Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Muharram 1442 Na: 1442 / 02
M.  Alhamisi, 20 Agosti 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wale Wanaolitambua Waziwazi Umbile la Kiyahudi, Mithili ya Imarati, Uturuki na Misri, na Wale Wanaoweka Masharti ili Kulitambua Mithili ya Pakistan, Saudi Arabia na Mamlaka ya Palestina, Wote Wamekusanyika katika Kuifanyia Khiyana Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina

Katika mahojiano ya runinga, yaliyopeperushwa mnamo 18 Agosti 2020, Imran Khan alikataa kulitambua umbile la kihalifu la Kiyahudi, lakini kwa uangalifu akaweka kukataa kwake sharti la kukombolewa Palestina. Vilevile, Saudi Arabia imeifanya "itifaki ya mkataba wa amani wa kimataifa," kuwa sharti la kulitambua rasmi umbile la Kiyahudi. 

Kinyume chake, Imarati bila ya aibu imeanzisha mafungamano ya kidiplomasia yasiyokuwa na masharti yoyote na umbile la Kiyahudi. Lakini, watawala wote wanaolikubali umbile la Kiyahudi, ima kwa masharti au bila ya masharti, wote wamekusanyika katika kuifanyia khiyana ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina, ardhi ambayo Ummah huu mtukufu utapigana kwa ajili yake mpaka mwisho wa pumzi zake.

Zaidi ya hayo, kuangamia kusiko kuwa na budi kwa umbile la Kiyahudi tayari kumedhamiriwa, na kujulishwa kupitia wahyi. Mikataba ya siri na ya dhahiri ya ulinzi wa umbile la Kiyahudi na watawala hawa haitalisaidia umbile hili la Kiyahudi pindi wakati ukifika.

Kuondolewa kikamilifu kwa umbile la Kiyahudi ndio suluhisho pekee linalokubalika kwa Ardhi Iliyo Barikiwa ya Palestina, kwani umbile zima la Kiyahudi ni uvamizi haramu wa ardhi tukufu ya Waislamu. Hivyo basi tunamuuliza Imran Khan, unamaanisha nini hasa kupitia kulikubali umbile la Kiyahudi baada ya ukombozi wa Palestina?

Kiuhalisia, watawala hawa wa Pakistan na Saudi Arabia wanaosaidiwa na Wamagharibi wamejitolea katika suluhisho la "dola mbili", ambalo linamaanisha kurudi katika mipaka ya kabla ya 1967, ambapo umbile la Kiyahudi limechukua asilimia 78 ya ardhi hii tukufu ya Waislamu. Zaidi ya hayo, umbile hili la Kiyahudi linadai makaazi yake ya baada ya 1967, ambapo yanaipunguza ile inayoitwa Dola ya Palestina kuwa gereza la wazi, katika asilimia 12 ya ardhi. Watawala hawa hawawezi kuudanganya Ummah wa Kiislamu kupitia kujificha nyuma ya lugha ya kidiplomasia. Wanyakuzi ambao watawala hawa wanafanya mikataba nao kwa masharti, hawakuridhika na hata Mitume wa Mwenyezi Mungu (as), wakivunja ahadi moja baada moja. Kwa khiyana hii ya kinyama, watawala hawa karibuni watakutana na hatma yao mikononi mwa Ummah, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).   

Enyi Waislamu katika Vikosi vya Majeshi! Macho ya Ummah yameelekezwa katika makao makuu ya majeshi ya Waislamu. Majeshi matukufu ya nchi yoyote Pakistan, Uturuki, Misri au Iran yanaweza kipeke yake kulimaliza umbile haramu la Kiyahudi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Sheikh Taqi ud Din An-Nabahani alilifananisha umbile la Kiyahudi na kivuli cha serikali zilizoko sasa, pindi serikali hizi zitakapo ondoka, kivuli hicho pia kitaondoka. Suluhisho pekee la Palestina ni lile lililotekelezwa na Umar (ra) na Salah ud Din. Hivyo basi, Ummah unasubiri hatua tukufu ya maafisa wa jeshi, watakaowaondoa wanyakuzi hawa wa mamlaka, na kutoa Nusra ili kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Hakika, ni Khilafah ndiyo itakayo timiza bishara njema ya hadith ya Mtume Muhammad (saw), iliyosimuliwa na Abu Huraira (ra):

«لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ فَيَقْتُلُهُمُ الْمُسْلِمُونَ حَتَّى يَخْتَبِئَ الْيَهُودِيُّ مِنْ وَرَاءِ الْحَجَرِ وَالشَّجَرِ فَيَقُولُ الْحَجَرُ أَوِ الشَّجَرُ يَا مُسْلِمُ يَا عَبْدَ اللَّهِ هَذَا يَهُودِيٌّ خَلْفِي فَتَعَالَ فَاقْتُلْهُ،‏ إِلاَّ الْغَرْقَدَ فَإِنَّهُ مِنْ شَجَرِ الْيَهُودِ»

“Hakitasimama Kiyama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi na Waislamu watawauwa mpaka Yahudi atajificha nyuma ya jiwe au mti kisha jiwe hilo au mti huo vitasema: ewe Muislamu ewe mja wa Mwenyezi Mungu huyu hapa Yahudi nyuma yangu; basi njoo umuuwe; isipokuwa mti wa Gharqad kwani hakika huo ni miongoni mwa miti ya Mayahudi.” (Muslim)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu