Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 16 Rabi' II 1442 | Na: 1442/03 |
M. Jumanne, 01 Disemba 2020 |
Barua ya Wazi
Kutoka kwa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
hadi kwa Serikali ya Mpito
Jinsi Gani Uduni Wenu Umekufikisheni Kumfungulia Kafiri Mkoloni Ngome ya Mwisho ya Uislamu; Familia?!
(Imetafsiriwa)
Kwa kutia saini Baraza la Mawaziri juu ya kuondolewa vipingamizi vya hapo awali kwa Mkataba wa Afrika juu ya Haki na Ustawi wa Mtoto; Ambao umejengwa juu ya hadhara ya Kimagharibi; Hadhara ya uzinifu, kutengana, na uasi, serikali ya mpito imefungua kabla ya mkoloni kafiri Magharibi ngome ya mwisho ambayo ilibakia haiwezi kushindwa kwa hadhara yake ulioharibiwa; Familia ambayo kwayo inakaribia zaidi kwa kafiri huyo wa kikoloni, na serikali ya mpito ambayo imekuwa, tangu kuanzishwa kwake, ikiunganisha chumo lake, usalama, maisha, na kifo kwa mabwana wake makafiri!
Hakika sisi katika Kitengo cha wanawake cha Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan tunazikataa sheria hizi zilizo jengwa juu ya msingi wa hadhara ya Kimagharibi, na tunatoa wito wa kuhamasishwa kwa nishati za Waislamu, watu huru wanawake na wanaume, kufanya kazi kukomesha usaliti wa watawala hawa kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume inayowaingiza Waislamu na watu wote katika kumtii Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:
]يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ]
“Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi.” [Al-Baqara: 208].
Na tunaweka wazi ukweli ufuatao:
Kwanza: Hakika hadhara ya Kimagharibi; pamoja na mfumo wake ya kirasilimali, ndiyo iliyourithisha ulimwengu wa leo mateso haya yasiyo na kikomo. Sheria za familia na watoto ndizo zilizowafanya zaidi ya asilimia 70 ya watu huko Magharibi watoto wa zinaa na mahusiano haramu, na kuzaa vijana wa kiume na wa kike ambao ni wenye kuwaasi wazazi na walimu wao, na kuwaunda wanaume na wanawake ambao wanaweka baba zao na mama zao katika nyumba za wazee! Je, hii ndio hadhara ambayo mtu mwenye akili timamu ataichukua kama kiigizo chema?!
Pili: Mtoto wa Magharibi ni mwathiriwa wa kutengana kwa familia, na kutosheleza kwa wazazi matamanio, ambayo kukosekana kwake kunasababisha utundu, uhalifu, dawa za kulevya, na kuporomoka kwa maadili, na hakuhifadhiwa na maoni ya uhuru kwa sababu ni janga, wala sheria za hadhara ya Magharibi kwa sababu ni za uongo. Ama mtoto katika nchi yetu, yeye ni mwathiriwa wa umaskini ambao husababisha ukosefu wa elimu, ukosefu wa makazi, na kuchukua silaha pamoja na makundi ya kisilaha. Lakini ni nani aliye sababisha umasikini katika nchi yetu iliyojaa utajiri wa mali na ni nani aliyeua masikini? Na ni nani anayesukuma silaha kwa waasi ili kuweka mikono yao kwenye utajiri wa nchi? Je! Wao sio Makafiri wa kikoloni wanaotanguliwa na watawala vibaraka?!
Tatu: Itikadi ya Kiislamu ndio msingi wa maisha ya Waislamu katika sheria na kanuni zao, na inapingana kwa msingi wake na maelezo yake hadhara ya kikafiri ya Kimagharibi, ikiwemo Mkataba wa Mtoto wa Kiafrika, mgongano kamilifu unaomithilishwa na yafuatayo:
Kila mtu aliyefikia hatua ya kubaleghe, mwanamume au mwanamke, hachukuliwi kuwa ni mtoto, tofauti na Mkataba wa Kiafrika, ambao unazingatia kila mtu chini ya umri wa miaka 18 kama mtoto. Watu mashuhuri katika Uislamu ambao walikuzwa kwa Qur'an na Sunnah Tukufu, na kumfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kiigizo chao ni watu imara, wabunifu na watukufu katika kufikiria kwao na hamu yao ni maendeleo na utulivu, lakini Magharibi, kwa sababu ya fikra finyo, mtu hawajibika na hajali kwanza wakati wa utoto wake na ujana wake.
Uislamu unaruhusu uchumba na ndoa chini ya umri wa miaka 18 wakati ambapo mkataba huu unakataza hilo na ni batili. Uislamu unatafuta ghariza kwa njia ya halali, na unaharamisha mahusiano ya kimapenzi baina ya watoto na watu wengine, na kile kilichoenea Magharibi cha kutengana ni kwa sababu ya kile kilichoelezwa katika Mkataba huu.
Mkataba huu inakataza adhabu ya viboko kwa mtoto, wakati Uislamu unaelekeza utumiaji wa adhabu nyepesi kwa mtoto wa miaka 10. Uislamu pia unahakikishia haki ya nidhamu na sio kulipiza kisasi, kwa mujibu wa kanuni za Sharia, na kutoa adhabu ya mwili kwa wazazi na walimu, na hivyo kuzuia shida za uasi na uonevu, kubeba silaha, na uzembe wa Vijana na wasichana, na ufisadi wao, kama inavyotokea Magharibi.
Yeyote anayefikia baleghe sio mtoto, bali ni mtu mzima, na haadhibiwi hata shuleni isipokuwa kwa uamuzi wa korti, ambao unaonyesha kuwa sheria hizi ni za kubomoa familia nchini Sudan na sio za kuijenga! Je! Sio wakati sasa ambapo mlango umekuwa wazi kwa watoto kuchukua hatua bila vizuizi au vidhibiti nyumbani, jamii na hata serikalini?
Hii ni chembe tu ya jabali kuu la hukmu zilizo teremshwa kwa Wahyi,
[أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ]
“Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?”]Al-Mulk: 14[.
Hii ni mifano ya hukmu za Uislamu ambazo Hizb ut-Tahrir inataka kuzitekeleza kwa uhalisia, kuleta furaha, utulivu na usalama kwa ulimwengu uliorithishwa na hadhara ya Kimagharibi mateso, kutokuwa na furaha, wasiwasi, na machafuko, ili tuishi kwa kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufanya kazi ya kusimamisha tena maisha ya Kiislamu. Kusimamisha Khilafah Rashida ya kwa njia ya Utume.
Ee Serikali ya Mpito:
Enyi watoto wa Waislamu mnaohusika na utiifu kwa Magharibi kafiri:
Je! Hampati funzo la kifo ambacho huwanyakua wafalme na watu wanaowazungukeni, ili mtambue ukuu wa Mwenyezi Mungu, na ulazima wa kuingia katika utii Wake, na kukataa kumuasi Kwake? Je! Humjifunzi kutokana na uhalisia wa vibaraka ambao walikuwa waaminifu katika utiifu kwa Magharibi na kuishia kukaa makaburini au magerezani? Kwa hivyo rudini kwenye akili zenu, na muingie katika kumtii Mola wenu, kwani kurudi kwenye haki ni fadhila, ondoeni mikono yenu kutoka katika uasi, na kabidhini utawala kwa wale ambao wanaweza kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya utume.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].
Msemaji Rasmi wa Kike wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: |