Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  26 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: HTS 1442 / 77
M.  Jumatano, 07 Julai 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Nchi za Troika Zakiuka Ubwana wa Nchi Hii na Kupelekea katika Kuvunjika Vunjika Zaidi
(Imetafsiriwa)

Wajumbe wa nchi za Troika, na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, walimaliza mazungumzo na mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Watu-Kaskazini (SPLM-N) Abdelaziz El-Hilu, katika ngome ya uongozi wa harakati hiyo. huko Kauda, Kordofan Kusini. Taarifa ya wajumbe wanaowakilisha Uingereza, Amerika, na Norway ilisema kwamba mikutano ilifanyika na El-Hilu kwa siku mbili, ili kumshajiisha kuendeleza maelewano yaliyofikiwa katika Azimio la Kanuni lililotiwa sahihi na serikali ya Sudan jijini Juba tarehe 28 Machi. Taarifa hiyo ilipongeza juhudi za pande hizo mbili kufikia makubaliano ya amani, na kusisitiza kwamba Azimio la Kanuni "ambalo linaonyesha kuwa inawezekana kusonga mbele juu ya maswala muhimu kama kutenganisha dola na dini." (Sudan Tribune 4/7/2021).

Nchi hii imekuwa mbaya, ambapo ujasusi na ujumbe wa kigeni wa nchi za kikoloni huzunguka. Wanakutana na yeyote wanayemtaka, kupanga na kula njama dhidi ya watu wa Sudan. Nchi hizi ndio nchi zile zile zilizoitenganisha kusini, na kuutambua uongozi wa serikali uliyoitenganisha kusini, kama ilivyosemwa na mkuu wa serikali iliyokuwepo wakati huo kwa wavuti ya Sputnik wa Urusi, mnamo 21/11/2017, ambapo alisema: "Sudan inakabiliwa na shinikizo kubwa na njama kutoka Amerika, na kesi za Darfur na Sudan Kusini zimepata usaidizi na uungwaji mkono kutoka Amerika, na chini ya shinikizo lake, Sudan Kusini imetenganishwa, ambayo inamaanisha kuwa Sudan iligawanywa. Tuna habari kwamba azma ya Amerika ni kuigawanya Sudan kuwa nchi tano. Na sasa pande zizo hizo zinainyemelea Sudan kutoka milango ya Kordofan Kusini, Nile na Blue Nile.

Kuingilia kati kwa nchi hizi za kikoloni chini ya usimamizi na mapendekezo yao, na serikali kutokuwa na uwezo wa kuchukua hatua yoyote, inathibitisha kwamba mfumo wa kisekula hauna umeshindwa kutatua matatizo ya watu, na vile vile umeshindwa kuwayeyusha ndani ya kinu kimoja, kwani ni serikali ya ovu yenye kuwafukarisha watu, kuirarua nchi vipande vipande kwa fikra za uhuru wa kujitawala, shirikisho, na haki ya kujiamulia. Kauli za maafisa hawa wakati wa ziara hii zinathibitisha lengo chafu ambalo wanataka kulifikia dhidi ya Uislamu; dini ya idadi ya watu wengi wa Sudan, "Taarifa hiyo ilipongeza juhudi za pande hizo mbili za kufikia makubaliano ya amani, na kusisitiza kwamba Azimio la Kanuni linaonyesha kuwa inawezekana kusonga mbele katika maswala muhimu kama utenganishaji dola na dini."

Nchi za Troika zinakiuka ubwana wa nchi hii, na hata zinashajiisha harakati za Wananchi kusonga mbele katika kushikamana na masharti yake yenye kulingania usekula, na kuvunjwa vunjwa kwa nchi hii kupitia haki ya kujiamulia au kujitawala, kwani ni nchi hizi ndizo zilizoshirikiana awali katika kuitenganisha kusini.

Ilikuja katika taarifa hiyo: "Taarifa ya wajumbe ... ilisema kwamba mikutano ilifanyika na El-Hilu kwa siku mbili, ili kumshajiisha aendeleze maelewano yaliyofikiwa katika Azimio la Kanuni lililotiwa sahihi na serikali ya Sudan jijini Juba tarehe 28 Machi ”. Jambo la hatari zaidi na la kushangaza ni kwamba masuala haya ni ya ndani, kwa hivyo nchi hizi zina uhusiano gani nayo? Jambo linalothibitisha kuwa bado wanafanya uangalizi na usimamizi wa kikoloni juu ya serikali hizi dhaifu ambazo walianzisha na kuzisaidia kupitia balozi zao za kigeni, ambazo ni viota vya uovu na njama dhidi ya watu wa nchi hii.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan daima tumekuwa tukiwaonya watu wa Sudan juu ya njama zinazopangwa dhidi yao kuisambaratisha nchi hii na kuupiga vita Uislamu, na hili lilithibitishwa na taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov mnamo Jumatano tarehe 12/4/2017, wakati wa mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Amerika Rex Tillerson, kwamba "utawala wa Obama uliitaka serikali ya Omar Al-Bashir kukubali kuigawanya Sudan hadi sehemu mbili ili kumaliza tatizo lake kwa badali ya kutompeleka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.” Jibu la Waziri wa Mambo ya Nje Ibrahim Ghandour siku iliyofuata, Alhamisi, 13 Aprili 2017, lilikuwa la kushangaza, kwani alithibitisha njama hii, akisema: "Kutenganishwa kwa kusini kimsingi ilikuwa ni njama, Lakini tuliikubali!" (Anadolu Agency 13/4/2017).

Ndio, nchi hizi zitaendelea kula njama, kupanga njama, kudanganya, na kufanya mipango machafu ya kuvunja azma yetu, ili tusiwe na mpango wa kuunda dola madhubuti inayosimamisha Uislamu na kutekeleza sheria yake. Kwa hivyo, watu wa Sudan wanapaswa kufahamu kile kinachopangwa dhidi yao kupitia dola hizi za kikoloni zenye chuki na Uislamu, na kuunga mkono mradi wa Uislamu mtukufu na dola yake, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwani ndio pekee inayokata mikono ya wakoloni na kuzuia uovu wao na njama zao. Na siku hiyo Waumini watafurahia ushindi wa Mwenyezi Mungu.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu