Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Muharram 1443 Na: 1443 / 02
M.  Ijumaa, 13 Agosti 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utegemezi wa Watawala wa Pakistan juu ya Dola za Wakoloni, Haswa Amerika, ndicho Kikwazo kwa Utawala wa Uislamu wa Kieneo na Kiulimwenguni.

(Imetafsiriwa)

Wapiganaji elfu chache, wenye silaha duni, wa upinzaji wa Afghanistan sasa wamewekwa nje kidogo ya Kabul, wakiwa tayari kukizika kiburi cha dola ya tatu ya wakoloni katika makaburi ya himaya, chini ya ardhi iliyomwagiliwa na damu safi ya majeshi ya mashahidi, tangu wakati ambapo Uislamu ulilikirimu eneo letu mara ya kwanza. Ni wakati sasa wa kusimamisha Khilafah, kuiunganisha Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati kama dola moja, kabla ya kuunganishwa kwa Ulimwengu mzima wa Kiislamu, kuanzia Morocco iliyo Mashariki hadi Indonesia iliyo Magharibi. Makadirio ya pamoja ya kijeshi ya Magharibi katika Ulimwengu wa Kiislamu yanarudi nyuma kwa udhalilifu, huku udhaifu wa jeshi la Amerika, uliolemazwa na vikosi vioga licha ya silaha za hali ya juu, imekuwa dhahiri kwa ulimwengu mzima, ikiwashajiisha Waislamu kujitokeza katika uwanja wa kiulimwengu kama dola. Lakini, badala ya kutumia fursa hii ya kimkakati ya dhahabu, uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan unasalia kama watumwa vipofu wa Washington, wakifuata kwa bidii mradi wake wa mashariki-magharibi wa "uunganishi wa kieneo," wakitelekeza maslahi muhimu ya kimkakati ya kijografia, kwa matumaini tasa ya mapato duni ya kiuchumi ya kieneo.

Hivyo basi, badala ya kusimamisha Khilafah juu ya nguvu imara ya Pakistan na kutokomeza makadirio mabaya, ya masafa mrefu ya nguvu ya Amerika ndani ya Eurasia, watawala wasio na ruwaza wa Pakistan wanafuata mpango wa wakoloni kwa lengo la mpangilio wa kiuchumi wa kieneo, ambao utatumiwa na mfumo mkuu wa wakoloni wa kiulimwengu, na kuzidisha umaskini zaidi na utovu wa usalama kwa Waislamu. Mnamo Jumatatu tarehe 9 Agosti 2021, Waziri wa Ulinzi wa Amerika, Lloyd Austin, alimpigia simu Jenerali Bajwa kuhusu kuunda "maslahi ya pamoja ya kieneo." Hapo awali, Mshauri Maarufu wa Usalama wa Kitaifa wa Pakistan, aliyefunzwa na Amerika, Moeed Yusuf, aliihimiza Amerika kuchukua uongozi wa kisiasa katika "mchakato wa mazungumzo," unaolenga kuipa Amerika kile ambacho haiwezi kujipatia kwenye uwanja wa vita. Kama mwezeshaji aliyeajiriwa kwa ajili ya matarajio yaliyoangamizwa ya Amerika, Moeed Yusuf hakuweza kujizuia kutokana na kuonyesha kiburi kwamba, licha ya ripoti mbaya za vyombo vya habari," maendeleo endelevu" yanafanywa kwenye mazungumzo, huku akidumisha mawasiliano ya karibu na mshauri na mwongozi wake, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Amerika.

Enyi Watu wa Nguvu nchini Pakistan! Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Watawala wa sasa wamefungwa minyororo kutegemea dola za wakoloni, hawawezi kutembea kwenye njia ya ruwaza huru ya kisiasa iliyojengwa juu ya msingi wa Uislamu. Watawala hawa wasio na maono wanaufunga mustakbali wa Pakistan kwa miradi miwili ya wakoloni, ukanda wa kiuchumi wa kaskazini-kusini wa China na mradi wa Amerika wa India, mradi wa kiuchumi wa mashariki-magharibi. Watawala hawa wanatuuza duni thamani kwani Ummah huu sio dhaifu, umebarikiwa na idadi kubwa ya wanajeshi wenye uwezo na walio tayari, na Ummah sio masikini, kwani sehemu kubwa ya rasilimali za ulimwengu iko chini ya miguu yake. Zaidi ya yote, Ummah una Dini ya Haki, ambayo nguvu yake iliwainua Mabedui wa Kiarabu na makabila ya Kituruki ya kuhamahama kuwa viongozi wa utawala wa kiulimwengu. Miradi ya mustakbali ya Ummah haifai kuamuliwa na maagizo kutoka Washington, London, Paris au Beijing, lakini baada ya kushauriana na Islamabad, Kandahar, Tashkent, Madinah, Jakarta na Rabat. Kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) peke yake kumekizika kiburi cha Amerika nchini Afghanistan na ni wakati sasa wa wale wanaomtegemea Mwenyezi Mungu (swt) kuuzika utawala wa Amerika ulimwenguni. Toeni nguvu zenu kama Nussrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itaunganisha nguvu za kijeshi za Umma na rasilimali za kiuchumi kama dola yenye nguvu zaidi duniani. Toeni Nussrah yenu sasa kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu (swt), ili milango ya ulimwengu ifunguliwe kwa kurudi kwa kutawala wa Uislamu uliosubiriwa kwa muda mrefu, kabla ya kuingia kwenu katika milango ya Pepo, makao ya milele kwa wale watafutao kweli ushindi au kuuawa shahidi. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

]إِن يَنصُرْكُمُ اللّهُ فَلاَ غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللّهِ فَلْيَتَوَكِّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [TMQ Surah Aali-Imran 3:160].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu