Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 15 Dhu al-Qi'dah 1441 | Na: 1441 / 76 |
M. Jumatatu, 06 Julai 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Unyanyasaji wa Wanafunzi wa Pakistan Utamalizika chini ya Mahakama na Nidhamu ya Kijamii za Khilafah
Mnamo 30 Juni 2020, shule moja ya kibinafsi jijini Lahore iliwafuta kazi waajiriwa waliotuhumiwa kwa kuwanyanyasa kimapenzi wanafunzi wengi wa kike. Sasa kadhia hii imepanuka kutoka unyanyasaji wa kimapenzi pekee, hadi unyanyasaji wa wanafunzi kijumla. Hakika, ingawa idadi kubwa ya walimu ni watu wenye shakhsiya murua, muundo wa elimu uliopo nchini Pakistan unawaruhusu baadhi ya watu kujihusisha katika suluki isiyo sawa, na fisidifu pamoja na wanafunzi wao. Kwa kukosekana nidhamu imara za kuhudumia malalamishi na njama za idara katika kulinda hadhi, wanyonge na walio hatarini wanaanikwa peupe hatarini. Nje ya shule, idara legevu ya mahakama huhakikisha kwamba waathiriwa wanateseka kwa muda mrefu kutokana na matatizo ya kifedha na kiakili, huku usikizwaji wa kesi ukiendelea kwa miaka kadhaa. Hivyo, ili kuepuka ufisadi ndani ya taasisi za kielimu na matatizo ya mahakama, waathiriwa wanaanguka kimya kimya na ukandamizaji unaendelea.
Enyi Waislamu wa Pakistan!
Uislamu hauadhibu tu uhalifu wa unyanyasaji pekee; unapunguza uwezekano wa kutokea kwa huo unyanyasaji wenyewe. Ushajiishaji wa Uislamu wa haya (حياء), pamoja na sheria za kuzuia hali ambazo unyanyasaji hutokea, zinatakikana katika wakati ambapo unyanyasaji wa kimapenzi ni tatizo la kiulimwengu. Ndani ya Khilafah, mchanganyiko huru baina ya wanaume na wanawake na mijumuiko ya mchanganyiko hayataruhusiwa, kwani kiasili Uislamu umetenganisha safu za wanaume na wanawake. Wanaume na wanawake wanaweza kukusanyika kwa lengo linalo ruhusiwa na Uislamu, lakini kwa kuzingatia utaratibu wa maadili baina ya jinsia, ambao ni rasmi na sio wa kisiri. Uislamu unaharamisha faragha (خلوة Khulwa) ya mwanamume na mwanamke ili kuzuia vitendo vya faragha baina yao. Zaidi ya hayo, mwanamke katika Uislamu hutazamwa kama heshima inayo lazimu kuhifadhiwa, na sio kutumiwa kwa ajili ya starehe za mwanamume.
Kurudi kwa Khilafah pia kutamaanisha kumalizika kwa maadili huru ya kifisadi ya Kimagharibi ambayo yanalazimishwa juu ya mujtamaa wetu, kuhujumu maadili yalio kita mizizi ya kifamilia na kutuanika katika matatizo ya kijamii ambayo sasa yameenea katika mujtamaa wa Kimagharibi. Mtaala wa elimu na sera ya vyombo vya habari ya Khilafah yataukuuza mujtamaa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na kujifunga na Quran na Sunnah kwa vitendo vyote, ikijenga mazingira ya uchaMungu, yanayo kinga dhidi ya maasi.
Baada ya yote haya, endapo unyanyasaji utatokea, unyanyasaji huu utaangukia chini ya sheria za Taazir, ambazo zina jumuisha madhara juu ya heshima na akili. Adhabu ya Taazir hutekelezwa katika visa ambavyo kuna vitendo vinavyo gongana na Haya (حياء) pamoja na matusi, vitisho, utumiaji vibaya na mateso ya kiakili. Zaidi ya hayo, katika upande wa kuhukumu kwa yale yote aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu (swt), idara ya mahakama katika Khilafah ilijulikana vyema kote ulimwenguni kwa uharaka wake wa kutoa haki isiyo kifani.
Ni kwa kurudi Khilafah Rashida pekee kwa Njia ya Utume ndio itakayo hakikisha kuregea kwa heshima ya pamoja katika ya wanaume na wanawake na kushirikiana kwao katika amali njema, ili kujenga mujtamaa imara, uliostawi na ulio na uadilifu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَـئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]
“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” [Surah At-Tawbah 9:71]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |