Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 2 Safar 1442 | Na: 1442/12 |
M. Jumamosi, 19 Septemba 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uidhinishaji wa Sheria ya FATF Iliyoungwa Mkono na Amerika Inathibitisha kuwa Vyama vya Upinzani na Tawala Vimo Mfukoni mwa Amerika
Katika mahojiano ya mnamo 12 Disemba 2012 pamoja na BBC, alipoulizwa kuhusu ni nani atakayeshinda uchaguzi wa Pakistan wa Mei 2013, aliyekuwa Balozi wa Amerika wakati huo Richard Olson alitangaza kwa ujasiri mkubwa, "Farasi wetu ni demokrasia." Jambo hili limethibitishwa kwa mara nyengine tena wakati kikao cha pamoja cha bunge kilipoidhinisha sheria ya FATF inayoungwa mkono na Amerika. Hata ingawa upinzani ulikuwa na idadi ya wengi, thuluthi moja ya wabunge wake walichagua kubakia kimya nyumbani, wakiruhusu upasishwaji bila ya kizuizi. Ilhali,upinzani unasubutu kudai kirongo kuwa uliipinga sheria hiyo ya kibabe, kana kwamba ndio matumaini pekee kwa watu. Kwa miongo mingi, Amerika imesaidia udikteta nchini Pakistan, kwani nyuma vyama vichache vya kisiasa vilibakia tiifu kwa Uingereza chini ya Demokrasia, vikizuia mipango ya Amerika. Lakini, katika miongo ya hivi karibuni, huku Uingereza ikipoteza nguvu yake ya kiulimwengu na ushawishi wa ndani, Amerika ilichukua udhibiti mkuu wa jukwaa la kisiasa la Pakistan, huku serikali na vyama vya kisiasa vikiwa mfukoni mwake. Sasa, Demokrasia pamoja na Udikteta ni pande mbili za sarafu moja ya ukoloni wa Kiamerika, huku uongozi wa kiraia na kijeshi ukiwa ni nyuso tu za Raj (ukoloni) wa Kiamerika. Khilafah pekee ndio itakayo hakikisha kuibuka kwetu kutokana na janga la ukoloni kwani sio Khalifah wa Baraza la Ummah walio na haki ya kutunga sheria kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na mwanadamu, wakati uo huo Khalifah ni lazima atabikishe hukmu zilizovuliwa kutoka katika Quran na Sunnah.
Sheria za FATF zilipitishwa kwa msingi kuwa endapo hatutazipitisha sheria hizi basi India itatuweka katika Orodha Nyeusi ya FATF. Hoja hii ni marudio ya kujisalimisha kwa Musharraf alipodai kuwa endapo hatutageuka juu kuiunga mkono Taliban, kutoa kambi zetu za kijeshi na njia za anga kwa Amerika, basi tutapigwa mabomu hadi turudi katika Zama za Kale. Musharraf alidai kuwa ndio njia ya pekee ya kuilinda Kashmir pamoja na uchumi na usalama wa Pakistan, kuiweka "Pakistan Kwanza." Lakini, kuiingiza Amerika, Pakistan ikawa ni uwanja wa mabomu, ambapo maisha ya watu zaidi ya elfu sabiini yalipotea kupitia idadi kubwa ya milipuko ya kujitolea mhanga na operesheni kadhaa za kijeshi. Uchumi wa Pakistan uliharibiwa kwa upungufu mkubwa wa gesi na umeme, huku ukipoteza hasara kubwa za kifedha zenye kufikia zaidi ya dolari za Amerika bilioni mia mbili. Kadhia ya Kashmir ilizikwa kwa ajili ya sera ya Amerika kwa India. Licha ya hasara zote hizi, Amerika "inaendelea zaidi" kukariri taarifa, huku watawala wa sasa wakijisalimisha kwa miradi mipya ya wakoloni. Uongozi wa kisiasa na wa kijeshi wa Pakistan kwa sasa unajishinikiza ili Amerika ishinde katika meza ya majadiliano kile ilichokipoteza katika uwanja wa vita nchini Afghanistan. Ama FATF, hakuna kikomo kwa matakwa ya njama hii ya wakoloni, kwani hugeuka kila upande ili kuhakikisha matakwa baada ya matakwa. Huku ikiwa iko mbali na kuwa ya kati na kati FATF ni chombo cha wakoloni cha kuimaliza miundomsingi ya jihad inayounga mkono Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, kikimakinisha ukandamizaji wa misikiti na madrassa. Huku, ikijificha nyuma ya FATF, serikali ya Bajwa-Imran imeshughulika na kulinda maslahi ya wakoloni ili kuhakikisha madhara zaidi kwa Waislamu.
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan inasisitiza kwa watu wenye nguvu kwa maneno wazi na yasiyo na utata kwamba chini ya mfumo wa wakoloni wa kimataifa utumwa wetu, hasara zetu na udhalilifu wetu utazidi kuongezeka. Asasi hizi hazikuundwa na dola za wakoloni ili kutatua mizozo ya mataifa mengine. Ziko kwa ajili ya kuwafanya watumwa kithaqafa, kijeshi na kiuchumi. Lakini, nyinyi mko na Itikadi na mfumo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wenu, Mwenyezi Mungu (swt), ulio na uwezo wa kuuvunja mfumo wa kiliberali wa Kimagharibi. Ummah wa Kiislamu ndio mrithi asili na mstahiki wa Eurasia, basi ni lazima muukanyage mfumo huu wa wakoloni chini ya miguu yenu. Si katika fahari ya Dini yenu tukufu na Ummah wake mtukufu kwamba mujisalimishe kwa mfumo huu wa wakoloni wa kimataifa, bali nyanyueni bendera ya Shahada kote ulimwenguni. Jitokezeni sasa mtoe Nusra kwa Hizb ut Tahrir iliyo na uwezo wa kuwaongoza katika ushindi baada ya ushindi, chini ya kivuli cha Khilafah kwa Njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ اِلَّا الضَّلالُ فَاَنّٰی تُصْرَفَوْنَ]
“Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?”[Surah Younus: 32]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |