Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  24 Safar 1444 Na: BN/S 1444 / 02
M.  Jumanne, 20 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mamlaka ya Palestina Inaendelea kutekeleza Dori ya Uvamizi katika Umwagaji damu ya Wapalestina
(Imetafsiriwa)

Kwa kushirikiana na umbile la Kiyahudi na uhali wake, vikosi vya Mamlaka ya kihalifu ya Palestina (PA) huko Nablus, jana usiku, tarehe 9/19/2022, walitekeleza uhalifu wao mbaya wa kumuua kijana Firas Yaish na kuwajeruhi wengine kadhaa, wakati wa uwakandamizaji wao wa waandamanaji wanaopinga kukamatwa kwa Mujahidina Musab Shtayyeh na Brigedia Jenerali Tabila ambao wanatafutwa na umbile la Kiyahudi wakati huo huo vikosi vya uvamizi vilikuwa vikikamata watu katika miji ya Ukingo wa Magharibi, na walowezi walikuwa wakivamia Mji wa Mkongwe wa Hebron wakiwa na ulinzi wa jeshi lao. Chomb cha PA kilikuwa kikitekeleza dori yao ya kufedhehesha, ya udanganyifu, na chafu walilokabidhiwa katika kuwaandama mujahidina na kuwaua watoto wa Palestina.

Mamlaka ya Palestina yalijitolea jinai yake kwa kulitumikia umbile la Kiyahudi kukataa udhaifu wake na kushindwa kutekeleza dori yake katika kulinda usalama wake, na kwa Hussein al-Sheikh, Majed Faraj na Ziad Hab al-Rih kuthibitisha kwamba wako tayari kutumia huduma za usalama kwa kazi zote chafu kwa niaba ya uvamizi.

Kwa upande mwingine, vyombo vya PA ni viziwi, mabubu na vipofu wa mauaji, mashambulizi, na uhalifu wa kila siku huko Jenin, Nablus na miji mingine yote ya Palestina yanayotekelezwa na umbile la Kiyahudi. Na kwa sababu hawana heshima wala uungwana, hawakukerwa na mauaji ya mashujaa na kupigwa mabomu na kubomolewa nyumba wakazi wao!

Kuielezea Mamlaka ya Palestina kuwa ni mzigo kwa watu wa Palestina sio maelezo sahihi tena, bali imekuwa ni njama hatari na yenye maangamivu kwa kadhia ya Palestina. PA imelenga maisha ya watu kupitia sera zake za kiuchumi zinazofukarisha watu, imefanya kazi katika kutekeleza sera za ushuru ili kufadhili ufisadi wake na kudumisha usalama wa umbile la Kiyahudi. Mamlaka ya Palestina imefungua milango wazi kwa sheria za taasisi na shughuli za ufisadi na kwa sheria zilizoingilia moja kwa moja chombo cha familia. Pia imedhamiria kuwatia nguvuni wale wanaoendeleza ulinganizi wa mema na ukatazaji maovu na wale wote wanaotahadharisha watu kuhusu njama za kikoloni za Kimagharibi. Mamlaka ya Palestina ni mradi wa kuisalimisha kwa haraka na kuibomoa kadhia ya Palestina na hii ndio iliyokuwa misheni yake tangu kutiwa saini kwa Makubaliano ya Oslo hadi sasa. Imefanya kazi na bado inafanya kazi kuvunja utashi wa watu na kuitokomeza nafsi yoyote ambayo bado ina fahari na hamu ya kupambana. Pia inafanya kazi ya kuzima moto wa jihad na upinzani kwa mvamizi, huku ikiwapotosha watu katika mpango wake wa kupata dola dhalilifu kwa mujibu wa azimio la Marekani la dola mbili na kila mtu anajua kwamba haya ni mangati ya udanganyifu.

Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: Mamlaka ya Palestina na viongozi wake sio sehemu ya lengo lenu bali ya ni adui yenu. Yale ambayo umbile la Kiyahudi imepata kupitia Mamlaka ya Palestina yasingewezekana bila ya usaliti na njama zake. Misheni yake ni kutokomeza ari ya mapambano ndani yenu na kuangamiza familia zenu ili Mayahudi wanyakuzi waishi kwa usalama katika ardhi hii iliyobarikiwa.

Kwa damu tukufu inayomwagwa na umbile la Kiyahudi kila siku nchini Palestina, imedhihirika wazi kwamba PA inafanya kazi kwa maslahi yake binafsi, na sio kwa maslahi yenu au ya lengo lenu.

Usaliti wa utawala wa Palestina na tawala zote zinazouzunguka na pia wale walio mbali nao umedhihirika.

Mbele ya ukweli wote huu, imebakia njia moja tu ya wokovu ambayo ni kuunganisha taifa na lengo lake na kufanya kazi ya kuregesha Khilafah inayounganisha Ummah na kuling'oa umbile la Kiyahudi na tawala zote zinazolilinda. Hapo ndipo hadhi, usalama na dini vitahifadhiwa, Palestina itakombolewa na Al-Aqsa itaregea kwa wamiliki wake halali, kwa Umma wa Kiislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu