Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Rabi' II 1442 Na: 1442 / 29
M.  Ijumaa, 20 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mradi wa Khilafah Pekee Ndio Unaoweza Kuiokoa Pakistan kutokana na Ukoloni, Sio Mkataba Potofu wa Demokrasia

(Imetafsiriwa)

Tangu kuwepo sheria mbaya za serikali za Musharraf-Aziz, Kayan-Zardari na Raheel-Nawaz, Amerika ililazimika kulinda nidhamu ya wakoloni nchini Pakistan isianguke. Huku watawala wa Waislamu wakiwa wamesimama wakianikwa waziwazi baada ya Mapinduzi ya Kiarabu, Washington iliweka mtego chini ya bendera ya utawala mseto wa Bajwa-Imran, na kauli mbiu ya "mabadiliko." Huku kile kinachoitwa mabadiliko yakiwa yamefeli, vibaraka wa zamani wa wakoloni sasa wanakusanyika chini ya bendera ya PDM na kauli mbiu ya "Mkataba wa Demokrasia."

Mkataba huu wa Demokrasia ni mkataba usio na meno uliokosa azimio la kukatikiwa la kuhamasisha vikosi vya kijeshi kwa ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa. Badala yake, kwa agizo la Amerika, uongozi wote wa kisiasa umekubali kuipatia Gilgit-Baltistan hadhi ya mkoa, ikitoa Kashmir Iliyokaliwa kwa Dola ya Kibaniani kama bahashishi, na kuifanya Laini ya Udhibiti kuwa mpaka wa kudumu. Ni mkataba haribifu ambao unakubali nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali inayoruhusu wasomi madogo madogo kunyakua rasilimali za Pakistan, huku pesa iliyopatikana kwa bidii ya mtu wa kawaida ikiporwa kwa jina la kodi, na kuhamishiwa kwa hazina ya wakopeshaji wa kindani na wa kimataifa kupitia malipo haramu ya riba. Ni mkataba usio wa haki unaounga mkono mfumo wa kimahakama uliopo, uliotokana na sheria mbovu ya Anglo Saxon badala ya Qur'an na Sunnah iliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, na vile vile kuwa sababu ya mateso ya mamia ya maelfu waliyonaswa katika safari zisizo na mwisho, za bure mahakamani. Ni mkataba dhaifu  ambao hauamuru hata risasi moja kwa ukombozi wa Msikiti wa Al-Aqsa kutoka kwa uvamizi wa Mayahudi, achilia mbali tishio la uhamasishaji wa jeshi kulinda heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mung (saw), kufuata mfano halisi wa Khalifa wa Kiuthmani, Abdul Hameed II. Ni mkataba wa udanganyifu ambao hautoi wito wa kufukuzwa kwa vikosi vyote vya Amerika kutoka Afghanistan, au kuungana kwa Pakistan na Afghanistan kama Dola moja ya Kiislamu. Mkataba wa upotofu unaokubali maadili ya uhuru ya Magharibi ambayo huharibu maisha ya familia na kuharibu kizazi kijacho. Ni mkataba wa kujitiisha ambayo unakubali mfumo wa kiulimwengu uliloundwa na wakoloni wa Wamagharibi, ikifunga minyororo Pakistan kwa utumwa wa Magharibi. Ni mkataba wa hila, unaotoa ahadi ya utiifu kwa katiba ya mkoloni aliyobuniwa 1973, badala ya kudai katiba inayotokana na Quran na Sunnah pekee.

Demokrasia na udikteta ni nidhamu za batili zilizofeki na Umma haupaswi kung'atwa kutoka shimo moja mara mbili. Umma utaamshwa kupitia kile kilichokuwa sahihi mwanzoni, Khilafah Rashida. Kujitolea kwa mradi wa Khilafah, watu wenye nguvu na watoe Nussrah kwa Hizb ut Tahrir, ili Pakistan iwe jukwaa lenye nguvu la kuunganisha Ardhi za Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake ndiye Bwana wa Mambo Yake, kwa hivyo ni nani atakayefuata nyayo za Saad bin Mu’adh (ra), kiongozi aliyebarikiwa wa Ansar, atoe Nussrah kwa ajili ya kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt)? Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[ياَ أيُّهَا الَّذِيۡنَ اٰمَنُوۡا كُوۡنُوۡۤا اَنۡصَارَ اللّٰهِ كَمَا قَالَ عِيۡسَى ابۡنُ مَرۡيَمَ لِلۡحَوارِيّٖنَ مَنۡ اَنۡصَارِىۡۤ اِلَى اللّٰهِ قَالَ الۡحَـوَارِيُّوۡنَ نَحۡنُ اَنۡصَارُ اللّٰهِ]

“Enyi mlio amini! Kuweni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama alivyo sema Isa bin Mariamu kuwaambia wanafunzi wake: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wakasema wanafunzi: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu!” [As-Saff 61:14]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu