / 08
M.  Alhamisi, 28 Mei 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jibu kwa Uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir wa Alang Ibn Shukrimun na Harakahdaily.net

Kwa mara ya kwanza baada ya kuwa sehemu ya vyama tawala, tovuti rasmi ya Chama cha Kiislamu cha Malaysia (PAS), harakahdaily.net imechapisha makala ya mwandishi kwa jina la Alang Ibn Shukrimun, ambaye ameisingizia Hizb ut Tahrir. Makala hayo ya tarehe 19/05/2020 yenye kichwa "Al-Kahfi: Kinga dhidi ya Fitina za Dajjal Mwishoni mwa Dunia (59)" [Al-Kahfi: Imuniti Fitnah Dajal Akhir Zaman (59)]" yalianza kwa mwandishi kufichua ajenda ovu ya Mayahudi na Wakristo kuwapotosha Waislamu. Kisha, mwandishi akasema:

“Upotofu mwishoni mwa zama hizi, sio tena katika muundo wa dini mpya, lakini katika muundo wa fikra iliyo chakachuliwa kati ya mirengo miwili iliyo shitadi; ulio huru sana au ulio kaza sana. Kwanza, adui wa Uislamu hukuza, kueneza na kudhamini fikra iliyo jitenga ya Uislamu ambayo ina umbile la misimamo mikali na ghasia. Wale ambao ni wajinga (Jahil) lakini wenye motisha kubwa watashawishiwa na mtazamo wa aina hii. Matokeo yake, wafuasi wa Hizb ut Tahrir na Dola ya Kiislamu (IS) wameibuka kote ulimwenguni.”

Baada ya kuyapata na kuyasoma makala hayo mnamo 22/05/2020, tumetuma ujumbe mfupi kwenye akaunti ya Facebook ya Alang Ibn Shukrimun, tukimtaka afute mara moja aya hiyo iliyoichafua Hizb ut Tahrir, na tuko tayari kumsamehe kama Muislamu mwenzetu. Kwa bahati mbaya, hadi leo, hajafanya hivyo. Kwa hivyo, tunapenda kusema kuwa:

1. Yale aliyo yaandika Alang Ibn Shukrimun ya kuifungamanisha Hizb ut Tahrir na upotofu, ubebaji fikra iliyo jitenga, uliyo chakachuliwa, iliyo pita mipaka na iliyo na misimamo mikali na ghasia iliyo fadhiliwa na maadui wa Uislamu – haya yote ni madai yasio na msingi, na kwa kweli ni kashfa mbaya dhidi ya Hizb ut Tahrir. Tumechagua kutoelezea nukta hadi nukta uzushi na ujinga wa mwandishi kuhusu Hizb ut Tahrir katika toleo hili, lakini inatosha kusema kwamba habari zote kuhusu Hizb ut Tahrir zinaweza kupatikana kwa urahisi kupitia tovuti zetu, na hata viongozi wetu na wanachama wanaweza kupatikana kwa urahisi nchini Malaysia, ili mwandishi aweze kuthibitisha (Tabayyun) na kupata habari za sawa kuhusu sisi.

Pia kuna amali mbali mbali za Hizb ut Tahrir, ambazo zinaweza kuunganishwa na kupatikana kwa urahisi ili mwandishi apate habari ya moja kwa moja. Kwa bahati mbaya, badala ya kuhakikisha, mwandishi alichagua kuikashifu na kuichafua Hizb ut Tahrir kwa uzushi na udanganyifu.

2. Kuwatuhumu wafuasi wa Hizb ut Tahrir kwa kuwa wajinga na kushawishiwa na ajenda ya upotofu inayo tekelezwa na maadui wa Uislamu kupitia fikra iliyo chakachuliwa, iliyo pita mipaka, iliyo na misimamo mikali na ghasia - hizi zote ni kashfa kubwa ambazo ni kinyume na ukweli. Ijapokuwa neno "misimamo mikali" lina maana fiche, lakini mwandishi hapa ameliweka bayana kwa njia mbaya, achilia mbali uwekaji pamoja tuhuma za “misimamo mikali” na tuhuma za vurugu. Hatushangai kabisa ikiwa uzushi na tuhuma zote hizi zimetoka kwa makafiri ambao ni maadui wa Uislamu, iwe ni kutoka Magharibi au Mashariki ya ulimwengu, kwani tumekuwa tukikabiliana kwa muda mrefu na kuendelea kukabiliana nao mpaka sasa. Lakini, inatushangaza wakati uzushi na tuhuma kama hizi zinatoka kwa Waislamu ambao walitoa sauti kama hizo kwa makafiri, sasa wanazitoa kuelekezea Hizb ut Tahrir. Hii ni kwa upande mmoja.

Kwa upande mwengine, ni bahati mbaya sana Alang Ibn Shukrimun anaonekana mjinga wa uhalisia kwamba fikra yenye upotofu wa kikweli iliyo letwa na adui wa Uislamu (Mmagharibi) ni Urasilimali, mfumo ambayo imeibuka kutokana na itikadi (Aqeedah) ya kutenganisha dini na maisha. Ni kutokana na mfumo huu ilio undwa na mwanadamu, ambapo demokrasia ilizaliwa, yenyewe ni nidhamu potofu na  kuibua nidhamu potofu ya utawala, inayo pigiwa debe na Wamagharibi katika nchi zote za Waislamu. Ni harakati ngapi za Kiislamu ambazo zimeangukia katika mtego na njama za Wamagharibi, hivyo kuitabani na kuifanyia kazi demokrasia ambayo ni wazi inapingana na Uislamu. Huu ndio mfumo (Urasilimali) ulio kuja na nidhamu ya kidemokrasia, ambayo imepotosha watu wengi ambao “wanaiamini” (“yu’minuuna” bihi). Hizb ut Tahrir iko dhidi ya mfumo wa Urasilimali na nidhamu yake unaozalishwa wa kidemokrasia, ambayo imekuwa ajenda ya Wamagharibi kupotosha Waislamu tangu iliyoizaa ya kidemokrasia, ambayo imekuwa ndio ajenda ya Kimagharibi ya kuwapotosha Waislamu tangu kuanzishwa kwake. Ni kwa msingi huu ambapo maadui wa Uislamu ni wakali kwa Hizb ut Tahrir kwa kiasi kwamba makafiri wa Magharibi na Mashariki na mawakala wao wa kidikteta miongoni mwa watawala wa Waislamu, wameipiga marufuku Hizb ut Tahrir, kuzuia Da’wah ya Hizb ut Tahrir, kukamata na kuwatia nguvuni wanachama wake, na hata kufikia kiwango cha kuwaua wanachama wake. Ni kinaya, kwa Alang Ibn Shukrimun kuwatuhumu wafuasi wa Hizb ut Tahrir kuwa wameshawishiwa na fikra potofu iliyoletwa na maadui wa Uislamu! Ni nani hasa anayewafuata maadui wa Uislamu – je, ni Hizb ut Tahrir inayo fanya kazi kusimamisha Uislamu kikamilifu, au wale wanaoukumbatia mfumo wa Urasilimali na nidhamu iliyo na Wamagharibi ya kidemokrasia?

3. Kuwaweka wafuasi wa Hizb ut Tahrir katika mstari mmoja na Dola ya Kiisilamu (IS) imeonyesha kwa mara nyengine tena uovu na ujinga wa mwandishi. Anawezaje kutotambua tofauti kati ya Hizb ut Tahrir na IS wakati hata kipofu anajua hilo!? Kama angefuata maendeleo ya Hizb ut Tahrir, bila shaka angejua tofauti kati ya Hizb ut Tahrir na IS ambayo ni kama mbingu na ardhi. Kama ulimwengu wote unavyojua Hizb ut Tahrir ni nani na IS ni nani, na ni zipi tofauti kati ya vyama vyote viwili, kwa hivyo hatuhitaji kuelezea hapa. Inatosha kusema kwamba ikiwa Alang Ibn Shukrimun alikuwa na ikhlasi ya kutosha katika kutafuta ukweli kuhusu Hizb ut Tahrir, angeliupata kwa urahisi.

4. Alang Ibn Shukrimun anapaswa kutenda haki na kuwa mwangalifu katika uandishi wake, haswa wakati anapogusia kuhusu wengine. Alipaswa kupata habari za uhakika mwenyewe kabla ya kuandika. Isipokuwa ikiwa ameilenga Hizb ut Tahrir kimakusudi katika mashambulizi yake ya uzushi, basi yaingia akilini kwake kuandika kwa njia hii. Hata kama hamuonei Mwenyezi Mungu (swt) hata kidogo, angefaa kuwaonea haya watu wakati wa kuandika uzushi dhidi ya chama cha kisiasa cha Kiislamu cha kiulimwengu kinacho julikana kote ulimwenguni, kinyume na yale aliyo yasifia!

Kinachoudhi zaidi ni kwamba makala hayo ya uongo yalichapishwa na harakahdaily.net, ulimi rasmi wa PAS ambayo inadai kuufanyia kazi Uislamu. Kama sauti rasmi ya harakati ya Kiislamu, harakahdaily.net ilipaswa kuwa makini sana katika kuchapisha kila makala, kuhakikisha kwamba yaliyomo kwenye kila uandishi hayawazulii wengine. Tunaiomba PAS daima kujifunga na fahamu ya ubainishaji (Tabayyun) ambayo ilijifunga nayo hapo awali, na kuhakikisha kwanza, kabla ya kuchapisha maandishi maovu ya uzushi kuhusu Hizb ut Tahrir kama yale ambayo Alang Ibn Shukrimun ameyaandika.

Kwa mwandishi: Kwa mara nyingine tena, tunakuomba uondoe mara moja kile ulichoandika kuhusu Hizb ut Tahrir, na hatuna shida kukusamehe kwa kuvuka kwako mpaka, kwani tabia nzuri ya muumini ni kumsamehe ndugu yake. Kwa harakahdaily.net: Tafadhali ondoeni maandishi ya uzushi kutoka kwa wavuti wenu mara moja. Tunajaribu kuwa na dhana njema (husnu zhan) kwenu kwamba mumepuuza maoni ya uongo ya mwandishi. Kwa hivyo, ondoeni sehemu ya uzushi mara tu munapojua au mara tu baada ya kupokea Taarifa hii kwa Vyombo vya Habari. Mutakapoweza nyote wawili kufanya hivyo, basi ni bora kwenu na Mwenyezi Mungu (swt) awasamehe. Lakini, ikiwa mutaendelea kuyawacha, basi tutayaacha mambo yenu kwa Mwenyezi Mungu (swt), na wakati huo huo, tambueni kwamba tunapata kujua sura yenu halisi wakati mumekuwa sehemu ya serikali hii ya kisekula!

Abdul Hakim Othman
Msemaji wa Hizb ut Tahrir Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu