Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  2 Rabi' I 1444 Na: BN/S 1444 / 03
M.  Jumatano, 28 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sheria ya Mtoto na Kanuni zake za Utendaji ni Utangulizi wa Kusambaratika kwa Familia, na Kisu chenye Sumu Upande wa Watu wa Palestina!
(Imetafsiriwa)

Sawia na jinai zake dhidi ya watu wa Palestina, Mamlaka ya Palestina (PA) imechapisha kanuni za utendaji kwa ajili ya hatua za kulinda na kumpa haki mtoto za mwaka 2022 katika toleo la hivi karibuni la Gazeti la Palestina, Na. 194, sheria ambayo inatoa njia ya kusambaratisha familia na kushambulia mfumo wa kijamii kwa kuharibu malezi ya baba kwa watoto wake na kuwatoa watoto katika familia zao na hukmu za dini yao! Hivyo, PA imekamilisha ukosi wa njama; kwa kuiachilia sehemu kubwa ya Ardhi Iliyobarikiwa, kuyatelekeza mambo matakatifu, kuharibu mitaala ya elimu, kushambulia uchumi wa watu uliolemewa na ushuru, kodi na ushuru wa uzalishaji, na hii hapa inataka kuisambaratisha familia kwa kupitisha sheria hii, kuchapisha kanuni za utendaji wake, na kuitia saini kupitia CEDAW.

Kuchapishwa kwa kanuni za utendaji za Sheria ya Mtoto kunathibitisha kwamba Mamlaka ya Palestina, kupitia sheria hii na kupitia kifurushi chengine cha sheria za wanawake na familia inachokiwasilisha, na vile vile kupitia harakati zake kali za kueneza fahamu ya jinsia na utamaduni. Jinsia imekuwa ni chombo, na sehemu ya mashambulizi makali ya kiulimwengu yanayofanywa dhidi ya Waislamu, wakiwemo watu wa Palestina, kuvunja familia, kuharibu muundo wa jamii na kufuta maadili ya Kiislamu, kama tawala zingine zilizopo katika ardhi za Kiislamu, ambazo sasa zinapitisha mikataba ya kimataifa kama hati ambayo kwayo wanataka kuunda maisha ya Waislamu kwa msingi huo, hata kama mikataba hiyo inajumuisha vifungu hatari sana kwa Dini na Iman, kama ilivyo hali kwa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto ambao kutokana nao sheria hii ilitungwa.

Kanuni za utendaji zilizoidhinishwa na kuchapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali mnamo tarehe 25/9/2022 ni kanuni za utendaji za Mkataba wa Kihalifu wa Haki za Mtoto uliochapishwa kwenye Gazeti Rasmi mnamo tarehe 27/7/2021, na ingawa sheria hii haikuwapa watoto haki zozote zinazodaiwa za malezi, sheria hiyo na sheria nyinginezo zinazo karibiana nayo na zinazohusiana na wanawake na familia, hazikusudii kumlea mtoto au kumtendea haki mwanamke, bali pamoja na kifurushi hicho chote cha sheria zinakusudia kubadilisha maadili yaliyopo sasa katika mujtamaa na kuyabadilisha kwa maadili ya Kimagharibi. Na tukiangalia haki katika mtazamo wa Kimagharibi, kwani sheria hii katika ufafanuzi wake wa mtoto na vile vile katika mtazamo na misingi yake, imeegemezwa juu ya yale yaliyoidhinishwa na makubaliano ya kimataifa, ukiwemo Mkataba wa Haki za Mtoto, ambao kwayo Mamlaka ya Palestina ilijiunga mwaka 2014. Makubaliano haya yanaegemezwa juu ya mtazamo na fahamu za Kimagharibi tu za haki na uhuru, na kusababisha kusambaratika kwa familia na kuelekekea kusikoepukika kwenye matukio yanayoonekana ambayo kwayo mujtamaa za Kimagharibi zimeharibika, ikiwemo muozo na ufisadi, maovu na upotovu, uasi na mfarakano. Bila shaka, mtazamo huu wa Kimagharibi kuhusu “uhuru” wake unaipeleka jamii kwenye njia ya upotovu na njia za ufisadi na uovu, na kukengeuka kwa ghariza na dhambi la upotovu hadi baadhi ya makundi, na huko Magharibi kwenyewe, yakaanza kuhisi hatari inayotishia mujtamaa zao.

Maelezo bora zaidi ya yale ambayo ruwaza ya Magharibi inayakusudia, ambayo yalikuuzwa kupitia taasisi za kimataifa, kupitia mikataba ya kimataifa iliyotajwa hapo juu, ambayo ilitiwa saini na mamlaka fisadi na tawala za aibu za Kiarabu, ni kile Rais Biden wa Marekani alichosema katika hotuba yake katika Umoja wa Mataifa siku chache zilizopita: “Mustakabali utapatikana kwa zile nchi ambazo zinafungua uwezo kamili wa idadi ya watu wao, ambapo wanawake na wasichana wanaweza kutekeleza haki sawa, ikiwemo haki msingi za uzazi, na kuchangia kikamilifu katika kujenga uchumi imara na mujtamaa imara zaidi; ambapo dini makabila ya walio wachache wanaweza kuishi maisha yao bila kubughudhiwa na kuchangia katika muundo wa jamii zao; ambapo wanajumuiya ya LGBTQ+ wataishi na kuwa huru kupenda bila ya kulengwa kwa vurugu; ambapo wananchi wanaweza kuwahoji na kuwakosoa viongozi wao bila kuogopa kuadhibiwa.”

 Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa:

Jambo hilo ni hatari sana, na endapo mtanyamaza kimya kuhusu uhalifu unaofanywa na Mamlaka ya Palestina dhidi yenu, watoto wenu, na Dini yenu, hakika mutapoteza watoto wenu, kama inavyotokea kwa watoto wa Kiislamu nchini Sweden, na mutapoteza uwezo wa kuwalea kwenye malezi na elimu sahihi ya Kiislamu yenye kuhifadhi Dini na maadili, na katika uharibifu huo na upotevu wa maadili. PA, na nyuma yake zile zinazoitwa nchi wafadhili, wanatoa njia kwa umbile la Kiyahudi kutekeleza udhibiti wake juu ya ardhi, heshima na matukufu, kuanzisha makaazi yake, na kuitenga al-Aqswa katika juhudi za kuigawanya na hata kuivunja na kujenga hekalu lake linalodaiwa mahali pake.

Ni juu yenu kuchukua msimamo unaomridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw) basi wahamini watoto wenu na Dini yenu, na simameni kama bwawa lisilopenyeka mbele ya madhalimu na vibaraka wa wakoloni, na mtangaze kwa sauti kubwa kwamba watoto wetu hawauzwi, na kwamba watoto wetu wa kiume ni wanajeshi wa Uislamu, kiigizo chao ni Muhammad (saw) sio Biden, na ni vizazi vya Abu Bakr na Omar na sio wajukuu wa Karl Marx au Adam Smith. Mkifanya hivyo, mtamridhisha Mola wenu Mlezi, na kuzihifadhi familia zenu, na kubakia kuwa mwiba kwenye koo za wavamizi na wakoloni.

[وَاتَّقُواْ فِتْنَةً لاَّ تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمْ خَاصَّةً]

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu.” [Al-Anfal: 25].

Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.” [At-Tahrim: 6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu