Jibu la Swali: Ruwaza ya Marekani ya Kutatua Kadhia ya Cyprus
- Imepeperushwa katika Maswali ya Kisiasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
“Afisi ya rais wa Uturuki ilitangaza mnamo Jumatatu kwamba Rais wa Jamhuri ya Uturuki ya Cyprus Kaskazini, Tufan Erhürman, atatembelea Ankara Alhamisi ijayo, 13/11/2025... Burhanettin Duran, mkuu wa idara ya mawasiliano ya rais wa Uturuki, alisema kwamba ziara ya Erhürman Ankara inakuja kutokana na mwaliko wa Rais Erdoğan, na Duran aliongeza kwamba ziara hiyo itakuwa kituo cha kwanza cha kigeni cha Erhurman... Na mnamo tarehe 19 Oktoba Bodi Kuu ya Uchaguzi ya Uturuki ya Cyprus ilitangaza ushindi wa kiongozi wa Chama cha Republican cha Kituruki, Tufan Erhürman, katika uchaguzi wa rais.” (Shirika la Anadolu, 10/11/2025). Kwa hivyo ni nini kimesababisha maridhiano haya? Ikifahamika kwamba Erhurman, wakati wa kampeni yake ya uchaguzi, alikuwa akitoa wito wa kuunganisha kisiwa hicho, huku Erdogan akitoa wito wa dola mbili? Na je, Amerika iko nyuma ya maridhiano hayo? Na Mwenyezi Mungu akulipe kheri.



