Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 21 Dhu al-Hijjah 1445 | Na: 1445 / 48 |
M. Alhamisi, 27 Juni 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jitihada Zinazorudiwa rudiwa, za Kutapatapa za Kuinasibisha Hizb ut Tahrir na Uanamgambo, ni Kwa sababu Magharibi Inaogopa Kuporomoka kwa Mfumo Wake Fisadi wa Kilimwengu, katika Ulimwengu wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Bado kwa mara nyengine tena upotoshaji mwengine kuhusu Hizb ut Tahrir umeonekana kwenye magazeti, katika mfululizo wa haraka hadi wa mwisho! Gazeti la ‘The Friday Times’ lilichapisha makala mnamo tarehe 20 Juni 2024, yenye kichwa “Hizb ut Tahrir: Kati ya Ghasia na Ugaidi,” yaliyoandikwa na Tariq Aqil. Ni makala mengine tena katika mfululizo wa makala katika machapisho ya ndani na nje ya nchi, yanayoashiria kwamba Hizb ut Tahrir ina mafungamano na uanamgambo.
Makala haya ni matokeo ya ajenda mbovu za kisiasa za dola za kikoloni na vibaraka wao katika Ulimwengu wa Kiislamu. Kwa hakika, mkoloni wa kafiri na vibaraka wao hawaogopi mafungamano yoyote yanayodhaniwa ya Hizb ut Tahrir na uanamgambo, kwa sababu mashirika yao ya kijasusi yanajua vyema kwamba mafungamano hayo hayapo. Hofu yao hasa ni kwamba ulinganizi wa Hizb ut Tahrir, wa kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha tena Khilafah Rashida, una uungwaji mkono mkubwa ndani ya Umma wa Kiislamu. Hofu yao ni kwamba Umma na majeshi yake watageuza mradi wa kikoloni wa dola za kitaifa, ambao umewagawanya na kuwadhoofisha Waislamu, tangu kuvunjwa kwa Khilafah yao, miaka mia moja iliyopita, mwaka 1924. Majaribio yao ya kuihusisha Hizb na uanamgambo hivyo ni ili kuunda kisingizio cha kukandamiza Hizb ut Tahrir, kuinyima Hizb njia ya kufikia majukwaa ya umma.
Ni dhahiri kwamba mfumo wa Hizb, Uislamu, ni tishio la kuwepo kwa mfumo wa kilimwengu wa Magharibi. Uislamu unakataa ubwana wa akili ya mwanadamu, na haki ya wanadamu kutunga sheria. Uislamu unatangaza ubwana pekee ni wa Mwenyezi Mungu (swt), na utabikishaji hukmu za Shariah. Uislamu unaamuru kuunganisha Ummah kama Umma mmoja, na unakataa mipaka ya kitaifa ambayo iliwekwa na wakoloni makafiri, ili kuwagawanya Waislamu katika zaidi ya dola hamsini. Uislamu unasisitiza kwamba maisha ya Waislamu wote, iwe Pakistan au Palestina, yana thamani sawa. Kwa mujibu wa Uislamu, majeshi ya Waislamu yanalazimika kukusanyika ili kuinusuru Gaza, kukomesha uvamizi wa Wazayuni na kuikomboa Palestina. Uislamu unataka umoja wa Ummah, chini ya mamlaka ya Khalifa mmoja. Uislamu unataka kusimamishwa upya kwa Khilafah Rashida, ambayo itaunganisha rasilimali za Ummah, kufukuza makampuni ya wakoloni ya kimataifa na kuangamiza kambi za kijeshi za dola za Magharibi ndani ya ardhi za Kiislamu. Ni ajenda hii msingi ya Kiislamu ya Hizb ut Tahrir ndiyo inayozilazimisha dola za Magharibi na vibaraka wao kuzusha mafungamano ya uanamgambo na Hizb ut Tahrir.
Hofu ya mabadiliko makubwa ya rai jumla wa Waislamu, kuhusiana na Gaza, imezua udharura wa kutapatapa katika tawala, na wasemaji wao kwenye vyombo vya habari. Kwa mfano, makala yaliyopo yamewekwa pamoja kwa haraka, katika kukimbilia kujiunga katika kibwagizo cha uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir. Matokeo yake ni uandishi mbaya wa habari, kwani hasa ni uchapishaji tena wa makala yaliyochapishwa kwa mara ya kwanza na jarida la Newsline miaka kumi na tatu iliyopita, mnamo Agosti 2011, yenye kichwa “Hizb ut Tahrir nchini Pakistani.” Hata ukaguzi wa ukweli wa kimsingi haupo, wakati makala hayo ya ‘The Friday Times’ yanapohariri upya makala ya asili ya ‘Newsline’ kuhusu Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan. Yanasema “mtu pekee anayetambulika sana wa HUT nchini Pakistani amekuwa ni Naveed Butt... Anaonekana mara nyingi akilingania usimamishwa wa Sharia ya Kiislamu.” Naveed hakika alionekana mara kwa mara, mwaka wa 2011. Hata hivyo, Naveed alitekwa nyara na mashirika ya kijasusi mnamo tarehe 11 Mei 2012, na hivyo haonekani kabisa sasa, achilia mbali “mara nyingi.”
Ama kuhusu ulinganizi wa Hizb ut Tahrir kwa majeshi ya Waislamu kuleta mabadiliko, makala ya ‘The Friday Times’ yanaibua jambo hili kana kwamba ni sababu ya kuhofisha. Kwa nini? Nchini Pakistan, inajulikana kuwa vikosi vya jeshi ndio nguvu nyuma ya serikali zote. Je, majeshi yanaruhusiwa tu kuunga mkono utawala huria, wa kisekula, wa Magharibi, na sio utawala wa Kiislamu? Kwa nini, wakati Pakistan ni nchi iliyoundwa kwa jina la Uislamu na raia wake wengi ni Waislamu? Njia ya Utume inathibitisha kwa uwazi kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipata msaada wa kimada (Nussrah) kutoka kwa wapiganaji wa Answaar, katika Ahadi ya Pili ya Aqabah. Ni Ahadi hii ya Nusrah ndiyo iliyouwezesha Uislamu kufikia hukmu na utawala, na kuigeuza Yathrib iliyogawanyika na yenye matatizo, kuwa Al-Madinah Al-Munawarrah adhimu, inayong’aa.
Tunatoa wito kwa Waislamu wa Pakistan, wakiwemo wanahabari wao wenye mawazo adilifu na waandishi wa makala, kusimama kwa ajili ya haki. Tunawalingania kukataa uzushi dhidi ya Hizb ut Tahrir. Vita kati ya haki na batili havipshindiki kwa uzushi, nguvu na kulazimishwa, bali kwa nguvu ya ushahidi na hoja. Kwa kumalizia, kwa kuwa sasa tumewasiliana nanyi, baada ya kushindwa kuwasiliana nasi, tunaomba muchapishe taarifa yetu kwa vyombo vya habari ndani ya machapisho yenu, kwa ukamilifu. Tunakuhimizeni mufanye hivyo, ili wasomaji wenu waweze kufanya chaguo sahihi kuhusu Hizb ut Tahrir, kutofautisha haki na batili. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَقُلْ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَزَهَقَ ٱلْبَٰطِلُ ۚ إِنَّ ٱلْبَٰطِلَ كَانَ زَهُوقًا]
“Na sema: Haki imefika, na batili imetoweka. Hakika batili lazima utoweke.” [Surah Al-Israa 17:81].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |