Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Jumada II 1443 Na: 1443 / 32
M.  Jumamosi, 08 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kadi ya Kitaifa ya Afya ni Hatua ya kuelekea Ubinafsishaji Kamili wa Sekta ya Afya, ambayo itafanya Huduma ya Afya Kutoweza kuimudu Zaidi, huku Serikali Ikitoa Njia kwa Huduma ya Afya ya Kibinafsi.

 (Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 31 Disemba 2021, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan alizindua Mpango Mpya wa Kadi ya Kitaifa ya Afya ya Pakistan kwa Mkoa wa Punjab. Kadi hii itatumika kwa matibabu katika hospitali za serikali na za kibinafsi. Serikali ya Punjab italipa Rupia bilioni 400 kwa kampuni za bima kwa mradi huu, licha ya kuwa mnamo 2021, jumla ya bajeti ya afya ya Punjab ilikuwa Rupia bilioni 370 pekee. Kadi ya afya ya bima kwa kweli ni hatua nyingine kuelekea ubinafsishaji wa sekta ya afya. Serikali ya Punjab itaweka Rupia bilioni 400 za ushuru wa watu kwenye hazina ya kampuni za bima na hospitali za kibinafsi. Serikali inatoa hisia kuwa bima ya afya ni hatua ya kimapinduzi. Lakini, kwa kweli, serikali inahakikisha hospitali za kibinafsi na kampuni za bima zitapata faida kubwa, huku mzigo wote utawaangukia watu ambao lazima watoe mapato ya ushuru.

Mtindo huu ni wa kawaida katika dola za kirasilimali za Kimagharibi, kama vile Marekani ambapo huduma za afya ziko mikononi mwa sekta ya kibinafsi, muungano wa hospitali za kibinafsi na makampuni ya bima, kuwapora watu kwa mikono miwili. Chini ya mfumo wa bima, kipimo cha ujauzito katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Pennsylvania kinagharimu kati ya dolari 18 hadi 93 kwa kampuni tofauti za bima. Lakini, ikiwa ungefanya kipimo hicho bila ya bima ya afya, ingegharimu dolari 10 pekee. Jambo kama hilo lilifanyika katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, ambapo hospitali za kibinafsi zilitoza Rupia 10,000 hadi 50,000 kwa usiku mmoja kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa wa virusi vya Korona, ambayo ingegharimu si zaidi ya rupia mia chache katika hospitali za serikali. Urasilimali umeikabidhi sekta ya afya kwa sekta ya kibinafsi kwa jina la "uhuru wa kumiliki." Kwa hivyo utoaji wa hospitali, dawa au vituo vyengine vya huduma ya afya umekuwa ni biashara, ambapo lengo kuu ni kuongeza faida, badala ya kuboresha huduma za afya.

Uislamu umeufanya utoaji wa huduma za afya kuwa hitaji la msingi la pamoja la jamii, ambayo dola inawajibika kwayo, na sio kwa sekta ya kibinafsi. Badala ya kumwaga Rupia bilioni 400 kwa kampuni za bima na hospitali za kibinafsi, serikali ya Punjab ilipaswa kutumia pesa hizi kuongeza hospitali za serikali na uwezo wao, ili mwananchi wa kawaida aweze kutibiwa bure katika vitengo vya kutibiwa kwa kurudi nyumbani (OPD) na vya kulazwa kwa matibabu ya ugonjwa wowote. Matokeo ya kadi ya afya ya serikali yatakuwa ni mmomonyoko zaidi au ubinafsishaji wa hospitali za serikali, huku kutoweka kwa huduma yoyote ya matibabu ya bure kukionekana sasa kwa umma, kama ilivyotokea kwa sekta ya elimu. Ni mfumo wa uchumi wa Kiislamu pekee, ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) ndio unaoiwezesha dola kutoa huduma za afya bila malipo kwa watu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «الْإِمَامُ رَاعٍ وَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam (Khalifa) ni mchungaji na ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake.” (Bukhari). InshaAllah, Khilafah itakayokuja hivi punde itasimamisha mfumo wa serikali wa Kiislamu, uliovuliwa kutoka katika Qur'an na Sunnah, ambao kwao raia wa Dola ya Kiislamu watapata huduma bora za afya, bila malipo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu