Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  12 Ramadan 1441 Na: 1441 / 57
M.  Jumapili, 03 Mei 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Naveed Butt, Mbebaji Ulinganizi wa Khilafah, Nembo ya Upinzani dhidi ya Raj wa Kiamerika (Ukoloni), Amekuwa Kizuizini katika Korokoro za Siri za Ukandamizaji za Vyombo vya Usalama Tangu Miaka Minane Iliyopita!

Mnamo 11 Mei, itakuwa ni miaka minane tangu Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan kutekwa nyara na kuzuiliwa katika kifungo kisicho halali katika Uislamu, ndani ya korokoro za siri za ukandamizaji za vyombo vya usalama. Ilhali, serikali ya Bajwa-Imran ilimuacha huru rubani wa Kihindi (Abhinandan) ambaye alikiuka mpaka wa udhibiti huku akijaribu kuishambulia Pakistan, baada ya kupita siku moja pekee. Vilevile serikali hii ilifanya maandalizi ya mkutano maalum wa kidiplomasia na jasusi gaidi wa Kihindi (Kulbhushan Jadhav), pamoja na mkewe. Pamoja na hilo, serikali hii ingali inamnyima Naveed Butt mawasiliano ya aina yoyote na familia yake. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ﴿

"Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao." [Al-Fath:29]. Basi ni jinsi gani hii ndio hali ya watawala vibaraka wa Amerika?! Hakika wao ni wapole mno kwa makafiri maadui na wanabadilishana hisia za mapenzi na huruma na upole, huku wakiamiliana pamoja na Waislamu kwa mkono wa chuma, hata pia wakiwatumilia lugha ya moto na mabomu, hii ni licha ya maneno Yake (swt) katika Hadith al-Qudsi ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ قَالَ: مَنْ عَادَى لِي وَلِياً فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ»  

"Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Yeyote anaye onyesha uadui kwa kipenzi (wali) changu, basi nimetangaza vita dhidi yake" (Bukhari)

 Naveed Butt mwenye umri wa miaka hamsini na moja, baba wa watoto wanne, ni mwana mtiifu na msifika wa Ummah wa Kiislamu. Yeye ni mwanasiasa wa kimfumo wa tabaka ambalo kwa urahisi anaweza kutimiza jukumu la utawala katika wadhifa wowote, baada ya kusimama tena Khilafah. Anatoka katika kabila tukufu la Kashmir linaloishi jijini Islamabad. Alipata usajili katika Chuo Kikuu maarufu cha Uhandisi na Teknolojia (UET) cha Lahore. Kwa werevu wake alipewa uhamisho hadi Chuo Kikuu cha Illinois nchini Amerika, ambako alikamilisha kufuzu kwake. Alikuwa anafanya kazi katika sekta ya kibinafsi nchini Amerika, alipo amua kurudi Pakistan ili awe sehemu ya mvutano wa kiulimwengu wa kusimamisha tena Khilafah katika Ardhi za Waislamu, akikhiari kuacha nyuma maisha ya kifahari kukabiliana na ghadhabu za watawala madhalimu. Alifichua pasi na kuchoka khiyana ya watawala dhidi ya Uislamu na Waislamu na utumwa wao kwa Amerika, kupitia kuandika mamia ya taarifa kwa vyombo vya habari, akiandika makala nyingi, akihutubia mikutano ya waandishi habari, warsha na makongamano mingi, na kukutana na maelfu ya watu wenye ushawishi, katika muda wote huu wa mvutano wake. Alisafiri kote nchini Pakistan ili kuwaelimisha watu kuhusu ufaradhi wa kusimamisha tena Khilafah na maelezo ya muundo wake. Wakati wa mvutano wake wa kisiasa na kifikra, alivumilia kukamatwa na kufungwa mara kwa mara na alijulikana kwa upingaji na ujasiri wake.

Na izingatiwe kwamba mnamo Februari 2018, kiongozi wa tume ya watu waliotoweka, Hakimu Javed Iqbal, alitoa amri ya kutolewa kwa Naveed Butt, akithibitisha kuzuiliwa kwa Naveed Butt na vyombo vya siri vya usalama. Naveed Butt alitekwa nyara katika wakati ambapo alikuwa anaongoza kampeni ya Hizb ut Tahrir katika kuwahesabu vikali watawala. Kampeni hii ilizinduliwa dhidi ya watawala hawa kwa kumwachilia huru jasusi wa Kiamerika na muuwaji, Raymond Davis, pamoja na kushindwa kwao kuzuia shambulizi la Abbottabad, ambayo yalifichua kikamilifu utumwa wao kwa Amerika kwa kila mtu isipokuwa wale wanaojitia upofu kwa sababu za kidunia. Ni wakati sasa kwa watawala kutubia uhalifu wao, kwa kumwacha huru mara moja Naveed Butt. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[إِنَّ الَّذِينَ فَتَنُوا الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ الْحَرِيقِ]

“Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.” [Al-Buruj 85:10]. Kwa hakika ni dhahiri kuwa serikali ya Bajwa-Imran ambayo licha ya kudumu unyanyasaji wake, Hizb ut Tahrir kamwe haijaachana na mvutano wake wala kupunguza kasi katika mvutano wake. Badala yake, ushawishi wa Hizb ut Tahrir kwa jumla umeongezeka katika Waislamu na haswa katika majeshi. Hakika, Waislamu huwaona wale wanaopata matatizo katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) kuwa ndio wenye ikhlasi na kustahiki uongozi. Katika mwezi huu ulio barikiwa wa Ramadhan, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kuwa, kama vile Nabii Yusuf (as), Yeye (swt) amruzuku Naveed Butt aondoke kutoka katika korokoro za watawala madhalimu na kumkirimu kwa utawala unao hukumu kwa yale yote yaliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Hakika, siku hiyo itakuwa ni siku kali mno kwa madhalimu, huku kwa yakini adhabu yao Akhera ikiwa ndio kali zaidi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Wilayah Pakistan

#FreeNaveedButt

#MwacheniHuruNaveedButt

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu