Jumapili, 05 Rajab 1446 | 2025/01/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  24 Jumada II 1442 Na: HTS 1442 / 47
M.  Jumamosi, 06 Februari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amali za Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Zawakasirisha Maadui wa Uislamu, Hivyo Basi Kudhamiria Kudanganya na Kupotosha
(Imetafsiriwa)

Wanaharakati walisambaza kwenye mitandao ya kijamii video ya kikundi kimoja cha Mashababu wa Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan mjini Gadharif. Wale walioisambaza video hiyo walidai kuwa wao ni kikundi kinachojiita Harakati ya Ukombozi wa Ummah wa Kiislamu miongoni mwa Watawala na kunyanyua mabango yanayotaka uteuzi wa Amir mmoja wa Ummah wa Kiislamu, na bendera nyeusi na nyeupe zilizoandikwa juu yake: La Ilaha Illa Allah Muhammadun Rasulullah. Video hiyo iko ubavuni mwa ghala la nafaka katika mji wa Gedaref.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah of Sudan, na kuhusiana na video hii, tunaweka wazi uhakika ufuatao:

Kwanza: Mtu aliyepiga video hiyo na kuripoti habari hizo ni mwongo; kwa sababu video ambazo ndani yake mna mashababu, hubeba nembo ilioandikwa juu yake Hizb ut-Tahrir, na ikiwa alikuwa na shaka, angekuwa amewauliza mashabab ili ajue hao ni kina nani, lakini aliwatambulisha kwamba kundi hili alilolipiga video ni wanachama wa Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan - Gadharif.

Pili: Mtu huyu aliyepiga video na kuchapisha video hiyo wazi ana kusudi baya pindi anaposema kwamba wao ni kikundi kinachojiita Harakati ya Ukombozi wa Ummah wa Kiislamu kutoka miongoni mwa Watawala, na ule uletaji taswira wake kwamba wanabeba bendera nyeusi na nyeupe zilizoandikwa ndani yake: La Ilaha Illa Allah Muhammadun Rasulullah.

Tatu: Kwa wale wanaojua na wale wasiojua, bendera zilizochapishwa kwenye video hiyo ni nyeusi, yaani bendera ya Uqab, na nyeupe, ambayo ni Liwaa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kutoka kwa Ibn Abbas (ra) alisema:

«كَانَتْ رَايَتُهُ سَوْدَاءَ وَلِوَاؤُهُ أَبْيَضَ»

"Raya yake ilikuwa ni nyeusi, na Liwaa yake ilikuwa ni nyeupe." [Imepokewa na Tirmidhi].

Nne: Shughuli za Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan katika maeneo yote ya Sudan zinajulikana na kila mtu isipokuwa kwa macho ambayo yana ugonjwa wa kiwambo ndiyo yanayoweza kuzifananisha kimakosa na watu wengine. Na amali za mashabab wa Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan mjini Gadharif zinajulikana na watu wa Gadharif, wao ni watoto wa Gadharif, na hatufikiri kwamba kuna mtu yeyote wa Gadharif ambaye haijui Hizb ut-Tahrir na mashabab wake, kwa hivyo nyumba ya Hizb iko wazi asubuhi na jioni katika kitongoji cha Dim Hamad, na shughuli za nyumba hiyo na vikao vyake vinajulikana kwa wote.

Kwa kuhitimisha: Tunawaambia wale wanaokasirishwa na shughuli ya Hizb ut-Tahrir / Wilayah ya Sudan kwamba fanyeni mtakavyofanya, hamtapata chochote ila fedheha hapa duniani na adhabu kesho Akhera; Ikiwa hamrudi kwenye haki na kubeba ulinganizi pamoja na Hizb ut-Tahrir ili kuukomboa Ummah kutokana na nidhamu za kikafiri za kirasilimali na fikra zake potofu, basi wengi kabla yenu wamejaribu kufuata njia hii na kutofaulu na fedheha ndiyo iliyokuwa hatima yao. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ)

“Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukana mema.” [Hajj:38].   

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu