Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  18 Rabi' II 1442 Na: 1442 / 31
M.  Alhamisi, 03 Disemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Badala ya Kutoa tu Mkusanyiko wa Ushahidi juu ya Ugaidi wa India, Hamasisha Jeshi letu kwa Ukombozi wa Kashmir

Katika mahojiano moja na Global Village Space lililochapishwa mnamo 3 Disemba 2020, msemaji wa jeshi, DG-ISPR Meja Jenerali Babar Iftikhar, alitangaza kuwa Pakistan imefuchua udhamini wa serikali ya India wa ugaidi katika mkusanyiko mpya wa ushahidi, uliosambazwa kwa "jamii ya kimataifa." Aliongeza zaidi kwamba ikiwa India inalenga CPEC, Pakistan itazuia kila shambulizi, ikitangaza, "tumeweka vitengo viwili kwa ajili ya usalama wa mradi huu na mbali na hivyo tuna takriban vikosi 8-9 vya kawaida pia vinavyolinda ukanda huu."

Kwa kuwa India imeiunganisha kwa nguvu Kashmir Iliyokaliwa kwa mabavu, Waislamu wa Pakistan na Kashmir wamekuwa wakitamani kutangazwa kwa Jihad na vikosi vyetu vya kijeshi kwa ukombozi wa Kashmir iliyokaliwa kwani India ilikiuka laini nyekundu ya mwisho. Lakini, badala yake, uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan umetangaza kuwa hakuna uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi, ikiipa Dola ya Kibaniani nafasi ya kutosha ya kuimarisha kazi yake, bila changamoto. Kwa kuongezea, uongozi wa kisiasa na kijeshi ulitangaza kuwa watatoa hadhi ya mkoa kwa Gilgit-Baltistan, ambayo inahalalisha uunganishaji wa Modi wa mnamo 5 Agosti 2019 wa Kashmir Iliyokaliwa kwa msingi wa ubadilishanaji. Utoaji  mkusanyiko wa ushahidi wa kufichua ukiukaji wa haki za binadamu na ugaidi wa India katika Kashmir iliyokaliwa ni kuficha khiana kubwa ya utawala wa Bajwa-Imran dhidi ya Kashmir, kwa kujifanya kuwa mkweli dhidi ya usongaji mbele wa India kwa eneo hilo.

Inaposemwa kwamba "vita sio chaguo," basi msaada wote wa kisiasa, kidiplomasia na kiakhlaki, ikiwemo mkusanyiko huo wa ushahidi, inakuwa hayana maana. Kuhusu kuwasilisha mkusanyiko huo wa ushahidi kwa "jamii ya kimataifa," haswa ilikuwa ni msaada wa Amerika ambao uliiwezesha India kutangaza kuunganishwa kwa Kashmir iliyokaliwa. Umoja wa Mataifa yenyewe ni chombo cha mataifa ya kikoloni yanayoongozwa na Amerika, yakitumika kama kiunzi ambacho haki na matukufu ya Waislamu huvunjwa. Kuwasilisha mkusanyiko wa ushahidi kwa wale ambao hushambulia Waislamu wenyewe, na kusaidia wengine kufanya hivyo, ni upumbavu. Kuhusu kulinda CPEC ambayo kimsingi ni mradi wa Wachina, serikali inatangaza vitengo na vikosi, lakini haijahamasisha kitengo hata kimoja cha wanajeshi wenye nia na uwezo wa Pakistan kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa kutoka kwa uvamizi wa kikatili na Dola ya Kibaniani.

Enyi Waislamu katika Jeshi la Pakistan! Ili kuficha uhaini wao juu ya Kashmir, utawala wa Bajwa-Imran unatukuza mkusanyiko huu wa ushahidi na mipangilio ya usalama kwa CPEC. Lakini, suala muhimu mbele yenu ni ukombozi wa Kashmir Iliyokaliwa, ambayo kamwe haitakombolewa kwa karatasi na maneno, lakini kwa damu yenu, moto na chuma katika Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Kujisalimisha kwa Washington na kumlegeza msimamo mshirika wake, New Delhi, utawala wa Bajwa-Imran kamwe hautawahamasisheni kama Khilafah kwa Njia ya Utume itakavyo kuhamasisheni, kama jukumu lililowekwa na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) . Hakuna shaka iliyobaki kwamba lazima mutoe Nussrah yenu sasa ili hukmu kwa yale yote yaliyoteremshwa Mwenyezi Mungu (swt) irudi tena namatembezi ya kwenda kwenye ushindi na shahada yaanza upya. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad 47:7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu