Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  16 Rabi' II 1442 Na: 1442/04
M.  Jumanne, 01 Disemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Kimeandaa Kisimamo cha Kupinga

Mbele ya Baraza la Mawaziri na Kukabidhi Barua ya Wazi kwa Afisi ya Waziri Mkuu

(Imetafsiriwa)

Kwa neema ya Mwenyezi Mungu (swt), kisimamo kilicho pangwa na kitengo cha wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kilifanyika, na kina dada walioshiriki walipanga foleni na kubeba miito ya kulaani utiaji saini Mkataba wa Kiafrika juu ya Haki za Mtoto, ambapo iliandikwa kwenye mabango: (Achaneni na usekula, na simamisheni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume - Ulinzi wa mtoto utapatikana kwa kutabikishwa sheria ya Mwenyezi Mungu sio kwa sheria zilizoundwa na wanadamu - Ndio kwa Khilafah mlinzi wa boma la Uislamu na hukmu zake - Wanataka tuwalee watoto wetu kwa hadhara ya Magharibi, ili watutie kwenye nyumba za wazee!! Watoto wetu ni mstari mwekundu), na miito mingine inayotaka kuhukumu kwa Uislamu chini ya kivuli cha Khilafah Rashida kwa njia ya utume.

Halafu ujumbe uliohusisha na kina dada wawili walikabidhi barua hiyo ya wazi kwa Afisi ya Waziri Mkuu kwa anwani: "Barua ya wazi kutoka Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan hadi Serikali ya Mpito ... Jinsi gani uduni wenu umewafikisha kumfungulia mkoloni kafiri ngome ya mwisho ya Waislamu; Familia?!", Tumevua yafuatayo kutokana nayo:

Hakik sisi katika Kitengo cha wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunazikataa sheria hizi zilizo jengwa juu ya msingi wa hadhara ya Kimagharibi, na tunatoa wito wa kuhamasishwa kwa nishati za Waislamu, watu huru wanawake na wanaume, kufanya kazi kukomesha usaliti wa watawala hawa kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume inayowaingiza Waislamu na watu wote katika kumtii Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ]

“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” [Al-Baqara: 208].

Na tunaweka wazi ukweli ufuatao:

Kwanza: Hakika hadhara ya Kimagharibi; pamoja na mfumo wake ya kirasilimali, ndiyo iliyourithisha ulimwengu wa leo mateso haya yasiyo na kikomo. Sheria za familia na watoto ndizo zilizowafanya zaidi ya asilimia 70 ya watu huko Magharibi watoto wa zinaa na mahusiano haramu, na kuzaa vijana wa kiume na wa kike ambao ni wenye kuwaasi wazazi na walimu wao, na kuwaunda wanaume na wanawake ambao wanaweka baba zao na mama zao katika nyumba za wazee! ....

Pili: Mtoto wa Magharibi ni mwathiriwa wa kutengana kwa familia, na kutosheleza kwa wazazi matamanio, ambayo kukosekana kwake kunasababisha utundu, uhalifu, dawa za kulevya, na kuporomoka kwa maadili, na hakuhifadhiwa na maoni ya uhuru kwa sababu ni janga, wala sheria za hadhara ya Magharibi kwa sababu ni za uongo. Ama mtoto katika nchi yetu, yeye ni mwathiriwa wa umaskini ambao husababisha ukosefu wa elimu, ukosefu wa makazi, na kuchukua silaha pamoja na makundi ya kisilaha. Lakini ni nani aliye sababisha umasikini katika nchi yetu iliyojaa utajiri wa mali na ni nani aliyeua masikini? Na ni nani anayesukuma silaha kwa waasi ili kuweka mikono yao kwenye utajiri wa nchi? Je! Wao sio Makafiri wa kikoloni wanaotanguliwa na watawala vibaraka?!

Tatu: Itikadi ya Kiislamu ndio msingi wa maisha ya Waislamu katika sheria na kanuni zao, na inapingana kwa msingi wake na maelezo yake hadhara ya kikafiri ya Kimagharibi, ikiwemo Mkataba wa Mtoto wa Kiafrika, mgongano kamilifu unaomithilishwa na yafuatayo:

Kila mtu aliyefikia hatua ya kubaleghe, mwanamume au mwanamke, hachukuliwi kuwa ni mtoto, tofauti na Mkataba wa Kiafrika, ambao unazingatia kila mtu chini ya umri wa miaka 18 kama mtoto. Watu mashuhuri katika Uislamu ambao walikuzwa kwa Qur'an na Sunnah Tukufu, na kumfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kiigizo chao ni watu imara, wabunifu na watukufu katika kufikiria kwao na hamu yao ni maendeleo na utulivu, lakini Magharibi, kwa sababu ya fikra finyo, mtu hawajibika na hajali kwanza wakati wa utoto wake na ujana wake.

Uislamu unaruhusu uchumba na ndoa chini ya umri wa miaka 18 wakati ambapo mkataba huu unakataza hilo na ni batili. Uislamu unatafuta ghariza kwa njia ya halali, na unaharamisha mahusiano ya kimapenzi baina ya watoto na watu wengine, na kile kilichoenea Magharibi cha kutengana ni kwa sababu ya kile kilichoelezwa katika Mkataba huu)...

Sisi hatutarajii majibu kutoka kwa serikali hii inayowatii Wamagharibi makafiri, kwani sauti ya Uislamu imefikia kukataa aina zote mbaya za ukoloni, pamoja na Mkataba huu wa Kiafrika wa Haki za Mtoto, na tuna hakika kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mshindi wa dini yake, ahadi ambayo haipaswi kukataliwa, na bishara njema ya Mtume (saw), ambayo wakati wake umewadia wa kuitimiza. Na tunaendelea kufichua khiyana ya watawala hawa, hadi Mwenyezi Mungu ashukishe Nusra Yake kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili wanadamu waepushwe kutokana na maovu ya nchi za kirasilimali za Magharibi na wenzao watawala vibaraka.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu