Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  18 Rabi' II 1444 Na: HTS 1444 / 12
M.  Jumamosi, 12 Novemba 2022

 Majibu ya Habari
(Imetafsiriwa)

Ndugu Mheshimiwa, Mhariri wa Gazeti la Al-Sudani,

Assalam Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Mada: Hizb ut Tahrir ni Chama cha Kisiasa Kisichofanya Vitendo vya Kisilaha

Sio kwa Kumuogopa Yeyote, lakini kwa Kufuata Mfano wa Mtume (saw)

Tulipitia ripoti yenye kichwa: “Wahubiri, Watu Wenye Msimamo Mkali, na Makundi ya Kidini Watuma Barua za Vitisho kwa Balozi wa Marekani jijini Khartoum... “Ni Mabomu Yaliyonaswa” Yanayozunguka kuelekea Ubalozi wa Washington huko Soba!” katika Gazeti lenu la Al-Sudani, Toleo la 5799, la Jumamosi, tarehe 18 Rabi' al-Akhir 1444 H sawia na 12 Novemba 2022, iliyoandikwa na mwandishi wa habari Al-Hadi Muhammad Al-Amin, katika ripoti hiyo yote, alijaribu kuonyesha kwa wasomaji kwamba Hizb ut Tahrir ni miongoni mwa makundi ya kijihadi yanayotekeleza vitendo vya kisilaha. Badala yake, aliitaja hizb kuwa yenye msimamo mkali, akisema: “... ambapo miitiko ya kasi ilionekana kuelekea harakati za John Godfrey na ikaja Hizb ut Tahrir ya Kiislamu (Wilayah ya Sudan), inayoongozwa na Ibrahim Othman (Abu Khalil) ambayo iko mstari wa mbele wa vikosi vya misimamo mikali vya Sudan ... nk.”

Katika imani yetu ya kupata haki, na katika kuweka mambo sawa, tunakuomba uchapishe majibu yafuatayo kwa uzushi wa ripoti yenu, kwa mujibu wa haki yetu ya kujibu:

Kwanza: Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu, na inafanya kazi kati na pamoja na Ummah kuuchukua Uislamu kuwa ndio njia yake na kuuongoza kuiregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kuwepo.

Pili: Hizb ut Tahrir inalenga kuuamsha Ummah, mwamko sahihi, kwa fikra angavu. Kwa hivyo, kazi yake imefungika kwa mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa, na haifanyi vitendo vya kisilaha, si kwa kumuogopa yeyote, bali kwa kujitolea kwa njia ya Mtume (saw) na kufuata seera yake inayonukia katika kusimamisha dola. Kwani yeye (saw) hakufanya amali yoyote ya kisilaha kabla ya kuasisiwa dola, bali alitekeleza mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa mpaka yeye (saw) alipoisimamisha dola, na dola ndiyo inayotekeleza vitendo vya kisilaha.

Tatu: Taarifa kwa vyombo vya habari ambayo mwandishi wa ripoti hiyo aliitegemea kuzungumzia Hizb ut Tahrir haina tishio la amali yoyote ya kisilaha kwa mtu yeyote, si balozi wa Marekani wala mtu mwengine yeyote. Taarifa hiyo inawalenga watawala wa Sudan na watu wa Sudan, na kichwa chake kinatosheleza, kinachosema: “Kwa kuzingatia Udhalilifu wa Watawala wa Sudan, Balozi wa Marekani anakaimu kama Mtawala Mkuu wa Sudan”, ambapo taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inawataka watu wa Sudan kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume ambayo inachukua ubwana wa kweli juu ya nchi yao, na kukata mkono wa mkoloni kafiri juu yake, au mwandishi wa ripoti hiyo anapendelea yale ambayo balozi wa Marekani na mabalozi wengine wa nchi za kikoloni wanayafanya nchini Sudan?! Je, balozi wa Sudan nchini Marekani, au balozi wake nchini Uingereza, anaweza kusubutu kufanya ushuri tu ya yale yanayofanywa na mabalozi wa Marekani na Uingereza katika upande wa kuingilia mambo yetu?! Kwa hakika hawasubutu kwa sababu wanajua kwamba Marekani na Uingereza hazitawaruhusu kufanya hivyo ili kulinda ubwana wa nchi zao.

Kwa kumalizia: Tunamuomba Mwenyezi Mungu, Aliye juu zaidi, Mtukufu, aondoe vitimbi vya makafiri na watumishi wao katika nchi yetu na nchi za Waislamu, na atujaalie Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kama bishara njema kutoka kwa Mtume (saw) ambaye amesema:

«... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ»

“…kisha utakuwepo utawala kwa kutenza nguvu, basi utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza.” (Imepokewa na Ahmed).

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu