Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  18 Rabi' I 1444 Na: BN/S 1444 / 04
M.  Ijumaa, 14 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tangazo la Algiers... Umakinishaji wa Orodha za Mamlaka Zilizoharibika, Kung'ang'ania Udanganyifu, na Jitihada ya Kufufua Shirika Linalopaswa Kuzikwa
(Imetafsiriwa)

Huku mashambulizi ya umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina yakizidi, mauaji, kuzingira na kunyanyasa, na huku makundi ya walowezi yakiharibu na kuwashambulia watu, na uvamizi wao kwa Al-Aqsa umeongezeka kwa kasi na ujeuri, na huku watu wa Palestina na watoto wao wakikabiliana na umbile la Kiyahudi kwa uthabiti, ushujaa, na ujasiri wote, makundi yanakusanyika nchini Algeria chini ya usimamizi wa serikali ya Algeria kutia saini makubaliano mapya ya maridhiano chini ya jina “Tangazo la Algiers!”

Yaliyoafikiwa na kutiwa saini nchini Algeria hayakuwa kwa upande wa makundi bali ni mwendelezo wa usimamizi wa kipuuzi, na mtazamo mbovu uliopelekea kadhia ya Palestina na watu wake kupata shida, hasara na kuzorota, na kwamba watu wa Palestina hawalipatii uzito tukio lililotajwa hapo juu la kuchosha au linalojirudia rudia, na kutokana na hilo makubaliano ya maridhiano yaliyotajwa hapo juu hayana chochote zaidi ya majaribio ya kuunda upya orodha zilizomomonyoka za mamlaka zilizotokana na Makubaliano ya Oslo na kufufua maiti kama vile Baraza la Kitaifa, na Shirika la Ukombozi, ambayo kwa asili yake, wasifu, pesa na uwepo wake si chochote isipokuwa maafa kwa Palestina na lengo lake na ishara ya kujisalimisha, kuakhirisha na usaliti, na ambayo, kwa kudai haki ya kipekee ya kuwawakilisha watu wa Palestina, imewatenganisha na Ummah wao na kulitupa lengo ndani ya shimo la wahalifu wa kikoloni miongoni mwa dola kubwa!

Mgawanyiko unaojadiliwa hivi sasa kwa hakika uko karibu zaidi na mgawanyiko wa makundi kutoka kwa watu wa Palestina kuliko mgawanyiko wa makundi wao kwa wao, kwa sababu watu wa Palestina wameunganishwa katika mtazamo wao juu ya adui yao, na wameungana katika msimamo wao wa kukataa kuiacha Palestina, na wa uhaini na uratibu na umbile la Kiyahudi. Wameungana katika mapenzi yao kwa mashujaa wa watoto wao wa kiume, mashahidi wao, mama zao na Aqsa yao, na wameungana katika mtazamo wao wa upuuzi wa udanganyifu unaoitwa jumuiya ya kimataifa na sheria za kimataifa, hasa kwamba makundi haya yaliyokusanyika yameunganishwa tu na nia yao ya kupanga upya nafasi zao kulingana na maslahi yao, na kujiunga kwao chini ya mfumo wa mamlaka na shirika ndani ya dori yake ya khiyana na mfumo na misheni yake zilizoamriwa zilizoainishwa na dola zake kuu za kikoloni.

Hatimaye, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

(وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا)  

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Ali-Imraan: 103]. Na kwa hivyo kuzungumzia kuhusu upuuzi wa mikataba yenye msingi wa kufufua taasisi ambazo zama zake zinapaswa kuzikwa haimaanishi kuwa mbadala wake lazima uwe ni kuendelea kwa mzozo ambao kichocheo chake ni watu wa Palestina na watoto wao. Ni dhahiri kwamba kila Muislamu ni haramu kwa Muislamu mwingine. Damu yake, mali yake, heshima yake, kukata kwake mafungamano ya kizazi, na kujitenga naye. Kwa hakika, maana yake ni kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu na sheria zake na mtazamo wake wa masuala, na kwamba mtazamo unapaswa kuunganishwa juu ya yale yanayoruhusiwa na kukatazwa na Mwenyezi Mungu na yanayotakiwa na kamba ya Mwenyezi Mungu na Uislamu kutoka kwa mtazamo wa maisha na masuluhisho, ikiwa ni pamoja na kukataliwa kwa kila khiyana na maafikiano na kila njia ya kutumia sheria za kimataifa zilizowekwa na wahalifu wakubwa kutoka katika nchi kubwa ili kuasisi umbile la Kiyahudi kama ilivyo suluhisho la dola mbili la Marekani, na pia inajumuisha kuukabili Ummah kwa kuzipita tawala zake za njama - ikiwemo utawala wa Algeria - na ambao hamu yao pekee ni kufutwa kwa kadhia ya Palestina, na kuhutubia nguvu na majeshi ya Ummah ili kuyashikisha jukumu la ukombozi wa Palestina, watu wake, na Aqsa kwani ni wajibu wa kisheria juu ya shingo za Waislamu wote, badala ya kuwapa mgongo katika hali ya unyonge na kuzorota, kama ilivyo kwa mamlaka na makundi. Wito wa haki kwa Umma na mwamko wake ndio unaofaa zaidi, uliothabiti zaidi, na ulio muhimu zaidi kwa ajili ya ushindi wa Mwenyezi Mungu kuliko wito wa batili, udanganyifu wake, na sheria zake za kimataifa. Maridhiano elfu moja na mapatano elfu moja hayabadili hali na kadhia ya watu wa Palestina hadi mtazamo na fahamu zibadilishwe na kuregeshwa kwa msingi wa Uislamu.

(إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ)  

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar-Ra‘ad:11] Kuzorota kutabakia maadamu njia iliyo nyooka ya Mwenyezi Mungu (swt) haifuatwi.

(وأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيماً فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)

“Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” [Al-An‘am: 153]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu